Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Wanawake na wanaume wengi ni wapenzi tamthilia za vipindi vya maigizo na mechi za mpira na kuwa wakati wengine hujikuta wakisalia sebuleni au kuweka umakini kwenye TV na kuacha wenza wao wakitangulia kulala peke yao au kukosa wa kuzungumza nao mambo mengine ya kimaisha
Vitendo hivyo vinafanya wanandoa wengi wajione wapweke na wakati mwingine wanaona hakuna umuhimu wa kuoa au kuolewa na mwisho hali hiyo inazalisha migogoro ambayo hatima yake ni kuvunjika kwa ndoa kwa kuwa baadhi hujiongeza kutafuta faraja nje ya ndoa zao.
Wanandoa watambue kuwa wenzao wanapenda kusikilizwa hasa wanaporudi kutoka kwenye mihangaiko ya ya kila siku, hivyo wanahitaji kufarijiwa na wenza wao sasa inapotokea mmoja kati yao anaanza kuwa na ratiba nyingine baada ya mihangaiko inawapa ugumu na kuwanyima nafasi ya kuzungumza au kuwa karibu na wenza wao.
Nashauri kuwa pamoja na kuwepo mapenzi binafsi ya vipindi vya TV bado wanandoa wanatakiwa kujua kuwa wanawajibika kupeana muda wao kwa wao bila kujali kuna vipindi gani vipo kwenye TV. Vinginevo hali hiyo isipodhibitiwa huwa chanzo ha kuharibu mahusiano mengi ya ndoa na familia kiujumla.