Tamko litolewe kukemea mwendokasi wa hizi treni.

Ajali mbaya ya gari moshi kulambana uso kwa uso na basi linasosadikiwa kumilikwa na Magereza ya Ukonga jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea muda wa jioni siku ya Mawlid maeneo ya Ukonga ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana lakini mashuhuda wanasema Dereva[Captain] wa gari-moshi aliliona lori la Magereza likipita kwenye reli na yeye Captain wa Treni badala ya kukwepa ama kusimama akalifuata na kujigonga kwenye Basi linalosadikiwa kuwa la Magereza.

Tuwaombee Majeruhi na dereva wa treni afikishwe mahakamani kwa kuendesha kwa uzembe na kutoheshimu sheria za reli.
Kumekuwa na tabia hivi karibuni, isiyo nzuri, kwa madereva wa DART[Mwendokasi] na TRENI wawapo kwenye barabara kutokwepa Bodaboda na kutokwepa Mabasi kama haya ya Magereza na kusababisha ajali.

Maelezo zaidi Msemaji wa vyombo husika watatuletea.
View attachment 2766990View attachment 2766990
Hivi kweli kabla ya kuandika, umewaza vizuri kabisa?!! Eti treni inashindwa kukwepa gari au kusimama ghafla?? Ni kweli treni ina breki kali ila madhara yake ni makubwa sana, kwa treni na miundombinu yake.
 
kwa akili yako unaona sawa basi hilo la Magereza kugongwa na kuumia ni sawa?
Treni ingesimama kungalikuwa na shida gani?
 
mashuhuda wanasema Dereva[Captain] wa gari-moshi aliliona lori la Magereza likipita kwenye reli na yeye Captain wa Treni badala ya kukwepa ama kusimama akalifuata na kujigonga kwenye Basi linalosadikiwa kuwa la Magereza.

Tuwaombee Majeruhi na dereva wa treni afikishwe mahakamani kwa kuendesha kwa uzembe na kutoheshimu sheria za reli.
Kumekuwa na tabia hivi karibuni, isiyo nzuri, kwa madereva wa DART[Mwendokasi] na TRENI wawapo kwenye barabara kutokwepa Bodaboda na kutokwepa Mabasi kama haya ya Magereza na kusababisha ajali.

Maelezo zaidi Msemaji wa vyombo husika watatuletea.
Mkuu uko serious kweli au Unatania sasa ulitaka Treni ikwepe iende Wapi 🤣🤣🤣🤣🤣 angalia sehemu nilizoweka Red colour halafu nijibu ulikuwa serious au just a joke 🤣🤣🤣 Sada unataka treni ikwepe bodaboda iende wapi ipae au 🤣🤣🤣
 
Ajali mbaya ya gari moshi kulambana uso kwa uso na basi linasosadikiwa kumilikwa na Magereza ya Ukonga jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea muda wa jioni siku ya Mawlid maeneo ya Ukonga ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana lakini mashuhuda wanasema Dereva[Captain] wa gari-moshi aliliona lori la Magereza likipita kwenye reli na yeye Captain wa Treni badala ya kukwepa ama kusimama akalifuata na kujigonga kwenye Basi linalosadikiwa kuwa la Magereza.

Tuwaombee Majeruhi na dereva wa treni afikishwe mahakamani kwa kuendesha kwa uzembe na kutoheshimu sheria za reli.
Kumekuwa na tabia hivi karibuni, isiyo nzuri, kwa madereva wa DART[Mwendokasi] na TRENI wawapo kwenye barabara kutokwepa Bodaboda na kutokwepa Mabasi kama haya ya Magereza na kusababisha ajali.

Maelezo zaidi Msemaji wa vyombo husika watatuletea.
View attachment 2766990View attachment 2766990
Nimeelewa ulichomaanisha. Watu wanakukasirikia bure lakini ulichoandika sicho ulichomaanisha, umeandika kimafumbo. Changamoto tu ni kwamba baadhi ya watu wanafikiri ulimaamisha treni ingelikwepa basi, kumbe ni kinyume chake. Hata hivyo, wengine wamekuelewa.
 
kwa akili yako unaona sawa basi hilo la Magereza kugongwa na kuumia ni sawa?
Treni ingesimama kungalikuwa na shida gani?
Mbona jina lako na unachoandika havioani?!!! Kwani hilo gari la magereza ndio gari la kwanza kugonga treni nchi hii?!! Tena sio kuumia tu wangekufa kabisa, kwani ni uzembe wa dreva!! Yaani treni isimame ghafla unajua balaa lake litakalotokea? Kipande chote cha reli lazima king'oke, bado kama imebeba abiria au mizigo lazima kuna madhara makubwa sana yatatokea, hata kama ni injini pekee yake bado, kisa uzembe wa mtu mmoja, na sheria iko wazi,. Treni sio bajaji. Duniani kote ukijipendekeza tu lazima ufe.
 
Pale aliposema TRENI INGELIKWEPA BASI, ilitosha kuelewa kuwa alichoandika ni kinyume chake. Ameandika kimafumbo. Kwa maneno mengine, utetezi wake ni kwa treni na captain wa treni. Ndiyo kusema, kakasirishwa na "uzembe" wa dereva wa basi la Magereza.
 
Ajali hiyo imetokea muda wa jioni siku ya Mawlid maeneo ya Ukonga ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana lakini mashuhuda wanasema Dereva[Captain] wa gari-moshi aliliona lori la Magereza likipita kwenye reli na yeye Captain wa Treni badala ya kukwepa ama kusimama akalifuata na kujigonga kwenye Basi linalosadikiwa kuwa la Magereza.
Kwa maelezo hata tukuombee wewe kwanza kabla ya wahanga wa ajali
 
Dereva wa bus anatakiwa alambwe kwanza faini
Maana huko alikokuwa anapita sidhani kama ni njia ya kupita gari
 
Watu wengi hawajamwelewewa mtoa mada, hii ni kejeli kwa Magereza na wazee wa kuvunja sheria kisa wako kwenye taasisi zenye mamlaka
Mtoa mada amenikumbusha kipindi tukiwa Chuoni. Mhadhiri aliahidi kutoa mtihani mrahisi kuliko mtihani wowote aliowahi kuutunga.

Siku ya paper, kinyume na llivyozoeleka, baada ya karatasi zenye maswali kugawiwa, tuliachwa peke yetu bila msimamizi yeyote. Isitoshe, tulitangaziwa kuwa ni rukhsa kutumia simu, pc, kutazazamia kwa jirani, na hata kwenda kutafuta majibu nje, isipokuwa tu, usipige kelele.

Wengi walipoyatazama maswali, walibaini ni marahisi sana, na kwa haraka haraka, walianza kuyajibu. Hawakushangaa kwa nini waliletewa maswali mepesi, ambayo hata mwanafunzi wa Sekondari angeyajibu vizuri sana tu.

Mimi, pamoja na wachache sana, ndiyo tulionsusrika na huo mtego. Wakati wenzangu walipokuwa wakiendelea kujibu haraka haraka, Mimi nilikuwa nikisoma instructions, taratibu. Ndipo, katikakati ya instructions nilipokuta, "DO NOT ATTEMPT ANY QUESTION".

Matokeo yake, niliandika tu Namba yangu yangu na darasa na kusubiria kukusanya. Hatimaye milipata 100% wakati wenzetu wengi wakiambulia sifuri. Kila aliyejibu, alipata zero, na kila aliyefuata maelekezo, kutokujibu swali lolote, alipata asilimia mia moja.

Mtoa mada anamponda dereva wa Jeshi la Magereza, kwamba hakuzingatia sheria.

Nafikiri wengi hawajalielewa fumbo lake. Kwani yeye hajui kuwa treni haiwezi kulikwepa basi?

Ni fumbo, na amefanikiwa kuwafumba wengi waliochangia mwanzoni.
 
Nahisi mtoa mada, Jaji Mfawidhi, atakuwa anacheka tu jinsi watu wanavyobabaika na mada yake, kwamba wengi hawajaelewa alichomaanisha.

Ila inafikirisha! Inawezekanaje watu wameshindwa kuelewa fumbo jepesi kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom