Tamthiliya ya Juakali isipoisha kwa funzo kuu, basi mwandaaji asipewe tena jukwaa kama lile kueneza upotovu

Tamthiliya ya Juakali isipoisha kwa funzo kuu, basi mwandaaji asipewe tena jukwaa kama lile kueneza upotovu

Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza dada Lamata kwa ubunifu na uchapakazi katika tasnia ya filamu (tamthiliya)

Nikiri huwa naifuatilia tamthiliya ya Juakali. Ilianza vyema ila huku mbeleni imechangamka kwa namna ambayo inaleta sintofahamu nyingi. Kwa akii ya kizazi cha leo bila shaka watachota kile waonacho bila kuchimba ndani kuelewa dhima nzima ya mwandishi (kama ipo).

Nitake kuamini tu kuwa mwandishi ana nia njema HUKO MBELENI mambako sijui tutafika lini. Ni wakati sasa ihitimishwe maana kila siku ni mauzauza.

Mamlaka husika naamini wanafuatilia kwa ukaribu. Hakika Lamata asipoitendea kazi yake haki kwa kuhitimisha kwa funzo KUU, basi atakuwa amefeli sana na kuwafelisha weng kwa kuwaingiza katika dhana ya kuchukulia ndoa kama mchezo rahisi tu na unaweza kufanya utakalo ukiwa ndani ya ndoa na hasa USALITI. Yaani UZINZI.

Asipohitimisha kwa funzo kuu atakuwa kawakosesha heshima kina Profesa Bill ( Mzee Masako), Mrs Bill (Sauda Simba), Zembwela (Patrick) na wengine.

Tunajua ni michezo ya kuigiza ndio, ila lazima pawepo na tahadhari kwenye kila hatua. Hata zile Disclaimer huwekwa zikakaa kwa sekunde 2 tu, nani ataweza kusoma maelezo yote yale kwa muda huo?
Tathmilia inafundisha ufuska na umalaya tu.
Hakuna scene isiyo na umalaya ndani yake.
Kwangu nilipiga marufuku
 
Hongera sana kama ulifanikiwa, maana kina mama huwaambii kitu.
Nilipiga marufuku tena kwa biti kali haijawahi kuonekana tena,ikifika muda wa Juakali naona wanahamisha chanell wenyewe tu.

Ni upumbavu Television kutengeneza tamthilia za maudhui ya ufuska na ngono.

Na Vyombo vyetu vya habari huwa hawachuji maudhui wala kutoa onyo kwa contents wanazoonyesha.

Usenge mtupu
 
Yaani hii tamthilia hata usipoiangalia kwa miesi kadhaa, ukija kuangalia hakuna jipya utakutana nalo zaidi ya wake za watu kuliwa
Duh!Mkuu Wanaonyesha live kabisa kama ile tamthilia ya Kisauzi Fatal Seduction, niaanze kuifatilia na mimi.
 
Nilipiga marufuku tena kwa biti kali haijawahi kuonekana tena,ikifika muda wa Juakali naona wanahamisha chanell wenyewe tu.

Ni upumbavu Television kutengeneza tamthilia za maudhui ya ufuska na ngono.

Na Vyombo vyetu vya habari huwa hawachuji maudhui wala kutoa onyo kwa contents wanazoonyesha.

Usenge mtupu
Hili waliangalie kama kweli wanajali wananchi wao, hii tamthilia imekamata wengi, wanaanza kukopi na kuishi maisha yale yale wanayoyaona kwenye tamthilia... Wanajifunza kutulia na mke/mume mmoja sio sawa.
 
Iv bado kumbe watu wana muda na utapeli wa hapa bongo kwenye mambo ya saana, pale hakuna kitu ni vile basi
 
Hili waliangalie kama kweli wanajali wananchi wao, hii tamthilia imekamata wengi, wanaanza kukopi na kuishi maisha yale yale wanayoyaona kwenye tamthilia... Wanajifunza kutulia na mke/mume mmoja sio sawa.
Kwenye mabasi ndiyo hovyo zaidi
 
Huko nako ni changanyikeni na video za muziki zao hovyo
Kuna namna mamlaka zinafeli sana kwenye hili.
Ukisafiri na mzazi au binti zako inabidi ujifanye unasinzia mwanzo wa safari mpaka mwisho.
 
Hii series sikuimaliza. Itabidi niirudie tena. Ila yule mzee cleaner alikuwa hatari sana. Haachi ushahidi
Breaking bad ni aina fulani ya series inayohitaji uvumilivu kidogo, kuiangalia mpaka mwisho.

Mimi binafsi nilikuwa bored kuanzia season one hadi four, nilikuwa natamani kuiacha ila nakomaa tu. Hata season five nilivutiwa na episode tano za mwisho, episode tano za mwisho ndio breaking ilipo.

Kwangu ndio best series of all time!
 
Bila shaka sikuimalizia kwa kuwa season za mbele zilikuwa hazijatoka. Si unajua mambo ya pirate? 😀
 
Back
Top Bottom