Ikitotanzila
JF-Expert Member
- Sep 22, 2020
- 1,409
- 2,263
MZAZI mwenza wa supastaa wa Bongo Fleva barani Afrika, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch, usiku wa jana Januari 22, 2020 ametua nchini akiwa na mtoto wake Naseeb Junior wakitokea kwao nchini Kenya.
Tanasha amepokelewa na gari ya Diamond katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Tanasha amesema amekuja kwa ajili ya shughuli za kimuziki ikiwemo ku-shoot video na Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania Faustina Charles maarufu kwa jina la Nandy.