TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Bado narudi pale pale.
Mtoa mada kasoma juu juu kakimbilia ku-post jambo asiloelewa.
Angalia content ya hiyo tender, kampuni husika itafanya feasibility study, ita build solar farm, ita operate yenyewe, then baada ya miaka kadhaa, kama 20 hadi 25 Solar Farm itakabidhiwa kwa Tanesco kama mali halali ya Tanesco.

All that long, Tanesco itakuwa inauziwa umeme hadi muda wataokubaliana ufike. Hapo wewe unataka nini tena?
Kiwanja hujatoa, initial investmest hujachangia, umeme unauziwa kwa bei ndogo.
Baada ya miaka 20 hadi 25 plant inakuwa yako 100%.

Ikumbukwe kuwa Return On Investment ya Solar Farms ni miaka 10 hadi 15.
So hapo bado Tanesco are to benefit.

20200306_125516.jpg

Binafsi pia huwa niko kinyume sana na energy hii ya solar. Huyu munayemuuliza atakuja na jibu lake lakini kinachoonekana ktk taarifa ni hiki, bonyeza hapo chini. Vyovyote ilivyo, Tanesco imejiingiza kwenye zoezi baya lisiloisaidia kutatua matatizo ya power ya nchi. Rais aliwaonesha wazi kwamba kuna mini-hydro nyingi ambazo hawazipi support, ndo wakastuka. Sasa tena wanakuja na support ya watu wa solar. Sijui wazo kama hilo wamelitoa wapi? Au ni nguvu ya watu fulani wanaotafuta biashara na Tanesco., ipigwe tena!
TANESCO LAUNCHES 150 MW SOLAR TENDER IN TANZANIA
 
Siyo kwamba hutozwi chochote bali umelipa zaidi ya yule wa grid ya taifa.
Tanesco ina jukumu la kitaifa siyo la familia yako unayewasha taa na kunyoa ndevu na ... Unapotoa umeme wa kitaifa, ukumbuke kuna wanaoyeyusha vyuma chakavu, kuna wanaohitaji kuendesha mitambo ya madini, kuna wanaotaka kuwa na textile industries. Hapo kuna solar gani ya kutumia ili ufanye kazi usiku na mchana?

Tanesco wanafanya majaribio kwa faida yao badala ya kutafuta umeme unaoeleweka.
As personal natumia solar na sijawahi kulipia chochote!!!...Nina washa na kutumia kila kitu Cha Umeme
 
We mtu unamtukana mwenzako lakini nikisoma ulichoandika, it's another piece of rubbish! Zygot anaonesha anayafahamu yote hayo, wewe unajificha kwenye kichaka cha mazingira na hapo ndo mimi nakuja na uelewa wangu. Wewe ni mzembe. Tanesco kwa ujumla hawajaweza hata kuzalisha umeme wa kujivunia. Angalia energy partitioning ya China nchi ambayo imeendelea hivi karibuni kabisa kwa kutumia nishati ya coal. China ndo nchi yenye bwawa kubwa la umeme duniani.

Kimazingira, Third world bado tunaruhusiwa kutumia mkaa tulionao kwa makusudi na jumuiya ya kimataifa, wanfahamu njia hizo zingine kweli ni luxurious! Wenyewe tumefanya commitment ya kutimiza matakwa ya kimazingira kwa kadri tunavyoweza, siyo tunavyolazimishwa (Paris Agreement). Sasa wewe unakuja kwa mkwara na matusi utadhani hata mazingira unayafahamu.

Kwa upande wa energy, niambie third world gani iliyojiingiza na kufanikiwa kwenye upuuzi huo unaokutia kiwewe hata umtukane mwenzako? Dar imejaa wapuuzi wadanganyifu wanawapiga watu pesa kwa solar kwa sababu ya uzembe wa Tanesco kuwapa umeme wa uhakika. Mbaya zaidi kwa tamaa ya upigaji, wizara nayo inatoa support ya kusambaza solar badala ya umeme wa grid. Nani anaweza kusaga mahindi kwa solar? Nani anaweza kuranda mbao kwa solar? Gharama gani ataitumia kuweka miundo mbinu kama hiyo ukilinganisha na umeme wa grid kuu? Ukimuona mwenzako mpuuzi, nawe usiweke upuuzi.

Kama nawe uko Tanesco kwa hilo ni upuuzi. Wekezeni kwenye mkaa, wekezeni kwenye mini-grids, wekezeni kwenye thermal ambako Kenya walishafanya, ninyi tunawasikia miaka miingi bila kufika kokote na ghafla tunawaona kwenye solar. Hizo ni dili na makampuni ya nje tu!
Maneno ya mtu mgonjwa wa akili haya, hivi athari za mazingira zinazotokea nchini kwetu hazijulikani?? hali ya jangwa shinyanga na simiyu kwa kukata miti kufanya mkaa haijulikani?? Dodoma, singida nk..hali hii ikiendelea miaka 10 ijayo nini kitatokea ?? halafu unaleta habari sijui china, waliofika china, india wanafahamu anga la nchi hizo lilivyo kutokana na CO2 emmissions, hewa ni nzito hata shida kupumua...hivi kufanya kitu cha faida kwako ni lazima third world wengine wawe wamefanya?? upuuzi mtupu! nenda katibiwe kwanza, ndio uje kuchangia mada hapa.
 
Solar ni umeme Bora na rahisi sana kuliko unavyopotosha!!!...nimetumia solar hapa Geza ulole kigamboni Dar es salaam miaka 6 sikuona Wala kupata shida ya aina yeyote!!!... tofauti yake uwekezaji wake unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika
Mkuu solar ndio solution kwa umeme wa majumbani.
Shida serikali haipo serious na solar wapo kitheory zaidi.
Wewe jiulize hata mji mdogo wa mfano/majaribio unaotumia solar hakuna.
Uzuri wa solar utaupenda hakuna kukatika umeme.
 
tanesco mjitahidi sana kuja na suluhisho mobisol wanatupiga sana nchini!kwamfano mi nalipa 50000/= kila mwezi mtambo wa mobisol wat 120!kisa uzembe wa tanesco nchini!!!
Hao Mobisol wamewapiga sana wanakijiji huku Meru kabla ya kuja kwa umeme wa Rea
 
Maneno ya mtu mgonjwa wa akili haya, hivi athari za mazingira zinazotokea nchini kwetu hazijulikani?? hali ya jangwa shinyanga na simiyu kwa kukata miti kufanya mkaa haijulikani?? Dodoma, singida nk..hali hii ikiendelea miaka 10 ijayo nini kitatokea ?? halafu unaleta habari sijui china, waliofika china, india wanafahamu anga la nchi hizo lilivyo kutokana na CO2 emmissions, hewa ni nzito hata shida kupumua...hivi kufanya kitu cha faida kwako ni lazima third world wengine wawe wamefanya?? upuuzi mtupu! nenda katibiwe kwanza, ndio uje kuchangia mada hapa.
Failure! Unajitutumua na elimu haba. Nini maana ya athari za mazingira? Au una maana athari za uchafuzi wa mazingira? Huijui hata elimu ya mazingira inavyotakiwa. Dodoma, Singida, shinyanga na Simiyu ni tatizo la athari ya mazingira kwa maoni yako? Hukusoma geography ya nchi yetu?

Nakupa shule ili kama unaweza upanuke kimawazo. Uchafuzi wa India na China, specifically Beijing unawafanya wavae mask barabarani. Je hiyo ni CO2? Unafahamu kwamba CO2 haionekani? Kweli unaweza kuvaa mask kuzuia CO2 eti hewa ni nzito! What is Nzito? Unachoandika ni yale unayasikia. Hakuna utaalamu hapo!

Unaleta tena mambo ya kukata miti. Umeme unazuia kukata miti? Dar tuna umeme, tumeacha kutumia mkaa? Umeme unazuia matumizi ya mkaa? Nigeria inaongoza kwa kuuza mkaa nje, hiyo ni ukosefu wa umeme? Hakuna uhusiano kati ya kukata miti na kuwepo kwa solar. Ukitaka kufundisha mazingira kwa usiowafahamu utaumbuka.
 
As personal natumia solar na sijawahi kulipia chochote!!!...Nina washa na kutumia kila kitu Cha Umeme
Kuna kitu hakiingii akili mwako. Tanesco hailengi kukufanya uwashe feni na redio halafu useme kila kitu. Hawa wanatakaiwa kutatua mahitaji ya nchi. what is that kila kitu? Kama umenunua inverter ya milioni 5 na betri za milioni 6 na pannel za kutosha na bado unasema ni umeme rahisi basi una matatizo ya maumbile.
 
Wengi tukisikia solar energy tunajawa na hisia kwamba ni jambo la maana sana! Ni umeme mzuri kwa mwanakijiji anayetaka mwanga wa kufukuza wanayama watembeao gizani tu! Kwani nchi zetu hizi maskini hatuhitaji miradi mikubwa kiasi hicho kinacholengwa na TAnesco.

Ni uharibifu wa pesa kwa kujidai kuingia kwenye renewable energy. Ni biashara ya makampuni ya kigeni kujipenyeza ndani ya TANESCO, nao wanaandika eti by 2050 Tanzania itatumia renewable energy, wakimaanisha wind na solar. Huu naweza kuita ni upuuzi.

Solar na wind bado ni luxarious energy sources ambazo tunawaachia nchi zilizoendelea kufanya majaribio. Ni aibu kwa shirika kama Tanesco kujiingiza kwenye miradi ya gharama kubwa kiasi hicho. Maneno kama renewable energy na alternative energy ni kujiridhisha tu na kuwazubaisha wanasiasa na kunufaisha makampuni ya nje ambayo yanatuuzia hizo pannels.

Katika East Africa walianza Uganda. Kwa mikogo wakatangaza kuwa na solar farm, ukweli ni kwamba hilo ni shimo la fedha. Wangeweza kupata umeme mwingi kutoka Nile kuliko hizo pannels. Sasa wameingia Tanesco nao kwa mikogo wanatangaza tender ya kufunga mitambo ya solar. Spain Andalusia inajigamba kuwa na solar farm ya kisasa kabisa na technolojia za kisasa lakini bado ni umwamba tu, wana umeme mwingi kwa njia za nuklia na mafuta.

Je, kwa nini Tanesco inajiingiza kwenye solar? Jibu ni rahisi: Kwanza hawaijui kiuhakika kiasi hicho zaidi ya kusimuliwa na makampuni yanayouza pannel na kutoa mifano ya nchi jirani na ulaya ambako hakuna nchi hata moja ilnayotegemea solar. Mfano mzuri ni ujerumani ambako Angela Merkel aliahidi kuondoa mitambo yote ya nuklia ili kuweka renewable kama hizi wanazokimbilia Tanesco. Tangu 2005 hadi leo hajafika kokote! Kumbuka huyu ni mfizikia, syansi anaijua sana. UK wao waliongeza nuklia na ikajengwa na kampuni ya China. Hivi karuibuni Afrika kusini imejenga nuklia mpya na ni mitambo itakayokuwa mikubwa kuliko yote duniani.

Pili Tanesco kuna tamaa ya kupewa kitu kidogo na makampuni ya nje ili kubeba techolojia ya aina hii ambayo kwa tender kama hiyo, lazima itajengwa na makampuni ya nje.

Bila kujali 2050 nani atakuwa hai, Munachokifanya ni wizi mtupu na hasara kwa kizazi kijacho. Kama muma ubavu jengeni mitambo ya nuklia.

Hilo andiko la renewable energy kuhusu Tanesco liko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanzo chako cha habari sio cha kuaminika nimesoma hiyo link mwanzo mpaka Mwisho ni promo tupu .

Pili kama taarifa ni ya ukweli hatupaswi kuikosoa TANESCO,Solar ni nishati mbadala,sijuhi kama unaelewa maana ya nishati mbadala??Mfano ww una gari Maki X kuna ubaya ukimiliki Vitz au Bodaboda??Kama upeo wako mdogo utaona ni jambo la kishamba lakini wajanja wana miliki gari Kali na bado wanamiliki na bodaboda au Vitz.

Hydro Electricity pekee haitoshi hata kama itazalishwa kwa Mega Watts kubwa kiasi gani lakini sio reliable compared na Solar .

Nakushauri kasome comparison ya Hydro Power Vs Solar au Wind utaelewa kwa mini TANESCO wameamua kumerge hzo Solar/Wind na Hydro.

Harafu hivi vitu ni Very Technical ,Tanesco ina wahandisi waliobobea kwny hzo mambo ww na ka BA kako ka Sociology pale Teku unaleta ka Uzi kako ka kishenzi shenzi .

Mimi nyumbani kwangu hapa Mbezi Luis natumia umeme wa Tanesco na Solar pia na nime design Bio gas system mwenyewe hata kuwe na itirafu kwny grid kwng silali giza wala siwezi lalamika Oryx wakipandisha being ya gesi au mama Kibona akipandisha bei ya mkaa.Mimi ndio mjanja sasa.
Mkuu, nimesoma unavyoandika, unavyopanga maneno yako. Halafu ukasema una vitu unavyojivunia nyumbani, kweli nimesikitika. Kwa ubovu wa uelewa ulionao ulistahili uwe ni shamba boy!

Hakika munaosoma maelezo haya jaribuni kurudi kwenye maelezo yake muone jinsi maelezo yake yasivyoendana na ufahamu wake.
 
Kuna kitu hakiingii akili mwako. Tanesco hailengi kukufanya uwashe feni na redio halafu useme kila kitu. Hawa wanatakaiwa kutatua mahitaji ya nchi. what is that kila kitu? Kama umenunua inverter ya milioni 5 na betri za milioni 6 na pannel za kutosha na bado unasema ni umeme rahisi basi una matatizo ya maumbile.
Have invested not more than 5 millions Rafiki na ukweli utabakia kwamba umeme wa solar ni Bora nafuu na Salama!!!.. matatizo ya maumbile unayo wewe ambae unataka ufanyie kila kitu na serikali bila kujua majukumu yako!!!...
 
Failure! Unajitutumua na elimu haba. Nini maana ya athari za mazingira? Au una maana athari za uchafuzi wa mazingira? Huijui hata elimu ya mazingira inavyotakiwa. Dodoma, Singida, shinyanga na Simiyu ni tatizo la athari ya mazingira kwa maoni yako? Hukusoma geography ya nchi yetu?

Nakupa shule ili kama unaweza upanuke kimawazo. Uchafuzi wa India na China, specifically Beijing unawafanya wavae mask barabarani. Je hiyo ni CO2? Unafahamu kwamba CO2 haionekani? Kweli unaweza kuvaa mask kuzuia CO2 eti hewa ni nzito! What is Nzito? Unachoandika ni yale unayasikia. Hakuna utaalamu hapo!

Unaleta tena mambo ya kukata miti. Umeme unazuia kukata miti? Dar tuna umeme, tumeacha kutumia mkaa? Umeme unazuia matumizi ya mkaa? Nigeria inaongoza kwa kuuza mkaa nje, hiyo ni ukosefu wa umeme? Hakuna uhusiano kati ya kukata miti na kuwepo kwa solar. Ukitaka kufundisha mazingira kwa usiowafahamu utaumbuka.
Vitu vidogo vidogo unataka utafuniwe, kufikirisha akili yako mtu akisema athari za mazingira huwezi..hiyo geography ya kusoma shuleni wewe ndiyo reference yako?? akili ya kudaka daka references hata ambazo hazikusaidii kupata ufahamu halisi kwa jambo fulani nadhani ndio zimedumaza uwezo wa reasoning yako..lakini usaidike, lengo hasa la renewable energy ni kupunguza matumizi yanayotokana na nishati zenye athari kwa mazingira hata kama ni kwa asilimia 1 ikiwepo nishati ya kutosha kutoka vyanzo mbadala itapunguza matumizi ya nishati zinazoharibu mazingira ikiwemo matumizi ya mkaa kupikia, si lazima ninayoandika hapa yakufundishe wewe..you can decide to remain fool.
 
Mkuu, nimesoma unavyoandika, unavyopanga maneno yako. Halafu ukasema una vitu unavyojivunia nyumbani, kweli nimesikitika. Kwa ubovu wa uelewa ulionao ulistahili uwe ni shamba boy!

Hakika munaosoma maelezo haya jaribuni kurudi kwenye maelezo yake muone jinsi maelezo yake yasivyoendana na ufahamu wake.
Shamba boy,sio MTU??
 
Wngn hatujalipiwa ada na serikali kwnd chuo kujifunza kupangilia maneno,we are technical men.Uelewa wko kuhusu maswala ya kihandisi ni zero,ww letaga Uzi za kina Membe na Mbatia Tu basi.
 
Punguani ndio hufikiria kila kitu ni kupigwa!!! mwenye maarifa haoni kupigwa kama kitu cha kwanza..
Hawa ndio wanataka kutuchonganisha na Serikali ya John Magufuli ,ss tushaamua kuunga mkono juhudi za mheshimiwa rais ,usiturudishe nyuma kwa propaganda zako za kishamba.
 
Vitu vidogo vidogo unataka utafuniwe, kufikirisha akili yako mtu akisema athari za mazingira huwezi..hiyo geography ya kusoma shuleni wewe ndiyo reference yako?? akili ya kudaka daka references hata ambazo hazikusaidii kupata ufahamu halisi kwa jambo fulani nadhani ndio zimedumaza uwezo wa reasoning yako..lakini usaidike, lengo hasa la renewable energy ni kupunguza matumizi yanayotokana na nishati zenye athari kwa mazingira hata kama ni kwa asilimia 1 ikiwepo nishati ya kutosha kutoka vyanzo mbadala itapunguza matumizi ya nishati zinazoharibu mazingira ikiwemo matumizi ya mkaa kupikia, si lazima ninayoandika hapa yakufundishe wewe..you can decide to remain fool.
Naona kama umeanza kuwa disorganized. Stop being a hardcore of the green movement! Achana na theory ya energy. hutaki hata jiografia jamani! Ktk nchi hii huelewi ecosystems mbali mbali tulizonazo kweli? ukiona dodoma unadhani waliharibu mazingira!

Kiuchumi na mazingira, bado tuko kwenye big difference ya economic development na equality. Walioko kwenye nyumba ya bati wanadhani wameendelea munaanza kuwaza eti renewable energy.
 
Have invested not more than 5 millions Rafiki na ukweli utabakia kwamba umeme wa solar ni Bora nafuu na Salama!!!.. matatizo ya maumbile unayo wewe ambae unataka ufanyie kila kitu na serikali bila kujua majukumu yako!!!...
Cost-base ya solar nchi hii tunaijua kama umetumia chini ya milioni tano hayo ni mahitaji ya chumba na sebule. Hakuna haja ya kujidai kulinganisha energy mbalimbali kwa matumizi kama hayo.
 
Kwa level ya familia sawa ila Tanesco wanafanya kwa level ya taifa
Hata huo umeme wako uliotumia kwa miaka 6 uliwahi kuangalia gharama ulizotumia kweli?
Solar ni umeme Bora na rahisi sana kuliko unavyopotosha!!!...nimetumia solar hapa Geza ulole kigamboni Dar es salaam miaka 6 sikuona Wala kupata shida ya aina yeyote!!!... tofauti yake uwekezaji wake unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gharama za kuendesha hydroelectric power ni ndogo mno. Gharama za kuendesha mitambo ya gesi inaeleweka kiasi. Sasa hizi wind turbine zina complication kubwa pamoja na kuhitaji maintenance mara kwa mara. Hiyo solar energy haiko reliable sana wala haitoi nishati ya kutosha.
Hakuna haja ya kukimbilia uko kwa sasa.
Samahani lakini, ila wewe ni mjinga nikiwa namaanisha hujui unacho andika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom