Mara nyingi watu wanaokuwa bored kirahisi ni watu ambao hawana uwezo mkubwa wa kufikiri. Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri wanaweza kuona vitu interesting in the most uninteresting things.
Umeni engage mchongaji, lazima upate anecdotal stories
Genius wa hesabu wa kihindi aliyeitwa Ramanujan, alitembelewa na rafiki yake Muingereza Harding. Hawa miamba wawili akili zao hazikuwa nzuri kwenye hesabu. Harding aliyekuwa kaletwa kwa Ramanujan na taxi , akamwambia Ramanujan, ile taxi iliyonileta ina nambq moja very boring, the number is not interesting at all. Hiyo taxi ilikuwa namba 1729.
Ramanujan na u genius wake akaona kitu tofauti kabisa.
Akamwambia Harding.Hiyo namba iko very interesting.
Akasema ""it is a very interesting number; it is the smallest number expressible as the sum of two [positive] cubes in two different ways."
en.m.wikipedia.org
Sasa pengine unaona watu wachongaji wako boring - especially wanaojua wanaongea nini, kuna wengine wako boring kwa sababu hawana point, I will give you that- kwa sababu wewe una uwezo mdogo tu wa kuelewa mambo.
Kuna sababu kadhaa za wewe kuwa bored na mtu anayechonga.
Na sababu hizi zinaweza kuwa valid au invalid kuhusiana na mazingira.
1. Wewe unamuonea gele huna uwezo wa kuchonga.
2. Anaongea vitu off point kwako
3. Anaongea vitu vyenye point ila wewe uwezo wako wa kumuelewa mdogo.
4. Wewe ni anti-social una tabia ya kuogopa watu tu.
5. Kakuingilia sehemu yako ya mapumziko.
6. Wewe ni msiri una mengi ya kuficha na unaogopa mtu akikuzungumzisha sana atafunua unayotaka kuficha. Winston Churchill alisema modest people have much to be modest about"
7. You are not curious or inquisitive.
8.Umekwenda sehemu isiyokuhusu. Yani kama wewe mtu hupendi maongezi halafu umekwenda kijiwe cha muuza kahawa. Hapo lazima uudhike watu wanaongea sana lakini tatizo ni wewe mwenyewe ulitakiwa kwenda kwa maburuda watawa walioapa kiapo cha ukimya.
JF ni kijiwe cha maongezi. Kama hupendi wachongaji na umekuja JF umepotea njia.
9. Hujui kujitetea kimaongezi na watu wanaochonga wanakushinda kwa hoja kila mara.
10. Umelianzisha na mtu anayechonga halafu hujui kulimaliza.
Wewe mtu hutaki watu wanaochonga halafu unalianzisha na Kiranga lazima nikuone hujui unachotaka ni nini katika maisha haya.
Maana atachonga alphabet nzima kuanzia Alpha particles mpaka Zeta functions, na zote zitakaa sawa na kuwa relevant kwenye maongezi.
Kuanzia mashairi ya Hip Hop ya Rakim The God MC mpaka milinganyo ya hesabu ya Ramanujan-Harding
Wakati huo wewe unajisemea "Why did I start it with this guy?"
Kama hupendi watu wanaochonga, hususan wanaojua wanachonga nini, kaa mbali na mimi.
Kuna siku nilimuuliza jamaa mmoja mzungu, kwa nini wazungu wanapenda sana vita?
Akanijibu, kwa sababu wanaiweza vizuri sana.
They are just good at it.
Labda sababu hupendi watu wanaochonga ni kwamba wewe huwezi kuchonga.
Na kuchonga kwa mpangilio kunataka akili, ujuzi wa lugha, kuwa na data, kumbukumbu, uwezo wa kuunganisha mambo kimantiki, kujiamini etc.
Vitu ambavyo kama huna, siwezi kushangaa ukiwa hupendi watu wanaochonga.
Unakuwa naturally hupendi watu waliokuzidi vitu fulani muhimu.