Wengi tukisikia solar energy tunajawa na hisia kwamba ni jambo la maana sana! Ni umeme mzuri kwa mwanakijiji anayetaka mwanga wa kufukuza wanayama watembeao gizani tu! Kwani nchi zetu hizi maskini hatuhitaji miradi mikubwa kiasi hicho kinacholengwa na TAnesco.
Ni uharibifu wa pesa kwa kujidai kuingia kwenye renewable energy. Ni biashara ya makampuni ya kigeni kujipenyeza ndani ya TANESCO, nao wanaandika eti by 2050 Tanzania itatumia renewable energy, wakimaanisha wind na solar. Huu naweza kuita ni upuuzi.
Solar na wind bado ni luxarious energy sources ambazo tunawaachia nchi zilizoendelea kufanya majaribio. Ni aibu kwa shirika kama Tanesco kujiingiza kwenye miradi ya gharama kubwa kiasi hicho. Maneno kama renewable energy na alternative energy ni kujiridhisha tu na kuwazubaisha wanasiasa na kunufaisha makampuni ya nje ambayo yanatuuzia hizo pannels.
Katika East Africa walianza Uganda. Kwa mikogo wakatangaza kuwa na solar farm, ukweli ni kwamba hilo ni shimo la fedha. Wangeweza kupata umeme mwingi kutoka Nile kuliko hizo pannels. Sasa wameingia Tanesco nao kwa mikogo wanatangaza tender ya kufunga mitambo ya solar. Spain Andalusia inajigamba kuwa na solar farm ya kisasa kabisa na technolojia za kisasa lakini bado ni umwamba tu, wana umeme mwingi kwa njia za nuklia na mafuta.
Je, kwa nini Tanesco inajiingiza kwenye solar? Jibu ni rahisi: Kwanza hawaijui kiuhakika kiasi hicho zaidi ya kusimuliwa na makampuni yanayouza pannel na kutoa mifano ya nchi jirani na ulaya ambako hakuna nchi hata moja ilnayotegemea solar. Mfano mzuri ni ujerumani ambako Angela Merkel aliahidi kuondoa mitambo yote ya nuklia ili kuweka renewable kama hizi wanazokimbilia Tanesco. Tangu 2005 hadi leo hajafika kokote! Kumbuka huyu ni mfizikia, syansi anaijua sana. UK wao waliongeza nuklia na ikajengwa na kampuni ya China. Hivi karuibuni Afrika kusini imejenga nuklia mpya na ni mitambo itakayokuwa mikubwa kuliko yote duniani.
Pili Tanesco kuna tamaa ya kupewa kitu kidogo na makampuni ya nje ili kubeba techolojia ya aina hii ambayo kwa tender kama hiyo, lazima itajengwa na makampuni ya nje.
Bila kujali 2050 nani atakuwa hai, Munachokifanya ni wizi mtupu na hasara kwa kizazi kijacho. Kama muma ubavu jengeni mitambo ya nuklia.
Umekosea kwa kuanza kwa kuwakejeli wanakijiji ambao ndio uti wa mgongo wa nchi yetu. Pili kwa kuwadharau wataalamu wetu wa Tanesco kwa kudai kuwa ni vilaza na malimbukeni ambao hawajui maana ya solar energy. Ungeweza kujenga hoja zako bila kuwakebehi wenzako lakini inaelekea ndio mtindo wa kisasa. Sasa hebu tuongelee hili suala la renewable energy ambalo umelivalia njuga:
1. Renewable energy haitokani tu na upepo na jua. Geothermal, biomass, mawimbi (tides) ya bahari n.k. vyote vinaweza kutumika kuzalisha nishati.
2. Renewable energy inaweza kuzalishwa katika scale yeyote ambayo mtu anataka, Kwa upande mmoja, huyo mwanakijiji unayembeza akitaka nishati kwa ajili ya taa ya kusome mtoto wake, kuchaji simu yake na kuangalia luninga anaweza kufunga panels za kumpatia umeme wa kumwezesha kufanya hivyo bila kungoja mradi wa serikali wa kumuunganisha kwenye grid ya taifa.Na wengine ambao wana umeme wa gridi lakini wamechoshwa na huduma zisizotabirika za huo umeme ( ambao kiasi kikubwa unatokana na Hydro) wanaamua kufunga solar system ambayo itamuondolea adha ya kukatika umeme mara kwa mara na wakati mwingine bila taarifa bila kelele zinazotokana na generators. Kwa scale ya miji au nchi, bado the jury is out. Tesla wamefanikiwa Hawaii lakini sio sana Puerto Rico. Kwa upande mwingine wachina wana zaidi ya Giga Watts 174 za Solar capacity. Lengo lao ni ifikapo 2050 watakuwa na Giga watts 1,300.
3. Hakuna mtu anaesema kuwa traditional sources zote za umeme zifungwe mara moja na tuhamie wote kwenye renewables. Lengo kubwa ni kudiversify na kuacha utegemezi wa traditional sources kama makaa ya mawe ambayo sio tu uungazaji wake unachafua mazingira lakini hata uchimbaji wake ni hatari na sehemu nyingi duniani unashindwa kushindana na vyanzo kama gesi asilia. Pamoja na mbwembwe zake Trump ameshindwa kufufua machimbo mengi ya Appalachian kwa sababu hayalipi. Hao wajerumani unaowabeza mwaka 2012 21.9 % ya umeme wao ulitokana na renewables, mwaka 2017 38%. Wakati huo huo matumizi ya makaa ya mawe yameshuka kwa 16%. Kwa mara ya kwanza, mwaka 2019 renewable sources zimetoa umeme zaidi ya wa nuklia na makaa ya mawe kwa pamoja. Merkel aliahidi kuwa Nuclear plants zote zitafungwa ifikapo Disemba 2022 na tayari mwaka 2016 walikuwa wameishafunga 9 kati ya 17.
4. Kuna dhana kuwa umeme wa hydro ni wa bei nafuu kuliko mwingine. Hii si kweli, hasa uki factor in gharama ya athari kwa mazingira, unpredictable nature yake n.k. Hapa kwetu, mojawapo ya vikwazo vikubwa kwa industrialization ni bei ya umeme wetu ambao kwa kiasi kikubwa ni wa hydro.
Ingawa natofautiana na wewe katika dhana yako ya kupigia debe Hydro na makaa ya mawe kama mkombozi wetu, nakubaliana nawe kuwa kuwekeza katika mradi mkubwa wa solar sio sahihi. Miradi midogo ya kati iliyotawanywa nchi nzima itakuwa more effective kwa vile tuna bahati jua linawaka kila sehemu ya nchi yetu. Aidha, serikali ingewawezesha wananchi kufua umeme wa renewable majumbani mwao, mashuleni n.k. kwa kupunguza gharama za uwekezaji kwa masharti kuwa umeme wa ziada wataweza kuwauzia Tanesco. Kwa kufanya hivi tutapunguza gharama za transmission na distribution. Ujerumani na nchi nyingine za magharibi zimefanya hivi kwa mafanikio makubwa. Vile vile viwanda ambavyo vinaweza kutengeneza umeme kutokana na process zao ( Cogeneration ) zipewe motisha wa kufanya hivyo. Kwa wenzetu ( Brazil, Mauritius n.k.) viwanda vingi vya sukari vinatumia bagasse wanayozalisha kuzalisha nishati kwa ajili ya shughuli zao. Umeme wa ziada unaweza kuuzwa kwa Tanesco ambao watawauzia wananchi.
Tunachohitaji hapa kwetu ni kuwa na sera ya ku diversify uzalishaji wetu wa umeme na kuondokana na source ambazo zinaweza kutuletea matatizo hapo baadae. Tungeweza kuwekeza katika umeme wa gesi asilia wakati tunaendelea na miradi ya vyanzo vingine vya umeme. Badala ya kutaka taasisi kama Tanesco kuhodhi uzalishaji wote wa umeme, serikali inatakiwa iwawezeshe wote wenye uwezo wa kuzalisha umeme (hata mdogo kiasi gani) kufanya hivyo ili kuipunguzia Tanesco mzigo.
Elon Musk sio mjinga kuwekeza katika solar. Hata wachina na wajerumani nao sio wajinga kuwekeza humo maana ndiko sote tunakoelekea. Kudhani kuwa mito ambayo kila mara inashindwa kujaza Kihansi, mtera n.k. itakuwa inajaza Stiegler kila mwaka ni kujidanganya.
Amandla......