carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) imekemea vitendo visivyo vya kimaadili vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya wanafunzi waliomaliza mtihani wa kidato cha nne mwaka 2026, ikiwemo kuimba nyimbo zisizofaa, kutumia lugha ya matusi na kutoa kauli za kashfa.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa Oktoba 26, 2026, TAMSYA imesema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na maadili mema, heshima na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Jumuiya hiyo imewataka wanafunzi na vijana wa Kiislamu kujiepusha na vitendo vinavyokiuka maadili ya dini, huku ikiwakumbusha kuwa kumaliza mtihani si mwisho wa wajibu wa kuzingatia maadili, bali ni hatua nyingine ya maisha inayohitaji ukomavu, hekima na uwajibikaji.
Aidha, TAMSYA imewahimiza wazazi, walezi, walimu na viongozi wa dini kuendelea kuwaongoza vijana katika misingi ya imani, nidhamu, heshima na tabia njema ili waweze kuwa viongozi bora wa baadaye na wenye manufaa kwa jamii na taifa.
TAMSYA imesisitiza kuwa uhuru wa kusherehekea mafanikio ya kielimu haupaswi kutumiwa kama sababu ya kukiuka maadili ya dini, kudhalilisha wengine au kuvunja misingi ya heshima katika jamii.
Jumuiya hiyo imehitimisha kwa kutoa wito kwa vijana kuendeleza tabia njema na kuheshimu mafundisho ya dini pamoja na misingi ya maadili katika maisha yao ya kila siku.
Chanzo : Tamsyatammsya