TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

We jamaa una akili sana, big up mazingira na nishati endelevu.
 
Unaposema renewable energy ina gharama kuendesha una maanisha nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Gharama za kuendesha hydroelectric power ni ndogo mno. Gharama za kuendesha mitambo ya gesi inaeleweka kiasi. Sasa hizi wind turbine zina complication kubwa pamoja na kuhitaji maintenance mara kwa mara. Hiyo solar energy haiko reliable sana wala haitoi nishati ya kutosha.
Hakuna haja ya kukimbilia uko kwa sasa.
 
Kumbukeni miti inapungua kwa kasi, mto Ruaha ambao unaishia kuwa Kilombero na Rufiji haukuwa kama ulivyo sasa, hali ya sasa ni moja ya tatu ulivyokuwa mpaka mwishoni mwa sitini. Mto Ruvuma umepungua kwa zaidi ya nusu, mto Wami nao ndiyo huo umebaki jina, mto Ruvu uliokuwa ukifurika mpaka Mlandizi sasa umebaki ndani ya korongo tu na Pangani limebaki jina na kwa wale wanaoujua mto Songwe uliokuwa ukibadili utaifa wa wanyakyusa mara wamalawi mara watanzania Mao umebaki kwenye korongo. Hivi sasa nishati usalama ni ya jua, upepo na joto la aridhini, swala la nuklia tusiliguse kwani tutishia kuingamiza nchi kwa uzembe na mbwembwe za kisiasa.
Kufa kwa miradi ya nishati ya sola kunaweza kutokana na uzembe wa kutoikagua mara kwa mara tukimuachia mwenyezi Mungu aiangalie, tukumbuke eneo la Mnazimmoja mpaka stesheni na Tazara Dar ziliwekwa kamera za CCTV lakini hazikudumu kwa kukosa uangalizi.
 
Una uhakika na unaelewa unachokisema?? wewe unaangalia gharama ya pesa tu, vipi mvua zinapopungua na maji ya mabwawa kupungua, nini gharama yake kwa maisha ya binadamu?? kuna chombo duniani kisichohitaji maintenance?? ikiwa hta mwili wa binadamu unahitaji maintenance, chombo je??..,au maintenance kwako ni pale kunapotokea uharibifu?? megawat 100 za HEP zina nguvu tofauti na megawat 100 za solar??? nini maana ya haitoi nishati ya kutosha...
 
Solar ni umeme Bora na rahisi sana kuliko unavyopotosha!!!...nimetumia solar hapa Geza ulole kigamboni Dar es salaam miaka 6 sikuona Wala kupata shida ya aina yeyote!!!... tofauti yake uwekezaji wake unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika

”umeme bora na rahisi...tofauti Yake...unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika” kauli yako inajichanganya Mkuu, ukisema Bora naelewa Utaalam unao na ukisema Rahisi ina maana Pesa zipo. Sasa tatizo ni nini?
 

Mzee unaongea very selfishly

Unajiangalia wewe mpaka utakapokufa

Huangalia miaka 1,000 from now utaiacha dunia katika uharibifu kiasi gani

Wewe unaona,nipo hapa,jenga umeme mwingi kwa fossils kadiri ninavyoweza then haya ma CO2 na house gasses yajae yaharibu dunia mimi nitakua nishakufa watajiju hao watakao kuwepo!

Bro,kwa selfishness kubwa kiasi hiki aisee hatuwezi fika!

Solar au wind au geothermal or whatever renewable energy source is,sio lazima upate wewe faida leo,weka punguza house gas emission kwa faida ya vitoto vyenu miaka 200 from now!

Nigga stop this nonsense!

Huweki kwa ajili yako leo wewe mamalia mwenzangu!

Stop this monkey see monkey do!
 
We mtu unamtukana mwenzako lakini nikisoma ulichoandika, it's another piece of rubbish! Zygot anaonesha anayafahamu yote hayo, wewe unajificha kwenye kichaka cha mazingira na hapo ndo mimi nakuja na uelewa wangu. Wewe ni mzembe. Tanesco kwa ujumla hawajaweza hata kuzalisha umeme wa kujivunia. Angalia energy partitioning ya China nchi ambayo imeendelea hivi karibuni kabisa kwa kutumia nishati ya coal. China ndo nchi yenye bwawa kubwa la umeme duniani.

Kimazingira, Third world bado tunaruhusiwa kutumia mkaa tulionao kwa makusudi na jumuiya ya kimataifa, wanfahamu njia hizo zingine kweli ni luxurious! Wenyewe tumefanya commitment ya kutimiza matakwa ya kimazingira kwa kadri tunavyoweza, siyo tunavyolazimishwa (Paris Agreement). Sasa wewe unakuja kwa mkwara na matusi utadhani hata mazingira unayafahamu.

Kwa upande wa energy, niambie third world gani iliyojiingiza na kufanikiwa kwenye upuuzi huo unaokutia kiwewe hata umtukane mwenzako? Dar imejaa wapuuzi wadanganyifu wanawapiga watu pesa kwa solar kwa sababu ya uzembe wa Tanesco kuwapa umeme wa uhakika. Mbaya zaidi kwa tamaa ya upigaji, wizara nayo inatoa support ya kusambaza solar badala ya umeme wa grid. Nani anaweza kusaga mahindi kwa solar? Nani anaweza kuranda mbao kwa solar? Gharama gani ataitumia kuweka miundo mbinu kama hiyo ukilinganisha na umeme wa grid kuu? Ukimuona mwenzako mpuuzi, nawe usiweke upuuzi.

Kama nawe uko Tanesco kwa hilo ni upuuzi. Wekezeni kwenye mkaa, wekezeni kwenye mini-grids, wekezeni kwenye thermal ambako Kenya walishafanya, ninyi tunawasikia miaka miingi bila kufika kokote na ghafla tunawaona kwenye solar. Hizo ni dili na makampuni ya nje tu!
 
”umeme bora na rahisi...tofauti Yake...unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika” kauli yako inajichanganya Mkuu, ukisema Bora naelewa Utaalam unao na ukisema Rahisi ina maana Pesa zipo. Sasa tatizo ni nini?
Bora na rahisi kutokana na muda kwamba ukishafunga hutozwi chochote Wala shida ni fedha hizo!!!...To me Solar ni the best because ninao na ninaendelea kuutumia!!!
 
Ni kweli boss!
Naona Tanesco wameingiza kundi la watu kutueleza tunachokifahamu kuliko wao. Solar ni tatizo kubwa kuliko hata wind! Storage ya umeme ktk solar bado ni shida ya Dunia ndo maana umebaki kuwa ni umeme wa mchana tu! Wana mazingira na wale waliokariri kama hawa wanaotetea, wanaifagilia sana lakini ni matumizi mabaya ya pesa kwa dunia ya tatu kwa kipindi hiki.

Wind imekuwa ni gharama kubwa pia ingawa unaweza kuzalisha hata wakati wa giza. Bei ni mbaya. mitambo inayozalisha 2 MW inaweza kukupeleka hadi shilingi bilioni 4! na bado unadaiwa matengezo na hadithi kibao maana wind mill za sasa ziko computerized.

Mi naunga mkono, Tanesco waache mzaha na maisha yetu! Niko tayari ku-debate nao kama watajitokeza hapa JF
 
Bora na rahisi kutokana na muda kwamba ukishafunga hutozwi chochote Wala shida ni fedha hizo!!!...To me Solar ni the best because ninao na ninaendelea kuutumia!!!
Siyo kwamba hutozwi chochote bali umelipa zaidi ya yule wa grid ya taifa.
Tanesco ina jukumu la kitaifa siyo la familia yako unayewasha taa na kunyoa ndevu na ... Unapotoa umeme wa kitaifa, ukumbuke kuna wanaoyeyusha vyuma chakavu, kuna wanaohitaji kuendesha mitambo ya madini, kuna wanaotaka kuwa na textile industries. Hapo kuna solar gani ya kutumia ili ufanye kazi usiku na mchana?

Tanesco wanafanya majaribio kwa faida yao badala ya kutafuta umeme unaoeleweka.
 
Uko kwenye anga isiyokuwa yako. Nani kasema mvua zinapungua? Au umeona msimu wa mwaka jana? Umesoma taarifa za IPCC zinasema nini kwa kanda ya East Africa? Tena hadi 2045! Soma taarifa ya 5 kabla ya kuja na hadithi za kubuni.

Then, yes! 100 mw za HEP ni tofauti na 100 mw za solar. Za HEP zipo usiku na mchana niambie za solar unazitunza kwa gharama kiasi gani ili ziwepo usiku?
Stop bhla! bhla bhana!
 
Nadhani hauna uzoefu mkubwa kwenye sector ya Solar. Naomba upate facts zifuatazo:
1. Tanesco haimiliki solar farms, wala haina mpango wa kuwekeza kwenye solar farms kwa sasa.
2. Tanesco wananunua umeme wa solar kutoka kwa IPP (Independent Power Producers).
3. Tanesco inaingia hasara kwa kuzalisha umeme kwa majenereta, maeneo hayo wakinunua umeme wa jua toka kwa IPPs ambao wananunua kwa bei ndogo hakuna shida yoyote.
4. Kwa hali ilivyo sasa IPPs wote wa Solar Farms wanauza umeme chini ya bei wanayonunua wateja kwa kila unit. Mfano Tanesco ananunua umeme wa solar kwa Sh 250, yeye anauza Sh 350.
5. Changamoto ya Solar ni maeneo ambayo Tanesco haipo kabisa, kama vijijini ndani ndani kabisa au visiwani, hapo Solar inabidi ifungwe na Battery na Generator, Initial Investmest cost inakuwa juu sana, hivyo kupelekea gharama per unit zifike hata Sh 2000.
6. Tanzania tuna opportunity kubwa sana ya kuzalisha umeme wa jua, uzuri ni kwamba serikali yenyewe haitoingiza hata Sh Tano, wenyewe waruhusu tu wananchi kuiuzia serikali umeme, namna hiyo makampuni ya solar yatakuwa yanaingia mikataba na wenye nyumba, wanafunga solar panels juu ya nyumba zao, umeme unaingia Tanesco, Tanesco wanamlipa mwenye panels ambaye yeye naye atamlipa mwenye nyumba kwa kukodisha paa lake.

 
Hizi Habari zimetoka kwny chanzo gani cha Habari??tuanzie hapo kwanza.
 
Hizi Habari zimetoka kwny chanzo gani cha Habari??tuanzie hapo kwanza.
Binafsi pia huwa niko kinyume sana na energy hii ya solar. Huyu munayemuuliza atakuja na jibu lake lakini kinachoonekana ktk taarifa ni hiki, bonyeza hapo chini. Vyovyote ilivyo, Tanesco imejiingiza kwenye zoezi baya lisiloisaidia kutatua matatizo ya power ya nchi. Rais aliwaonesha wazi kwamba kuna mini-hydro nyingi ambazo hawazipi support, ndo wakastuka. Sasa tena wanakuja na support ya watu wa solar. Sijui wazo kama hilo wamelitoa wapi? Au ni nguvu ya watu fulani wanaotafuta biashara na Tanesco., ipigwe tena!
TANESCO LAUNCHES 150 MW SOLAR TENDER IN TANZANIA
 
Hichi ulicho kizungumza mkuu hata mwanafunzi wa Physics form two atakucheka sanaa, mkuu rudi darasani kajifunze topic ya sustainable energies ipo form two binafsi mimi niliwahi kuwa mwalimu miaka ya nyuma hizi ndio mambo zangu.
 
Chanzo chako cha habari sio cha kuaminika nimesoma hiyo link mwanzo mpaka Mwisho ni promo tupu .

Pili kama taarifa ni ya ukweli hatupaswi kuikosoa TANESCO,Solar ni nishati mbadala,sijuhi kama unaelewa maana ya nishati mbadala??Mfano ww una gari Maki X kuna ubaya ukimiliki Vitz au Bodaboda??Kama upeo wako mdogo utaona ni jambo la kishamba lakini wajanja wana miliki gari Kali na bado wanamiliki na bodaboda au Vitz.

Hydro Electricity pekee haitoshi hata kama itazalishwa kwa Mega Watts kubwa kiasi gani lakini sio reliable compared na Solar .

Nakushauri kasome comparison ya Hydro Power Vs Solar au Wind utaelewa kwa mini TANESCO wameamua kumerge hzo Solar/Wind na Hydro.

Harafu hivi vitu ni Very Technical ,Tanesco ina wahandisi waliobobea kwny hzo mambo ww na ka BA kako ka Sociology pale Teku unaleta ka Uzi kako ka kishenzi shenzi .

Mimi nyumbani kwangu hapa Mbezi Luis natumia umeme wa Tanesco na Solar pia na nime design Bio gas system mwenyewe hata kuwe na itirafu kwny grid kwng silali giza wala siwezi lalamika Oryx wakipandisha being ya gesi au mama Kibona akipandisha bei ya mkaa.Mimi ndio mjanja sasa.
 
Kwanza ni kuonyesha kutoelimika kutetea chanzo cha taarifa usichojua basis za kuandaliwa kwake, taarifa haitaji walichoona nchi kwa nchi, ni taarifa ya jumla, lakini huhitaji kuelimishwa kufahamu athari za kimazingira zilizotokea ndani ya kipindi cha miaka 20 nchini mwetu, mito na mabwawa kukauka, mvua zisizotabirika, miti ya asili kupotea, wanyama kufa na kuhamia maeneno mengine nk, wakati haya yanatokea Tanzania predictions za report kama hiyo uliyoquote zilisema hali tofauti kabisa..kama akili unazo utajua kitu gani sahihi cha kufanya kulingana na kinachotokea na si kinachotabiriwa..kwa hiyo maisha ni usiku na mchana tu?? mabadiliko ya misimu ya mvua, joto, baridi kwako hayo si sehemu ya maisha...jua lipo kila siku toka uzaliwe na utakufa utaliacha, mvua ni zile zile kila siku??? HEP inaweza zalisha nishati ya hata mwezi mmoja ukaiihifadhi mahali??? akili ya kuku, ni ya kutizama kitu kimoja, na kudhani mwisho wa maisha ni pale yeye anapokufa, ndio wewe..
 
Tufanye lile tunaloliweza hizi nyingine ni mbwembwe tu..
 
Sijui wazo kama hilo wamelitoa wapi? Au ni nguvu ya watu fulani wanaotafuta biashara na Tanesco., ipigwe tena!
Punguani ndio hufikiria kila kitu ni kupigwa!!! mwenye maarifa haoni kupigwa kama kitu cha kwanza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…