Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,488
- 20,051
Salamu wana JF
Sitapoteza muda wenu bali nitafanya rejea fupi kwa yale yaliyotokea miezi michache iliyopota kule Ngorongoro tulishuhudia baadhi ya vijiji vikifutwa na watu kuhamishwa.
Lile lilikuwa ni kwa maslahi mapana ya ikolojia na uhifadhi wa mbuga zetu .
Sasa kuna hii mbuga ya taifa Arusha, inaweza ikawa sio maarufu sana kwa watu wengi lakini hii ni mbuga ya taifa iliyopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Hii mbuga ni kama inaenda kuwa kisiwa kiikolojia sababu ya miingiliano kati ya watu na wanyama hasa kwenye mapitio ya wanyama pori.
Kwa ushauri wangu, kwa sasa serikali na wataalamu wa masuala ya wanyamapori, ardhi na makazi kuanza upya mchakato wa kuondoa watu na kufuta baadhi ya vijiji vinavyozunguka mbuga hii ili kufungua upya mapitio ya wanyama pori sababu kwa sasa wanyama ni kama wanapungua na kupotea sababu ya kuzuiwa kwa uzalianaji wao.
Tusipokuwa makini ile mbuga itageuka mbuga ya vipepeo na ndege sababu wanyama hawana pakupita kwenda kuzaliana na wanyama wa mbuga na pori zinazopakana na mbuga ile.
Nina amini wapo wataalamu na washauri wataweza kuliamsha hili na kuepudha migogoro hapo baadae ikitokea ikahitajika ulazima wa kuwaondoa watu na kufuta vijiji.
Sina mengi wana JF.
Wasalimu.