Tamthiliya ya Juakali isipoisha kwa funzo kuu, basi mwandaaji asipewe tena jukwaa kama lile kueneza upotovu

GoLC

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
268
Reaction score
466
Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza dada Lamata kwa ubunifu na uchapakazi katika tasnia ya filamu (tamthiliya)

Nikiri huwa naifuatilia tamthiliya ya Juakali. Ilianza vyema ila huku mbeleni imechangamka kwa namna ambayo inaleta sintofahamu nyingi. Kwa akii ya kizazi cha leo bila shaka watachota kile waonacho bila kuchimba ndani kuelewa dhima nzima ya mwandishi (kama ipo).

Nitake kuamini tu kuwa mwandishi ana nia njema HUKO MBELENI mambako sijui tutafika lini. Ni wakati sasa ihitimishwe maana kila siku ni mauzauza.

Mamlaka husika naamini wanafuatilia kwa ukaribu. Hakika Lamata asipoitendea kazi yake haki kwa kuhitimisha kwa funzo KUU, basi atakuwa amefeli sana na kuwafelisha weng kwa kuwaingiza katika dhana ya kuchukulia ndoa kama mchezo rahisi tu na unaweza kufanya utakalo ukiwa ndani ya ndoa na hasa USALITI. Yaani UZINZI.

Asipohitimisha kwa funzo kuu atakuwa kawakosesha heshima kina Profesa Bill ( Mzee Masako), Mrs Bill (Sauda Simba), Zembwela (Patrick) na wengine.

Tunajua ni michezo ya kuigiza ndio, ila lazima pawepo na tahadhari kwenye kila hatua. Hata zile Disclaimer huwekwa zikakaa kwa sekunde 2 tu, nani ataweza kusoma maelezo yote yale kwa muda huo?
 
Umeona kitu cha muhimu sana, siku za nyuma nilifuatilia hasa yale mazingira ya kijijini yalikuwa na funzo jema, baadaye nikaona hekaheka za kubeba wake na waume za watu. Nikaacha kuifuatilia, nikawa naona vipande vifupifupi kwenye mtandao, ila ukweli isipohitimishwa vizuri inaacha funzo baya sana kwa jamii. Imekuwa na hekaheka za hovyo sana.
 
So far ujumbe atakuwa kaupata
 
Chai
 
Dah kiukweli umeona kitu cha msingi sana. Umenifanya nitafakari jinsi mtengenezaji wa series yangu pendwa ya breaking bad alivyo tengeneza kisa cha miss skyler white alipofumbia macho uhalifu wa mumewe na madhara makubwa aliyoyapata mwishoni.
 
Dah kiukweli umeona kitu cha msingi sana. Umenifanya nitafakari jinsi mtengenezaji wa series yangu pendwa ya breaking bad alivyo tengeneza kisa cha miss skyler white alipofumbia macho uhalifu wa mumewe na madhara makubwa aliyoyapata mwishoni.
Hii series sikuimaliza. Itabidi niirudie tena. Ila yule mzee cleaner alikuwa hatari sana. Haachi ushahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…