Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Nk kweli kabisa yani muda mwingine unatamani kungekua na copy and paste ya binadamu upate copy yako ataekua na nia kama uliyonayo wewe,ila nadhani ushakua milionea sindio
Changa'moto niliokutana nayo katika biashara zangu ni 'human resource' kupata mtu mwaminifu self driven and determined katika kazi zangu, limenichelewasha kua millionaire....watznia wengi wakiwemo na ndugu sio waminifu hawapendi kazi boss wao anachukuliwa kama adui wao
 
Nafanya/napenda kufanya biashara ya kununua na kuuza..chungu ni pale unaponunua mzigo mwingi then inatokea kwenye market bidhaa zimeshuka so wapinzani wako wanapata kwa bei chee , hakika utaiona chungu ya biashara

Tamu ni pale unakuwa na stock nyingi then product inakuwa in demand kwenye soko, ahha utaona tamu ya biashara au competitors wako wapate the same product kwa bei ya juu
Hii inakuaga vizuri sana unatamani kila siku iwe faida kama uliyopata but ukweli ni kwamba bizness ni kushuka na kupanda
 
Ambao hawajaanza hawawezi elewa kitu hapa.... Anyway, mimi ndo kwanza nina siku ya tatu toka nianze biashara. Mambo si rahisi kama nilivyokua nafikiri.

Sikati tamaa, nakua mvumilivu maana naamini mafanikio yangekua rahisi kila mtu angekua amefanikiwa. Kila jambo linahitaji muda.

Wakati una wazo zuri la biashara, unaanza hadi ku-calculate faida ilhali hujaanza hata [emoji23][emoji23]
Hahaha mkuu hapa umenigusa mimi kabisa,yaani faida unakua nayo kabisa kichwani tayari,lakini ukishafika katika uwanja wa biashara unakuta mambo tofauti,hongera kwa kufungua biashara mkuu.
 
Nilifungua duka la reja reja kwa mtaji wa million moja na nusu, nikwamweka wife anisaidie kuuza sababu yuko home free, kumbe mwenzangu hapendi biashara, baada ya miezi mitatu vitu vimeisha dukani nimemkuta na balance ya laki mbili tu, namshukuru mungu nilifunga duka nikawekeza kwenye kufuga mbuzi naishi mjini mbuzi nafungia kijijini msimamizi ni mama yangu,namshukuru mungu nilianza na mbuzi wa nane saivi mimefikisha mbuzi arobaini na tatu. daima nitaendelea kumwamini mzazi kuliko Mke.
Safi mkuuu[emoji119][emoji119][emoji122][emoji122]
 
Changamoto ni nyingi hata sijui nianzie ipi ila kubwa kuliko zote nilipoingia kwenye ufugaji ugonjwa ukaingia bandani kila siku naokota kuku 15-30 wamekufa na kati ya kuku 700 niliuza 150 sitasahau

Kutofanya research ya biashara kabla ya kuanzisha kulinicost sana kwenye biashara ya mgahawa unapika chakula hakuna wateja kila siku unalaza aisee
Aisee pole sana mkuu,kuku 700 mpaka 150 ni jambo linaloumiza na kuvunja moyo sana ila naimani hukukata tamaa na bado unapambana,research ni muhimu sana tofauti na tunavyoichukulia poa.
 
Wakati niko chuo nilipata boom kiasi cha lakhi 4. Nikaamua nikizalishe. Nikaanza biashara ya mbao. Kwa vile sikuwa na muda wa kusimamia, ilibidi tu niwaamini marafiki. Weee... kosa kubwa. Biashara ilifirisika. Nikajifunza kuwa usimamizi wa biashara ni muhimu tu kama ilivyo mtaji. Kuanzia hapo kama sina muda wa kusimamia, sifanyi biashara.
Umenikumbusha niliwahi lima mpunga alafu akawa anasimamia rafiki yangu aisee ile hasara sitakuja kusahau
 
Usimamizi wa biashara unaenda pamoja na utunzaji wa kumbukumbuku kwa njia ya maandishi..ata awe ndugu gani anatakiwa kuweka record ya kile kilochotoka na kuingia
Hapa umegusa penyewe wengi hatutunzi kumbukumbu,inafika hatua hela ya ofisi unaitumia kwenye mambo binafsi.
 
Siku zote mwanzo mgumu... And you can raise and fall several times...

Biashara ni imani...

Biashara mwanzoni inahitaji uvumilivu, ila ukishakua kwenye channel mambo mtelezo...

Cc: mahondaw
Hakika mwanzo ni mgumu boss,je wewe changamoto zako zilikua zipi
 
Biashara ya mkaa kutoa pori kupeleka mwanza,changamoto niliyokutana nayo ni jamaa tunayeshirikiana nae kupeleka mzigo yaani anaweza kupeleka mzigo hata mara tatu kwa mwezi ila mimi ananificha kwa kuwa niko bize na kazi nyingine.ila sasa hivi nasubiri akinimalizia mzigo wangu namtema naanza ku fight kivyangu.
Kuna kaka yangu alikua anafanya hii biashara anatoa mkaa iringa anapeleka dar,yeye alikua anashiriki kila hatua kuanzia kutafuta mkaa,kupakia mpaka kuja nao dar,waliomuangusha ni madalali wa dar,aisee wale jamaa ni wajanja sana.
 
Walikuwa wanapiga pesaa za juu nini??
 
Hahaha wanawake bwana yani alafu anavyokuja kukupa mrejesho anakupa kirahisi tu kua zimebaki laki mbili [emoji3][emoji3][emoji3] hongera kwa ufugaji mkuu.
Nilifungua duka la reja reja kwa mtaji wa million moja na nusu, nikwamweka wife anisaidie kuuza sababu yuko home free, kumbe mwenzangu hapendi biashara, baada ya miezi mitatu vitu vimeisha dukani nimemkuta na balance ya laki mbili tu, namshukuru mungu nilifunga duka nikawekeza kwenye kufuga mbuzi naishi mjini mbuzi nafungia kijijini msimamizi ni mama yangu,namshukuru mungu nilianza na mbuzi wa nane saivi mimefikisha mbuzi arobaini na tatu. daima nitaendelea kumwamini mzazi kuliko Mke.
 
Hapa umegusa penyewe wengi hatutunzi kumbukumbu,inafika hatua hela ya ofisi unaitumia kwenye mambo binafsi.

Ata wahenga wanasema mali bila daftari itaisha bila kujua.. so record ni muhimu itakusaidia kujua bidhaa gani imekupa faida au ipi inauzika kwa haraka
 
Aisee pole sana mkuu,kuku 700 mpaka 150 ni jambo linaloumiza na kuvunja moyo sana ila naimani hukukata tamaa na bado unapambana,research ni muhimu sana tofauti na tunavyoichukulia poa.

Yes details ndogondogo mara nyingi tunazidharau lakini ndozenye maana kwenye biashara mkuu,haikuwa rahisi maana nilikata mpk mtaji wenyewe lakini nilisimama tena now namshukuru Mungu
 
Ata wahenga wanasema mali bila daftari itaisha bila kujua.. so record ni muhimu itakusaidia kujua bidhaa gani imekupa faida au ipi inauzika kwa haraka
Na wengi tusio andika haya mambo tunakosa kuyajua na biashara inakua haikui kwa kuto kujua bidhaa zipi nzuri na zinazotoka zaidi
 
Back
Top Bottom