Tamko litolewe kukemea mwendokasi wa hizi treni.

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Ajali mbaya ya gari moshi kulambana uso kwa uso na basi linasosadikiwa kumilikwa na Magereza ya Ukonga jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea muda wa jioni siku ya Mawlid maeneo ya Ukonga ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana lakini mashuhuda wanasema Dereva[Captain] wa gari-moshi aliliona lori la Magereza likipita kwenye reli na yeye Captain wa Treni badala ya kukwepa ama kusimama akalifuata na kujigonga kwenye Basi linalosadikiwa kuwa la Magereza.

Tuwaombee Majeruhi na dereva wa treni afikishwe mahakamani kwa kuendesha kwa uzembe na kutoheshimu sheria za reli.
Kumekuwa na tabia hivi karibuni, isiyo nzuri, kwa madereva wa DART[Mwendokasi] na TRENI wawapo kwenye barabara kutokwepa Bodaboda na kutokwepa Mabasi kama haya ya Magereza na kusababisha ajali.

Maelezo zaidi Msemaji wa vyombo husika watatuletea!
 
Mwalimu aliwapa kauli kuwa Gari ndio linagonga Treni kwa hiyo ni ngumu kupewa hizo kauli kutokana na Sheria zilizowekwa kuhusu ajali za Treni...
 
Mwenye makosa hapo ni dereva wa basi la Magereza. Maana yeye ndiye aliyeligonga gari moshi kwa mbele.
 
"Captain w Treani badala ya kukwepa ..." eeh mtoa mada serious ulitegemea train "kukwepa" ?!! Kwamba kuna reli pembeni ya kukwepea ?! Au train ingeweza kupita kwenye ardhi ?!! Mkuu samahani, kuna vileo umetumia au umevuta ?!
 
Mwenye makosa hapo ni dereva wa basi
 
"Captain w Treani badala ya kukwepa ..." eeh mtoa mada serious ulitegemea train "kukwepa" ?!! Kwamba kuna reli pembeni ya kukwepea ?! Au train ingeweza kupita kwenye ardhi ?!! Mkuu samahani, kuna vileo umetumia au umevuta ?!
Nipo sober, leweni kwa "roho mtakatifu"
 
Treni ni kama mabasi ya mwendokasi yana njia yake maalumu. Kwa hio haiwezi kugonga bali inagongwa na chombo kinachotumika njia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…