GoLC
JF-Expert Member
- Jul 10, 2025
- 268
- 466
Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza dada Lamata kwa ubunifu na uchapakazi katika tasnia ya filamu (tamthiliya)
Nikiri huwa naifuatilia tamthiliya ya Juakali. Ilianza vyema ila huku mbeleni imechangamka kwa namna ambayo inaleta sintofahamu nyingi. Kwa akii ya kizazi cha leo bila shaka watachota kile waonacho bila kuchimba ndani kuelewa dhima nzima ya mwandishi (kama ipo).
Nitake kuamini tu kuwa mwandishi ana nia njema HUKO MBELENI mambako sijui tutafika lini. Ni wakati sasa ihitimishwe maana kila siku ni mauzauza.
Mamlaka husika naamini wanafuatilia kwa ukaribu. Hakika Lamata asipoitendea kazi yake haki kwa kuhitimisha kwa funzo KUU, basi atakuwa amefeli sana na kuwafelisha weng kwa kuwaingiza katika dhana ya kuchukulia ndoa kama mchezo rahisi tu na unaweza kufanya utakalo ukiwa ndani ya ndoa na hasa USALITI. Yaani UZINZI.
Asipohitimisha kwa funzo kuu atakuwa kawakosesha heshima kina Profesa Bill ( Mzee Masako), Mrs Bill (Sauda Simba), Zembwela (Patrick) na wengine.
Tunajua ni michezo ya kuigiza ndio, ila lazima pawepo na tahadhari kwenye kila hatua. Hata zile Disclaimer huwekwa zikakaa kwa sekunde 2 tu, nani ataweza kusoma maelezo yote yale kwa muda huo?