Wakati mwingine ni uungwana kukubali kuwa wewe ni mjinga na pengine mpumbavu inapotokea kitu unachofahamu kuhusu jambo fulani ni matokeo ya ujinga ulio nao..suala la nishati kwa maisha ya binadamu wa leo ni nyeti sana, hasa kwa vile aina nyingi za nishati zina madhara ya kimazingira kupelekea kuathiri uhai wa viumbe hai akiwemo binadamu na hivyo nishati yoyote ambayo inaleta madhara iwe ni ya muda mfupi au mrefu ni vyema kutathimini vizuri namna ya kuitumia, mengine yanayohusiana na vyanzo vya nishati ni pamoja na kujua kama nishati hiyo ni endelevu, gharama zake nk. Ukiorodhesha aina zote za vyanzovya nishati vilivyopo..jua, upepo, maji, mafuta, madini (gesi , uranium,coal nk), joto ardhi na vingine jibu unalopata kuhusu nishati gani inakidhi changamoto za kimazingira na uendelevu jibu ni jua, upepo pengine na joto ardhi..gharama haiwezi kuwa kigezo cha kudrive maamuzi unapochagua aina ya nishati.
Baada ya kufahamu hayo kinachotokea kwenye maisha yetu tunapochagua aina ya nishati tulizo nazo ni kuwa na mchanganyiko wa kutumia nishati zote...ili hata kama nchi yetu inayo nishati fulani kwa wingi, let say maji..ni muhimu pia kutumia nishati ya jua na upepo japo kwa asilimia kidogo ili kuwa na mbadala wa nishati inayotokana na maji ili kuchangia kupunguza athari za kimazingira na kuwa na uendelevu, kama nishati moja ikipata changamoto, maji yana matumizi mengi, lakinimaji yanategemea mvua, mvua zinaweza kupungua na hivyo maji kupungua pia, kama huna chanzo kingine utaathirika sana...ni muhimu na lazima kuwa na MIX ya vyanzo vyote...na hicho ndicho wanafanya TANESCO!!
Kwanza wamechelewa sana, ilitakiwa tuwe na megawat zaidi ya 300 zinazotokana na jua na upepo kwenye gridi yetu, hizi sio luxurious energy..ni reliable energy!