Kama nilivyokwambia awali ulaya kwa umoja wao kwenye bara kupambana na climate change wali-commit kupunguza 40% by 2030 output ya GHG kupitia ‘United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCC) hiyo ndio document endelevu iliyokuja na Kyoto Protocol, Doha Agreement and Paris Agreement; inaelezea njia tofauti ya kufikia malengo.
Sasa wanachokifanya EU ni kutekeleza walichokubaliana nchi tajiri katika hayo makongamano.
Ingawa wengine hawapo serious hila EU hili jambo lipo kisheria kila nchi inatakiwa kukata a minimum of 40% and there are sanctions for failure to comply kwa mwanachama yeyote.
Japo block target ni 40% kwa kila nchi, however zinaweza jiongezea wenyewe malengo na kupanga mipango yao watakavyofikia.
Hivyo nchi kama UK wao wame set target zao at 57% reduction compared to 1990 output by 2030.
Hili kutekeleza UK kuna Climate Act 2008 ni sheria mwongozo kama nchi watakavyofikia hayo malengo na njia watakazo tumia ambazo:
- kuhakikisha viwanda vinapunguza GHG kwa kuboresha technology inayochuja CO2 (swala ambalo limepelekea viwanda visivyo na hela ya ku adapt kufungwa),
- kuongeza insulation’s kwenye majumba hili watu wapunguze kutumia nishati ya gas during winter
- kuongeza greener public transport,
- kuongeza matumizi ya renewable energy
- Increase research and development on greener technologies
- kutumia market based instrument ambazo na zenyewe zipo za aina tatu ‘Clean Development Mechanism’ ambapo ukiwekeza third world unapata cheti ambacho kinakuruhusu ku-compensate kuchafua kiwango ulichopunguza africa, ‘Cap and Trade’ mfano unaweza ingia makubaliano na kiwanda in similar industry and size ndani ya EU ambacho kiko chini ya uchafuzi we utumia deficit zao na mwisho Carbon Taxes ikibidi uzidishe unalipia kodi hiyo nyongeza.
Kwa ivyo wanachokifanya wao sio eti ni diversification bali ni malengo waliyojiwekea, hila nchi kama marekani chini ya Trump aitaki upuuzi huo ndio maana imejitoa wao bado wanaamini kwenye umeme wa makaa ya mawe (ndio most reliable source na wenye uchafuzi mkubwa wa mazingira) awataki pressure isipokuwa wamejikita kwenye kuboresha carbon capture technology kupunguza CO2 emission na China pia watafanya hila kwa mtindo wao.
Kwa ivyo wanaofanya ivyo ni kisera zaidi na malengo yao ya lazima sio Investor’s choice bali ni block and national policies; otherwise kila nchi ingependa kutumia fossil sources kuzalisha umeme.
Kama kuna mtu anataka kuja kuwekeza kwenye renewable energy Tanzania kwa hela zake hakuna shida, lakini TANESCO kuweka hela zake wakati nchi bado inahitaji nishati ya uhakika huo utakuwa ni upuuzi wa hali ya juu.