KERO TANAPA mna shida gani? Wageni kukaa siku nzima getini kisa mfumo wa malipo haufanyi kazi si sawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wafanye pia kaguzi za permit tunapotoka magetini, kuna wafanyakazi wao washaanza kutengeneza mfereji wao wa kula hela za Extra day
Cha ajabu sasa ambacho mimi binafsi nimewahi kukishuhudia ni kuwa,wakati tunaambiwa kuwa mfumo wa malipo uko chini hivyo tusubiri urekebishwe kuna madalali wapo pale ambao unaweza kuunganishwa nao na wao wakakulipia kwa kadi zao kwa namna wanayojua wao, mimi waliniambia niwape 260,000 cash ili wanilipie 210,000,sasa nikajiuliza huo mfumo unagoma kwetu tu? Kutokana na haraka niliyokuwa nayo ilinibidi nimpe,kuna shida mahali.
 
Kula kwa urefu wa kamba...
 
Hii sio sawa. Hii ilikua geti lipi, na mwaka gani mkuu
 
Kipenzi na mtukufu wa daraja kwenye uislamu ni mtume Muhammad s.a.w pekee..
 
Nilikuona mda mrefu umeinamia simu pale nikajui lazima tuisome pahala
 
Nani anap
Mbinu chafu za ushindani wa kibiashara. Kwamba, watalii wazichukie hifadhi za Tanzania kutokana na kukosekana kwa customer care ya kuridhisha.
ata
hao wanafanya hivyo ni wahuni, mfumo ukienda sown hakuna namna nyingine. uli report kokote?
 
Changamoto za internet zinaeleweka Dunia nzima.
Swali linakuja ni kwanini wasiwe na plan B?
Binafsi lishanitokea... Nilipoteza muda mwingi na kushindwa kuwahi flight!
yes plan b lazima iwe standby kama standby generator kwa katiko la umeme
 
Aise hii aibu ya mwaka hawa jamaa washughulikiwe haraka sana
 
Lakini maafande wale hawanaga plan B... Wao ni amri amri tu!
In short wageni wengi wakija hawarudi!!

Inaelekea hakuna SOP kwa kazi yao wala hawajishughulishi kutengeneza
"Instant remedial action"
 
nchi yenyewe inapokea watalii wachache kwa sababu ya usenge bado tena hao wachache muwakose kabisa
kweli muafrika yake jembe kushinda shamba
 
Isije ikawa ni mbinu ya kuwapunguza watalii wanaoingia Tanzania.

Kama tetesi kuwa kipindi fulani bwawa la Mtera lilikuwa likihujumiwa ili kusababisha mgao wa umeme, hilo nalo halishindikani kufanyika.
Au kuwapa upenyo wavuna ndovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…