Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 581
Kauli hiyo ya Zitto aliyoitoa kupitia mtandao wa mijadala wa Jamii, imekuja ikiwa ni baada ya gazeti hili kubainisha kuwa jina la Idris limepenyezwa Ikulu ili ateuliwe kuendelea na wadhifa huo, hali ambayo imesababisha mgawanyiko katika Bodi ya Tanesco ambako baadhi ya wajumbe wameukana uamuzi huo kuwa si wao.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye alisema akirejea nchini atachunguza suala hilo kwani inawezekana hata yeye amerukwa kwa kutofahamishwa mchakato huo. Ngeleja kwa sasa yuko na Rais Jakaya Kikwete, nchini Jamaica na baadaye watakwenda visiwani Trinidad na Tobago.
"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya www.jamiiforums.com.
Kwa vile mimi ndiyo niliweka post hii, naomba kuwajulisha kuwa kwenye habari hiyo ya Kulikoni kuna attribution kuwa mjadala huo wa Dk. Rashidi uko kwenye JF. Nadhani pia kwa wanaosoma Kulikoni kila mara wanafahamu kuwa gazeti hilo mara nyingi hawaweki majina ya waandishi wao hadharani