KERO TANAPA wananizungusha na malipo yangu kwa miaka miwili sasa

KERO TANAPA wananizungusha na malipo yangu kwa miaka miwili sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni muathirika wa hali ya sasa katika taasisi ya TANAPA.

Nilifanya kazi moja, na ni miaka miwili sasa imepita bila kulipwa. Mbali na mimi, kuna mwenzangu analalamika kuwa mama yake alifanya kazi tangu mwaka jana akiwa bado hajastaafu, lakini mpaka sasa ni mwaka umepita tangu astaafu na bado deni halijalipwa.

Ikumbukwe kuwa kazi hizi zilifanyika nje ya vituo vya kazi, na watu walikopa ili waweze kujikimu.

Tunapofuatilia malipo yetu tunaambiwa, “mtalipwa,” lakini tunaendelea kuzungushwa huku madeni yakizidi kuongezeka.

Jambo jingine linaloumiza ni kuona taasisi hiyo hiyo ikifanya kazi na wasanii, hasa wachekeshaji na matiktoker, ambao wanalipwa kwa wakati na vizuri, huku sisi raia wa kawaida tunaofanya kazi halisi tukizungushwa tu.

Mungu atuone kama Taifa na wananchi wake jamani
 
Back
Top Bottom