Tamthilia ya Zahanati Kijijini

Si mpenz wa bongo movie,niliikuta wanaitizama nami nikajikuta naitizama, iko poa saana...

Bongo waigizaji ni wachache mnoo wengi si wazuri hawajui kuuvaa uhusika, mtu unaona kabisa huyu anaigiza,habebi uke uhusika.. ila yule mama ambae zamani alikuwa mama nyamayao na kibakuli yuko vizuri mnoo, haimbwi lakini ni moja kati ya waigizaji bora tz.. kwenye zahanati sijui anatumia jina gani mwanae mguu wake mmoja ni mbovu.
Wengi wamejitahidi kubeba uhusika na ndio maana inaonekana ni nzuri.
 
Mimi hata siipendi 😃😃😃 naona ni preference

Mie maybe Fungu Langu, Kosa Moja na ile mpya Mwanamziki

Mie tamthiliya inayoonyesha dhiki kila saa hapana yaan plot yake imebase mazingira duni akaa mie 😂😂😂😂😂
 
Hata kama sanaa 😂😂😂ndo bi ubwa akafue na kuoga choo cha wanaume😂😂😂yan wale wanafurahisha sn
 
Bi Star,mama Mwazani
Hana kazi mbovu yule mama,, halafu ni mkali sana hasa anapocheza na wasanii wachanga au wazembe wasio serious na kazi.
Yeye ukipangwa naye jiandae kumeza script na ujipange kweli maana anawapiga msasa wenzie kabla director hajaanza.
Hataki uzembe kabisa yule mama..
Ukiwa mzembe lazima Cha moto ukione kucheza naye [emoji1787]
 
Ile scene inayochekesha zaidi[emoji1787]
Yaani hii scene
Na ile ya J5 hii
Alikuwa amebeba fuko la nguo

Mgonjwa anamwambia shkamoo
Anajibu shkamoo mwenyewe[emoji1787]
Umebeba Nini
Eti nywele zakoo[emoji23]

Yaani yule mama ni boonge la comedian
Bahati mbaya waandaaji wengi wameacha watu wenye vipaji kama Hawa
Ila wanatujazia watu ambao hata kuigiza hawawezi, kisa tu jitu Lina mwenekano mzuri.
 
Hata kama sanaa 😂😂😂ndo bi ubwa akafue na kuoga choo cha wanaume😂😂😂yan wale wanafurahisha sn
That’s the whole point!😂

Sasa namna walivyokuwa wanajibizana asee ni kaka kweli hawaigizi, Bi. Ubwa na wenzao wako very natural wallah siwezi ikosa kutazama 😂😂😂

Unazizungumziaje zile love story za
Mbiki na Msichoke
Tausi na Masalu
Ombeni na yule bi mzee (hii naipenda sana)😂😂
 
Mie napenda ya Tausi na Masalu[emoji91]
 
Couple ya ombeni ni 🔥 napenda anavyompenda yule mzee yan utadhn kweli😂😂😂 ila ndo wapo kuharibiwa😂😂..
 
Kabisaa mkuuu
 
Hizi nyingine nyingi watu mda woote wapo na makeup.. Hadi muda wa kulala😂😂 adi unashangaa ni kwelii jamanii?

Ndo maana kuna mdau alisema kuwa japokuwa ni sanaa lakn wanaigiza kuigiza maisha😂😂
 
Yani wanaoandaa ile tamthilia wako fire kuanzia quality mpaka story na muonekano wa wachezaji hakuna tamthilia inayozidi quality pale
Ila kosa moja inastory nzuriii ila inasubiri kwa zahanati ya kijiji
Fundi vp?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…