Tamthilia ya Jua Kali ilipaswa iishe siku nyingi

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
491
Reaction score
1,907
Kwa wale mnaofatilia tamthilia hii mtaungana nami kuwa director Lamata analazimisha kuongeza matukio ili ivutie lakini katika uhalisia ilipaswa iwe imeisha siku nyingi.

Bill kashajua mama yake ni aunt Zai, Maria na Frank kila siku vitimbi kama ilivyo femi na luka kila siku drama za kufumaniana na kuombana msamaha🚮🚮

Kule kijijini ndio washapotezea hawapaoneshi tena. Hii tamthilia wanailazimisha iendelee kuwa ndefu lakini kiuhalisia ilipaswa iwe imeshaisha maana inaanza kupoteza mvuto.
 
Isidingo ilichukua miongo kadhaa kuisha.

Muache Lamata aendelee kutengeneza pesa na vijana wa mjini wauze sura kwa jina la uigizaji.

Maana hiyo tamthilia imekuwa kimbilio la kila mwenye jina mjini haijalishi ni wa tasnia gani.

Yeyote mwenye ku trend town anapewa nafasi ya kuigiza. Tusibiri kumuona mama wa Kichaga alietoa kero za TRA nae apewe nafasi ya kuigiza humo kwenye hiyo tamthilia.
 
Tofautisha isidingo na juakali, isidingo ilihusu wakazi wa mji fulani, ilikuwa kisa ikiisha inakuja stori nyengine, yani mtu anahama, anakufa anahamia mtu mwengine, kam ilivyo katika miji halisi duniani, ila jua kali kisa ni cha wahusika haohao hata stori imeisha ila bado haohao
 
Ok
 
Kuna matukio anayavuta sana bila sababu
 
Lamata kafany story kuwa ndefu by the way ndo anatengeneza pesa[emoji24][emoji24]
 
Tofautisha isidingo na juakali, isidingo ilihusu wakazi wa mji fulani, ilikuwa kisa ikiisha inakuja stori nyengine, yani mtu anahama, anakufa anahamia mtu mwengine, kam ilivyo katika miji halisi duniani, ila jua kali kisa ni cha wahusika haohao hata stori imeisha ila bado haohao
Umeelekeza vizuri sana hapa hadi nimependa safi sana.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
ki ukweli imepoteza mvuto bora azam wao ni bandika bandua tamthiliya lazima iishe kama inavyotakiwa kisha inakuja nyingine. sasa hao dstv kwanza wanapenda kutuletea tamthiliya ambazo zinaishia njiani kapuni, sarafu,karma na nyingine..sasa jua kali waliona watu wameipenda sana sasa hawataki iishe mpaka story imepoteza mvuto si wangeimailiza tuu hiyo story wakaja na story nyingine ndefu
 
Inshort ile channel ya 160 inaonesha Tamthilia za kibongo ni Channel inayoonesha ni jinsi gani Tanzania hatupangi mambo yetu yakaisha. Sijui kama kuna Tamthilia iliisha pale.

Ya wema ilikatishwa,ikaja La Familia hii ndo ya kipuuzi sijawahi ona,ya kichawi na mchawi anaringishia wali mateka wake yaani acha tu. Afu pia ilikatishwa ikaqnza tena.

Imekuja Yalaiti ikakatishwa afu ikaanza tena.

Kaja huyu Lamata, ni nzuri sana ila imeanza kuchosha sababu asili yetu binadamu nikuchoka tunapotazama watu wale wale kila siku. Afanye mpngo iishe aje na nyingine maana kaonesha uwezo anao.
 
Isidingo ilichukua miongo kadhaa kuisha.

Muache Lamata aendelee kutengeneza pesa na vijana wa mjini wauze sura kwa jina la uigizaji.

Maana hiyo tamthilia imekuwa kimbilio la kila mwenye jina mjini haijalishi ni wa tasnia gani.

Yeyote mwenye ku trend town anapewa nafasi ya kuigiza. Tusibiri kumuona mama wa Kichaga alietoa kero za TRA nae apewe nafasi ya kuigiza humo kwenye hiyo tamthilia.
Mbona tayari ashapewa "pointment' na Lamata!🤣🤣🤣🤣!!!
 
Back
Top Bottom