Tamthiliya ya Juakali isipoisha kwa funzo kuu, basi mwandaaji asipewe tena jukwaa kama lile kueneza upotovu

Mkuu, mbona kuna TV programmes nyingi tu mbali ya hiyo tamthiliya ya Juakali!? Nini kinachokufanya uvutiwe kuiamgalia zaidi na zaidi na hata kutaka kuwapangia wahusika nini cha kufanya!?

Lazima utambue ya kwamba tamthiliya ni aina ya sanaa ya maigizo ambapo hadithi inasimuliwa kupitia wachezaji wanaojifanya wahusika wa matukio yaliyopangwa vyema ili yaonekane mbele ya watazamaji kwa njia ya vipindi muendelezo wa filamu fupi zionekanazo katika luninga

Wahusika wake wanapewa majukumu tofauti ili kuweza kufikisha ujumbe fulani kwa wafuatiliaji wake. Tamthiliya inafundisha kwa kusikia na kuziona tabia mbaya na nzuri, na matokeo yake, kupitia maisha ya wahusika. Vipindi vya tamthilia vyenye ujumbe todauti vinawekwa katika channel tofauti ili watazamaji waweze kuziangalia kwa kadiri muda unavyowaruhusu.
Ujumbe wenye mapenzi, lugha za matusi, mauaji, ujambazi na mambo mazito kama hayo, tahadhari hutolewa mapema ili watazamaji waepuke kuwaonyesha watoto waliio na umri chini ya miaka 16 ama 13.

Aidha watazamaji wanashauriwa kuweka nywira katika baadhi ya TV programmes ili watoro wasiweze kuziona ana pasipo kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima na wenye kujiheshimu.

Ni jukumu lako binafsi la kuchagua nini cha kuona ama kusikia. It is simply, the garbage in,, the garbage out.
 
Ndugu Izato asante kwa mchango wako. Nitabakia na sentensi yako ya mwisho, kwamba ukipanda maharage utavuna maharage
 
Aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…