TANESCO board split on MD Rashidi's fate


Sasa kuna tatizo gani na hili? na si ndio maana halisi ya "Great Thinkers?"
Lazima wanaJF mkubali kuwa maoni yanayotoka hapa ni uchambuzi tosha wa hoja yoyote inayaojitokeza jukwaani.
Anayeogopa kunukuliwa ana njia mbili, aidha kuretract tamko lake au kuliweka katika proper perspective kama amenukuliwa vibaya.
Mtu hata akijiita "Mwandishi wetu" mpigie Mhariri Mkuu wa hilo gazeti na umpe tamko lako halisi.
This is an open forum na sidhani kama kuongea hapa ni kuongelea kwapani.
 
Nawapongeza Kulikoni kukubali kuwa JAMIIFORUMS sasa ni uwanja wa kuchota mawazo, badala ya kuwashambulia mimi naona tuwa-incourage maana itwafanya watanzania wengi wasiojua kuwa kuna jamvi hapa watakuja na wakija tutapata tija ya mabadiriko tunayoyataka. Magazeti mengine igeni Kulikoni njooni hapa mtapata news Bin Newz
 

kweli ila wasiandike kishabiki

ukianza na habari; KATIKA HALI ISIYOTARAJIWA YULE MH.XX, tayari umeshajiweka kwenye kundi au una hidden ajenda!
 
Kuna mtu hapa nimeshitukia kama ni mwandishi wa habari wa hilo gazeti ila anataka tu maoni yetu
kwa herini muwe na kazi njema
 
Nashangaa mawazo ya Zitto ni kama ya rais vile akisema kitu basi kinakuwa,....this sense of inferiority imetuweka wazi sana watanzania tulivyo. vita ya maneno na mawazo mapya watu waoga hivi ndio maana hata EAC hatutaki!

sad and shame.


Hapana Zitto tangu alioibua ufisadi wa Buzwagi amekuwa na wafuasi wengi ndani na nje ya nchi ambao hufuatilia kwa karibu yale yote yasemwayo na Zitto au maamuzi yake mbali mbali. Ndiyo maana utaona kauli yake ya kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans ilianzisha mjadala mkali sana hapa jukwaani na nchini pia.

Pia uamuzi wake wa kugombea Uenyekiti wa CHADEMA na baadaye kujitoa ili kuhakikisha mshikamano ndani ya CHADEMA pia ulizua mjadala mkali sana.

Hivyo hakuna la ajabu lolote pale waandishi wa habari wanapomuandika zaidi Zitto kuliko Kikwete. Kikwete yuko busy na uVD na mambo mengi yanayojiri ndani ya nchi ameamua kuwa bubu kutokana na udhaifu mkubwa aliokuwa nao.
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.




Zitto

Zitto una maana gani haswa unaposema habari hii "imeandikwa kwa nia mbaya"?Ulishasema unaplay devils advocate,so then why worry?maana kuplay devils advocate ni kutaka kuchochea mjadala ili uweze kupata maoni mengi zaidi,na haina maana kuwa na uamuzi wa upande mmoja,is that right?Lakini kwenye issue hii tayari una maamuzi,kama unaplay devils advocate then hitimisho lako nini?

Kwasababu hakuna hata moja lililoandikwa kwenye makala hapo juu ambalo ni uongo,kama lipo liweke wazi.Usikimbie Mh,unless iwe ni guerila tactic ya kufight and runaway and live to fight another day?lol! Umesema unachochea mjadala,hilo siyo kweli kwasababu maamuzi yako tayari yanajulikana,na ulishasema you're a man of principle,ni vyema basi ukasimamia misimamo yako na si kukimbia kivuli chako,Bob Marley anakwambia you can run away but you can never run away from yourself.

Zitto one thing you need not to forget during your leadership especially when issues on the table zina impact wananchi either directly ama hata indirectly is empathy,put yourself in wananchi's shoes and you'll know where iam coming from...Kuwakimbia si solution...Ukithibitisha kuna lililosemwa la uongo kwenye hiyo makala na ni kwa kivipi makala hiyo ina nia mbaya na maslahi ya Tiafa basi nitaanzisha thread ya wana jf kukuomba radhi.
 
ina maana KULIKONI hawana jina la MWAANDISHI ? wanaogopa nini?


oili inamaaan hawa kulikoni hawawezi kuandika JAMIIFORUMS.COM


its about tgime wan JF mkahit back on these people
Mwandishi amesema habari katoa jamii forums.kunanini wadanganyika?tujadili ya Zito je rashidi pekee ndo bora aendelee au awapishe wengine?Kama kuna data watu washushe humu.kwanini aendelee au kwa nini asiendelee. NDO hoja hiyo.Siyo mwandishi jamani.Na ubora wa mtu tuangalie alipo ingia unit za umeme zilikua ngapi na sasa ni ngapi. Mgao wa umeme je ulikuwa ni mara ngapi kwa wiki au mwaka je nasasa hali ikoje.sisi mapato ya tanesko hayatuhusu. garama ya umeme umepada au kupungua.
 
Ninashtuka kitu kimoja! tokea huko kwenye thread hiyo ya tanesco na hata hapahapa wanaomtemtea/msimamia huyo Zito ni wanachama wa chama cha mafi***di hii ndo nini!! Huyu mtu ni mtatanishi saana....... sijawahi kuona.
 
Hivi Tina ni nani aliyekwambia kuwa huyu Zitto wa JF ndiyo mbunge?
Yeye hajasema amekuwa misquoted bali habari haijaandikwa kwa nia njema. Hebu angalia mjadala ulivyoenda kuunganishwa na DOWANS, RICHMONDS etc. Km ishu ni kumtetea Rashid kwanini wasiizungumzie hiyo? Tena basi wameacha hoja za msingi alizozungumza juu ya Rashid. Kwanini hawakuwepo evidence alizotoa Zitto kama wanataka kuwa objective? Nini kitufanye tuaamini waliandika kwa nia njema na kama si kuachafuana?
 
Hivi, Zitto anaposema kuwa Rashidi ni one of the best CEOs wa Tanzania. Akatoa track record yake alipokuwa BoT na kumwagia sifa tele za "msimamo" wake wa kukataa kuburuzwa na wanasiasa. Tena akatumia takwimu ambazo bila shaka amezipata kupitia cheo chake kama m'kiti wa kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kusema kuwa eti Rashidi ameweza kuboresha hali ya kipato ya Tanesco. Sifa zote hizi kede kede zimetolewa kukiwa na mjadala mkali juu ya Rashidi na hatma yake. Je, ni upotoshaji au uandishi uchwara au malice kusema kuwa Zitto ampigia debe Rashidi? Wote tumeshuhudia humu kwenye JF how Zitto went out of his way to shower lavish praise on Rashidi.

Kuhusu
gazeti la KULIKONI ku pick mjadala wa JF na kuandikia habari, nadhani ni jambo la kusifiwa na kuigwa kwani linathibitisha kuwa JK ni Home of Great Thinkers kweli na vile vile linasaidia kuleta umaarufu zaidi kwa JF na kusambaza mijadala ya humu ndani kwa umma wa Tanzania. Tukumbuke kuwa ni asilimia chache sana ya Watanzania wenye access ya Internet. Long live JF, magazeti muwe huru kusambaza mijadala ya JF ili Watanzania wote mijini na vijijini waweze kuchangia mawazo yao.
 
Hebu pitia tena hiyo habari uone ilivyo bias km inania njema katu isingekebehi na kuunga ishu na kuchanganya mada. Mbona hoja alizotoa Zitto hazipo wazi? Lakini hata hivyo Kulikoni imekuwa ikiandika saana kuhusu Rashid ilikuwa ni lazima habari iwe vile ili wasijicontradict na makala zao za siku za nyuma.
 



He he he he ndg yangu kwenye accounts ukiwa na Qualified opinion kwenye accounts manake hesabu zako zina mushkeri na ndio maaana wakaguzi wanaqualify... na kama accounts zako hazina kasoro basi opinion inayotolewa ni Unqualified audit opinion. Ni tofauti na ulivyozoea kuelewa qualified na unqualified... kwa hiyo kama audit inaonyesha Qualified opinion manake mushkeli hapo kaka/dada
 
Huyu mwandishi amefanya vibaya, wala asiwepo mtu wa kumtetea. Endapo angekuwa fair angetaja hoja za Zitto kumtetea Dr. Rashid, yeye amechukua one side of the story.

Tatizo la media za bongo, zimegawanyika katika makundi yaani zinazotetea mafisadi na kuwalima wapiganaji na zile zinazowalima mafisadi na kutetea wapiganaji. so, hii ni vita btn media groups na masalahi binafsi.

Hata hivyo, nikuambie Mhe. Zitto kwamba upande uliouchagua ktk hii issue ya umeme unachangamoto nyingi kuliko fursa. Ingekuwa ni SWOT analysis ingebidi uachane kabisa na hii issue.
 

Jamani, KULIKONI kama yalivyo magazeti mengine hapa Tanzania lina mapungufu yake. Lakini pia lina mema yake. Lazima tuseme ukweli kuwa kwenye hii habari yao wamemnukuu Zitto extensively. Nimehesabu sasa hivi gazeti hilo limetoa zaidi ya paragraph 6 kueleza "hoja" kama sio "Vioja" vilivyojengwa na Zitto kumtetea (kumbeba) Rashidi. Zifuatazo ni direct quotes kutoka kwa Zitto zilizo andikwa na gazeti hilo...


"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya www.jamiiforums.com.

Zitto alipuuza kauli hizo akisema: "Nimesema hili (la rada) ni suala la mahakamani na tushinikize wanaotajwa wapelekwe mahakamani na mahakama ndio pekee zenye mamlaka ya kusafisha mtu au kuhukumu.

"Sijaona hoja hii (ya rada) imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale Tanesco. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.

"Kinachonipa tatizo ni jinsi watu walinvyoline up (jipanga) kuchukua nafasi pale Tanesco ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote,"alisema mbunge huyo na kusisitiza suala hilo bado halijathibitishwa na Mahakama
 



Mwandishi hanan makosa .. na ameeleza wazi kwamba amepatat habari toka mtandaoni. Pia kazi ya mwandishi ni kuandika .. na Zitto kamam mbunge akitoa maoni yake watu wataandika .. hakuna cha ajabu hapo.
 



Na kwa kusema ukweli Kulikoni hawajaongeza chumvi.. walichoandika ndicho ambacho Zitto unatetea hapa .. kwa hiyo hata kama hawakukutafuta huo ndio msimamo wako .. labda kama hukutaka na watu wengine nje ya JF wajue unachosimamia. juu ya Dr.. lakini ukweli unabaki pale pale kuwa unampigia debe Rashid .. na kwa kuwa wewe unasema unasimamia unachoamini basi nenda kwa umma ukamtee your "best CEO".hakuna sababu hata chembe ya kuwalaumu Kulikoni .. wamefanya kazi yao .. upashaji wa habari na wameeleza habari wameitoa hapa .. sio yao .. sasa whats wrong with that?
 
Hivi bado hamjamstukia dogo Zitto alikwishatekwa na mafisadi siku nyingi.
 
Kibs Umemwona Chairman wako akibembea kule Jamaica....."angechoka" ghafla ingekuwaje pale LOL

Si tu lazima achoke. Anaweza akapita karibu na pwani na akaona akina Shaggy wana shoot video na zile totoz za Kilimanjaro Ze bia. Hapo kunakuwa na mfadhaiko na uchovu kwa papo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…