Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Nk kweli kabisa yani muda mwingine unatamani kungekua na copy and paste ya binadamu upate copy yako ataekua na nia kama uliyonayo wewe,ila nadhani ushakua milionea sindio
 
Hii inakuaga vizuri sana unatamani kila siku iwe faida kama uliyopata but ukweli ni kwamba bizness ni kushuka na kupanda
 
Hahaha mkuu hapa umenigusa mimi kabisa,yaani faida unakua nayo kabisa kichwani tayari,lakini ukishafika katika uwanja wa biashara unakuta mambo tofauti,hongera kwa kufungua biashara mkuu.
 
Safi mkuuu[emoji119][emoji119][emoji122][emoji122]
 
Aisee pole sana mkuu,kuku 700 mpaka 150 ni jambo linaloumiza na kuvunja moyo sana ila naimani hukukata tamaa na bado unapambana,research ni muhimu sana tofauti na tunavyoichukulia poa.
 
Umenikumbusha niliwahi lima mpunga alafu akawa anasimamia rafiki yangu aisee ile hasara sitakuja kusahau
 
Usimamizi wa biashara unaenda pamoja na utunzaji wa kumbukumbuku kwa njia ya maandishi..ata awe ndugu gani anatakiwa kuweka record ya kile kilochotoka na kuingia
Hapa umegusa penyewe wengi hatutunzi kumbukumbu,inafika hatua hela ya ofisi unaitumia kwenye mambo binafsi.
 
Siku zote mwanzo mgumu... And you can raise and fall several times...

Biashara ni imani...

Biashara mwanzoni inahitaji uvumilivu, ila ukishakua kwenye channel mambo mtelezo...

Cc: mahondaw
Hakika mwanzo ni mgumu boss,je wewe changamoto zako zilikua zipi
 
Kuna kaka yangu alikua anafanya hii biashara anatoa mkaa iringa anapeleka dar,yeye alikua anashiriki kila hatua kuanzia kutafuta mkaa,kupakia mpaka kuja nao dar,waliomuangusha ni madalali wa dar,aisee wale jamaa ni wajanja sana.
 
Walikuwa wanapiga pesaa za juu nini??
 
Hahaha wanawake bwana yani alafu anavyokuja kukupa mrejesho anakupa kirahisi tu kua zimebaki laki mbili [emoji3][emoji3][emoji3] hongera kwa ufugaji mkuu.
 
Hapa umegusa penyewe wengi hatutunzi kumbukumbu,inafika hatua hela ya ofisi unaitumia kwenye mambo binafsi.

Ata wahenga wanasema mali bila daftari itaisha bila kujua.. so record ni muhimu itakusaidia kujua bidhaa gani imekupa faida au ipi inauzika kwa haraka
 
Aisee pole sana mkuu,kuku 700 mpaka 150 ni jambo linaloumiza na kuvunja moyo sana ila naimani hukukata tamaa na bado unapambana,research ni muhimu sana tofauti na tunavyoichukulia poa.

Yes details ndogondogo mara nyingi tunazidharau lakini ndozenye maana kwenye biashara mkuu,haikuwa rahisi maana nilikata mpk mtaji wenyewe lakini nilisimama tena now namshukuru Mungu
 
Ata wahenga wanasema mali bila daftari itaisha bila kujua.. so record ni muhimu itakusaidia kujua bidhaa gani imekupa faida au ipi inauzika kwa haraka
Na wengi tusio andika haya mambo tunakosa kuyajua na biashara inakua haikui kwa kuto kujua bidhaa zipi nzuri na zinazotoka zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…