PreGE2025 TAMWA yataka wanawake watakaojitokeza kutia nia kwenye Uchaguzi waungwe mkono

PreGE2025 TAMWA yataka wanawake watakaojitokeza kutia nia kwenye Uchaguzi waungwe mkono

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Joyce Shebe amesema wanawake watakaoonesha nia ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 wanapaswa kuungwa mkono na jamii ili waweze kutimiza ndoto zao za kuwa viongozi.

Ushauri huo ameutoa Jijini Dodoma katika Mkutano wa wanachama waTaasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA - TAN) na wadau wa habari,ambapo amesema Mwanamke hapaswi kukatishwa tamaa pindi anapotaka kuomba nafasi mbalimbali katika uchanguzi mkuu.



Mwanamke asihukumiwe kwa jinsia yake na badala yake ahukumiwe kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake katika nafasi aliyonayo na uchaguzi usitumike kama kigezo cha kumkandamiza ili asipate haki ya kikatiba ya kuchaguliwa.

"Wanawake wamekuwa waoga kujitokeza kugombea katika chaguzi mbalimbali kwa hofu ya kudhalilishwa,wakiwa majukwaani hivyo ni budi jamii iondokane na dhana hizi kandamizi ambazo sisi TAMWA tumekuwa tukizipinga,"amesema Shebe.


IMG_0671.jpeg


Source: Nipashe
 
Back
Top Bottom