DOKEZO TANESCO Arusha inawanyanyasa Wafanyakazi Wake

DOKEZO TANESCO Arusha inawanyanyasa Wafanyakazi Wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,394
Reaction score
1,434
Lengo la uzi huu ni kuitaka serikali iwe makini na utendaji wake, na pia kuwataka wananchi wazinduke na kupinga matendo maovu yanayoendelea nchini.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kule mkoani Arusha limekuwa na historia kwa muda mrefu sasa ya kutojali wafanyakazi wake pamoja na maslahi yao hasa wale wafanyakazi wa chini.

Shirika hili kubwa la kiserikali kule mkoani Arusha limekuwa na tabia ya kutowalipa mishahara wafanyakazi wao wa chini kwa muda mrefu na pia hawawalipi kwa wakati huku maslahi yao mengine yakiingia kwenye mifuko ya watu binafsi. Vile vile viongozi wa mkoa huo wamekuwa na tabia ya kuwafanyisha watu kazi pasipo kuwapa mikataba, hali inayopelekea maslahi ya watu wao kunufaisha watu wachache wenye tamaa za mali.

Viongozi hao pia wamekuwa na tetesi za kupunguza wafanyakazi hao kwa njia zisizo rasmi na hii inatia wasiwasi kwa umma. Vile vile viongozi hao wamekuwa hawawapi wafanyakazi hao stahiki zao zinazotokana na kufanya kazi baada ya muda wa kazi kupita (overtime) na pia zitazotokana na Safari za nje ya wilaya, wamekuwa wakiwanyonya.

Tunatoa wito kwa serikali iwe makini na utendaji wake na iweze kudhibiti matendo maovu yanayoendelea kwa siri nchini. Vile vite tunatoa wito kwa wananchi wasifumbie macho maovu yanayoendelea nchini. Lengo ni ili sote tuijenge nchi yetu kwa pamoja na asiwepo wa kumrudisha mwenzake nyuma.

Wasalaam!
 
Back
Top Bottom