TANAPA na POLISI wasema wanashirikiana na Wananchi wa Kisaki Morogoro kufuatilia madai ya watu kupotea hifadhini

TANAPA na POLISI wasema wanashirikiana na Wananchi wa Kisaki Morogoro kufuatilia madai ya watu kupotea hifadhini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya kusambaa kwa video ikionesha Wananchi wa Kijiji cha Kisaki Mkoani Morogoro wakidai kuna ndugu zao wamepotea katika mazingira tata kwenye Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, mamlaka husika imetoa ufafanuzi.

Kuangalia Hoja ya Wananchi hao bofya hapa ~ Clip ya Wananchi wa Kisaki kupinga mauaji yanayofanywa na Askari wa Hifadhi Morogoro, inatuma ujumbe gani kwa Mamlaka?

MAELEZO YA TANAPA
Kuhusu madai hayo ya Wananchi, upande wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema “TANAPA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tumewapa ushirikiano Wananchi hao kwenda kutafuta Watu wanaodaiwa kupotea lakini hatujafanikiwa kuwapata, hivyo tunaendelea kushirikiana nao katika suala hilo.

“Pia, tunatoa wito kwa Mwananchi yeyote mwenye taarifa za uhakika, awasiliane nasi katika kushirikiana nasi kupata ukweli wa malalamiko yao.”

JESHI LA POLISI MKOA WA MOROGORO LATOA TAMKO
Upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limetoa ufafanuzi kufuatia malalamiko na video hiyo ikiwahusisha Askari wa Wanyamapori wa waliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na vitendo vya ukatili dhidi ya wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Kantimbo amesema jeshi hilo limefanya uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na wananchi ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

ACP Kantimbo ameeleza kuwa hadi sasa, uchunguzi uliofanywa hauoneshi kuwepo kwa mauaji, miili iliyojeruhiwa, au uthibitisho wa kifo cha mtu yeyote kama ilivyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, jeshi hilo limethibitisha kuwepo kwa watu wawili ambao wanadaiwa waliingia ndani ya eneo la hifadhi, lakini mpaka sasa hawajaonekana wala kurudi kwenye maeneo yao ya vijijini. Kutokana na hali hiyo, uchunguzi unaendelea ili kuwatafuta watu hao.

Wito kwa Wananchi na Kuzingatia Sheria za Uhifadhi
Kamanda Kantimbo ametoa wito kwa wananchi wote wenye taarifa za ziada au ushahidi kamili kujitokeza ili kuisaidia polisi kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha, amewakumbusha wananchi kuwa maeneo ya hifadhi yana wanyama wakali, na amewasihi kuheshimu sheria kwa kutooingia ndani ya hifadhi hizo bila vibali au bila kufuata taratibu maalumu za kisheria. Polisi imeahidi kuendelea na uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wote na kuchukua hatua stahiki.
 
Back
Top Bottom