TANESCO board split on MD Rashidi's fate

TANESCO board split on MD Rashidi's fate

Kaka analysis nzuri sana.

Unawajua “wazee wa data” wetu hapa JF. Unadhani wana uwezo(capacity), haiba (caliber) ama mamlaka ya kimaadili (moral authority) kuachwa kuwa waamuzi wa mawazo ya wananchi na hata kutaka kutuamulia hatma ya nchi yetu?

omarilyas

Omar, Asante. Suala la capacity na caliber za Wazee wa data wa JF ni relative tuu kutegemeana na mazingira, time na place, lakini hapa JF, hakuna waamuzi wa mawazo ya wananchi, bali watoaji wa mwelekeo wa kuchambua sifa na kupanga malengo bila kujadili utekelezaji, inapofikia kufikia maamuzi ni wananchi wenyewe huamua kwa kura zao.
 
Yes!
Huyo mwenye bold hapo juu ni mhandisi na amekuwa wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1984, anajua details kibao kuhusu wizara na Tanesco, na kwa sasa ni kamishna msaidizi wa nishati jadidifu (Renewable energy) pale wizarani.

Hii inasaidia nini kuongoza shirika uongozi ni utawala mjamaa na sio utaalama wa copper wire au fiber wire. Kuhusu wenyekuwa na ufahamu na Tanesco mkisema hivyo ndio matokeo yake mnateua watu bomu kwanini wazungu wanataka kuwapo na independence ndani ya bodi!! Jibu simple tunataka uhuru wa maamuzi sasa utapata independence na jitu lilikuwa mfanyakazi wa Tanesco miaka iliyopita kweli????

Msitudanganye jamani
 
Yahitaji ujasiri usio wa kawaida kuwatetea watu kama akina Rashidi - swali ninalobaki nikijiuliza ni huu ujasiri unajengeka katika misingi ipi. Kuna wakati huyu Rashidi alitishia kujiuzulu akitoa sababu za kuingiliwa na wanasiasa katika maamuzi. Lakini inavyoelekea hivi sasa, pamoja na mkataba wake kwisha, ni wazi bado anautaka uCEO wa TANESCO na kuna watu wanaendelea kumpigia debe - eti one of the best CEOs Tanzania ever had ! Jamani, halafu wanaomsifia Rashidi si ajabu ukawakuta ni wale wale wanaomsifia JK kama the best President Tanzania ever had ! Nachoka na Watanzania !
 
Yahitaji ujasiri usio wa kawaida kuwatetea watu kama akina Rashidi - swali ninalobaki nikijiuliza ni huu ujasiri unajengeka katika misingi ipi. Kuna wakati huyu Rashidi alitishia kujiuzulu akitoa sababu za kuingiliwa na wanasiasa katika maamuzi. Lakini inavyoelekea hivi sasa, pamoja na mkataba wake kwisha, ni wazi bado anautaka uCEO wa TANESCO na kuna watu wanaendelea kumpigia debe - eti one of the best CEOs Tanzania ever had ! Jamani, halafu wanaomsifia Rashidi si ajabu ukawakuta ni wale wale wanaomsifia JK kama the best President Tanzania ever had ! Nachoka na Watanzania !

Na utachoka sana na kijiba chako hicho!
 
Napenda mijadala iwe hivi, hii ndiyo standard ya JF.

Nakiri kutomjua Dr. Rashid na kutokuwa na data za uzuri wake au ubovu wake. Hata hivyo nashawishika kuungana na wanaotaka aondoke kutokana na sababu kadhaa

(a) Kashfa ya radar ni kubwa na Dr angekuwa makini angekwa ametolea maelezo. Katika suala la kashfa huwa halihitaji mahakama kudhibitisha ndo mhusika awajibike. Anatakiwa awajibike na endapo mahakama ikijakumsafisha ndipo anapopata heshma zaidi. But as for now Dr. Rashid hana credibility ya kuwa CEO wa TANESCO.

(b) Hata kama ni mtendaji mzuri, bado tunahitaji mtu mwingine mchapa kazi zaidi. CEO wa TANESCO ni mtu mkubwa kazi hiyo ilipaswa kutangazwa internationally hata akija mzungu poa tu.

(c) TENESCO anahitaji mtu mwenye uwezo si tu kusimamia makao makuu bali nchi nzima. Mtu anayeweza kuleta mabadiliko yenye tija nchi nzima.
 
Kwa jinsi ninavyofahamu, Dr. Rashid angekuwa one of the best CEO kama ambavyo mnasema basi tungeona performance yake pale Tanesco. Uwezo wa mtu unapimwa na performance yake! Kama mnataka kumtetea kwa kusema eti anaingiliwa na bodi ya wakurugenzi, waziri husika, katibu mkuu na baadhi ya wakurugenzi wizara ya nishati na madini basi angejiuzuru mapema na huo ndio weledi duniani kote!!

Professionalism means meticulous adherence to undeviating courtesy, honesty, and responsibility in one's dealings, plus a level of excellence that goes over and above the commercial considerations and legal requirements. Professionalism is not about your job title or self-proclaimed worth. It is not about self-perception at all. Professionalism is about personal ethics, quality work and a quality attitude.

Na kama kuna mazingira ya watu kukushurutisha ufanye jambo ambalo ni kinyume na wewe unavyoamini, you resign!!

Hata kama Rais atakuomba urudi unampa masharti ya kurudi, akishindwa kukutekelezea you quit!!!

He is just another failure, period!!!!

Brooklyn,

Good message, for all people who believe in integrity and principles.However, is the message that all CCM member and so called wapiganaji should take this note as an evaluation sheet!

sadly, most of us we are not of this caliber, our stomach needs are far ahead than our noses!

This is situation that we need to fight with now, this is our chronic unsolved disorder.We were supposed to learn from our forefather like Mkwawa!

Discussing about how Kilango,Mwakyembe are good! make us naked at the end!!!!
 
Nimesema hoja ya Radar na hoja tofauti na sijaona hoja hii imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale TANESCO. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.

Kama huyu ndiyo mmoja wa maCEO bora kabisa katika hayo mashirika basi sishangai kuwa hadi sasa hivi tuko hapa tulipo! Ati kipimo cha ubora ni kuwa hakuharibu! Ebo. Tunataka kuona tofauti katika upatikanaji wa hii bidhaa muhimu. Mimi si Radar wala Richmond iliyonionyesha kuwa huyu jamaa hafai. Kilichonikatisha tamaa ni jinsi alivyoshughulikia suala la Tanga Cement. Ingekuwa vyema angeachiwa kuondoka tumpate mtu ambae angeleta maendeleo na si kuwa mpoza kiti tuu.

Amandla........
 
*Adai ni mtendaji makini, asiyeyumbishwa na wanasiasa
*Apuuza tuhuma zake za rada, ang'ang'ana tena na Dowans

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam


WAKATI kukiwa na hisia ya kuwepo mtandao unaofanya jitihada za kuhakikisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), Dk. Idris Rashidi, anateuliwa tena kushika nafasi hiyo nyeti, Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, ameibuka hadharani kumpigia debe Rashidi katika mazingira yanayoongeza utata kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa mbunge huyo katika siku za karibuni.

Katika hali isiyotarajiwa, Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, amedai kuwa Dk. Rashidi ni mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika ya umma waliopo Tanzania, licha ya tuhuma zinazomwandama na utendaji wake ambao umewakera Watanzania wengi.

Zitto, ambaye alipachikwa jina la "Mr Dowans" na baadhi ya watu mapema mwaka huu baada ya kuchukua mtazamo wa aina yake wa kutetea mpango tata wa Dk. Rashidi wa kutaka kununua mitambo yenye kutu ya Dowans kwa bei kubwa kuliko hata waliyoitumia Richmond kuinunua awali, sasa amejitokeza na kudai kuwa kiongozi huyo ni lulu.

Kauli hiyo ya Zitto aliyoitoa kupitia mtandao wa mijadala wa Jamii, imekuja ikiwa ni baada ya gazeti hili kubainisha kuwa jina la Idris limepenyezwa Ikulu ili ateuliwe kuendelea na wadhifa huo, hali ambayo imesababisha mgawanyiko katika Bodi ya Tanesco ambako baadhi ya wajumbe wameukana uamuzi huo kuwa si wao.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye alisema akirejea nchini atachunguza suala hilo kwani inawezekana hata yeye amerukwa kwa kutofahamishwa mchakato huo. Ngeleja kwa sasa yuko na Rais Jakaya Kikwete, nchini Jamaica na baadaye watakwenda visiwani Trinidad na Tobago.

"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya www.jamiiforums.com.

Zitto amedai kuwa mjadala unaondelea hivi sasa nchini kuhusu hatima ya Rashidi huenda ikawa ni jitihada makusudi za kuzuia asiendelee na nafasi hiyo.

Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto alipingana hadharani na uamuzi wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyo chini ya uenyekiti wa William Shellukindo iliyo kataa mpango wa Rashidi kununua mitambo ya Dowans iliyorithiwa kutoka kwenye kampuni ya Richmond.

Wataalamu wa maswala ya Bunge wanasema kuwa kitendo cha Zitto kuipinga hadharani kamati ya Shellukindo kilikuwa ni uvunjaji wa utaratibu, kwani kamati ya Shellukindo ndiyo yenye mamlaka ya kushughulikia sekta ya nishati nchini.

Kiutaratibu, Mbunge huyo angetakiwa kuiandikia barua kamati ya Shellukindo na kutoa ushauri wake kwenye jambo hilo badala ya yeye kupingana nayo hadharani. Kitendo cha Zitto cha kumtetea Rashidi hadharani kumeleta hisia kuwa huenda ana maslahi binafsi kwenye jambo hilo.

Hata hivyo uteteuzi huo wa Zitto ulipingwa na wachangiaji wengi katika mtandao huo kiasi cha Zitto naye kujibizana nao na wakati fulani mjadala huo ukienda mbali zaidi kwa wachangiaji kurushiana tuhuma nzito.

“Dk. Rashid sidhani kama ni mzuri hivyo kwani kama angekuwa hivyo alivyo hii miaka 3 tungeona kitu fulani. Kwani kwa position (nafasi) yake anaweza kutoa ushauri wa kipi kifanyike na kama hakikufanyika anajua nini cha kufanya. Kama ni kweli is a man of principles (mtu wa kufuata utaratibu) kama baadhi walivyo mnadi.

“Matatizo ya umeme ni yale yale na mpaka leo hii...Hakuna jipya analoweza kufanya nina imani kuna watu competent (wenye uwezo) uswahilini wawatumie tuone. Siyo kukalia historia,” alisema mchangiaji mmoja.

Mwingine akamvaa mbunge huyo: “Zitto nadhani una maslahi katika issues (masuala) za Dk. Rashidi na Dowans vinginevyo usingeshabikia uozo huu eti Rashidi ni mzuri wakati bei ya umeme inapanda kila siku, mgawo mkali, n.k.

“Kwa ufupi ni kwamba Rashidi hana tena uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo. Kinachoonekana pale Tanesco eti inapata faida ni kutokana na kutowalipa IPTL, Aggreko, Dowans ndio maana inaonekana walau wanapata faida lakini kusema kuna improvement (mabadiliko) yoyote pale ni hakuna.”

Mchangiaji mwingine alisisitiza: “Mimi kwa taarifa nilizopata toka wakati ule alipokuwa BoT ni (yaani Dk. Idris alipokuwa Gavana) alikuwa ni mtu Competent (mweledi) sema miaka ya mwanzo, lakini wanasiasa walimuharibu na yeye akakubali kuharibiwa, kwa sasa namuona hafai hata, labda tuseme kwamba wanasiasa wanamhitaji kwa shughuli zao za kifisadi.”

Wachangiaji kadhaa walitaja kuwa kiongozi huyo wa Tanesco pia alipaswa kujiauzlu kupisha uchunguzi wa rushwa unaoendelea dhidi yake hasa katika sakata la rada.

Zitto alipuuza kauli hizo akisema: “Nimesema hili (la rada) ni suala la mahakamani na tushinikize wanaotajwa wapelekwe mahakamani na mahakama ndio pekee zenye mamlaka ya kusafisha mtu au kuhukumu.

“Sijaona hoja hii (ya rada) imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale Tanesco. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.

“Kinachonipa tatizo ni jinsi watu walinvyoline up (jipanga) kuchukua nafasi pale Tanesco ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote,”alisema mbunge huyo na kusisitiza suala hilo bado halijathibitishwa na Mahakama hata hivyo akapingwa vikali kutoka kwa mchangiaji mmoja aliyehoji:

“Hivi Mh Zitto kwenye ile list yenu of shame mliyoitoa pale Mwembe Yanga wale watu walikuwa wameshahukumiwa na mahakama gani? Kama ni mahakama za kisiasa kwa nini watu wengine wakitumia njia hiyo kumhukumu Dk. Idris unaona wanakosea?”


SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009
 
Hi Barubaru,

Walau umsema, na wegine waje tuone. Tuliyoyaona tumeyaona, kwa ubinaadamu ni busara tu kuachia wengine
 
Zitto ampigia debe
Dk. Rashidi Tanesco


*Adai ni mtendaji makini, asiyeyumbishwa na wanasiasa
*Apuuza tuhuma zake za rada, ang'ang'ana tena na Dowans


MWANDISHI WETU
Dar es Salaam


WAKATI kuk...........siasa kwa nini watu wengine wakitumia njia hiyo kumhukumu Dk. Idris unaona wanakosea?”

SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009

Eti Mwandishi wetu Dar!! Unajificha ficha unaogopa nini kuweka jina lako kama una uhakika na unachoandika?
 
Tunapogeuza ufisadi ni mijadala ndio tunapoenda mrama. Mpaka sasa ni tuhuma na mahakama ikimtia hatiani hutaniona ninajenga hoja hizi. Lakini kama kuna ufisadi, au tuhuma za ufisadi akafanya TANESCO toka amekuwa CEO pale ziwekwe hapa na sio kutumia visingizio vya SFO kumhukumu mtu katika court za vijiweni.QUOTE][/COLOR]

Hivi Mh Zitto kwenye ile list yenu of shame mliyoitoa pale Mwembe Yanga wale watu walikuwa wameshahukumiwa na mahakama gani? Kama ni mahakama za kisiasa kawa nini watu wengine wakitumia njia hiyo kumhukumu Dr Idris unaona wanakosea? Halafu katika ripoti ya EPA ya auditors ambayo iko JF wakaguzi wanasema kwamba waliona barua ya Ruth Mollel kwa Gavana wa Benki ya mwaka 1997 (wakati huo akiwa Idris) ikitaka kujua status ya EPA ambayo haikujibiwa. Kitu kingine ni CIS ambayo pia inafanana na EPA ambayo ilitokea Dr Idris akiwa gavana na hiyo utakuwa unafahamu maana zaidi kuliko mimi maana nadhani kuna kamati iliundwa kuchunguza. Pia Idris alivyoondoka BoT alikwenda Akiba ambako hakukaa akaenda Vodacom ambako alishushwa cheo kutoka CEO mpaka Marketing Manager, wewe unatuambia kuwa the guy is the best CEO.

Inawezekana unatumia vigezo vingine na sisi, lakini kipimo cha utendaji siyo faidia tu ndugu Zitto, na inabidi uwe makini sana kwani faida inaweza kutengenezwa kwa kupunguza matumizi ambayo pengine yangekuwa muhimu katika utoaji huduma. Hivyo basi kipimo kingine zaidi ya vipimo vya fedha ungeangalia kama kiwango cha huduma na ubora wa huduma.

Ukiangalia utaoji huduma ya umeme hali imekuwa ile na bila ubora kuongezeka. Na kibaya tunapata mgao hata msimu wa mvua tofauti na zamani ambapo tulipata wakati wa kiangazi tu. Muheshimiwa Zitto unaweza kuwa unamwona jamaa ni mzuri na hata ukiongea naye unamwelewa lakini ni kwamba ukiangalia utoaji huduma jamaa hajaweza kufanya kile kitu ambacho ungetaka watu tuamini utetezi wako.
embu muulize zitto alivyomshambulia Karamagi alikuwa amuhukumiwa na mahakama gani
 
Eti Mwandishi wetu Dar!! Unajificha ficha unaogopa nini kuweka jina lako kama una uhakika na unachoandika?

Cynic

Ndugu yangu hawa waandishi ushwara utawaweza? kila kukicha Zitto, Zitto,
 
Hii imechukuliwa kama ilivyo humu humu JF! Zitto anawaweka mjini waandishi wa habari!

Zitto kaa kimya mkuu,this is now too much, umeshakuwa robot sasa, ukisema kitu kama wewe tatizo!
 
Ni kweli Tanzania kuna waandishi wengi uchwara kama Cynic na IsayaMwita wanavyo sema. Lakini ukiisoma kwa makini hii habari ya gazeti la Kulikoni ime "capture" mjadala unaoendelea kwenye jamiiforums kuhusu Dk. Rashidi kama maoni yalivyotolewa na wachangiaji wenyewe, ikiwemo Zitto
 
Mwandishi ameishiwa. hana maana.

Jamani lazima tukumbuke Zitto ni mtanzania kama wananchi wengine. na vile vile tunatakiwa tujuwe Zitto hayupo juu ya sheria za nchi. Yeye anao uhuru wa kutoa maazo yake kama mtanzania yoyote ili mradi tu asivunje sheria za nchi.

Kwa hakika hata mimi na kwa ninavyomfahamu Dr Idriss siwezi amini kabisa kama aneeza fanya mabaya dhidi ya Tanesco. Hata vyombo vyenu vya habari vya huko vimesema wazi kuwa Dr anapendwa sana na wafanyakazi wa chini na anachukiwa na mameneja. Sababu kuu ni kuwapunguzia posho zao walizojiwekea na kuwalipa wafanyakazi wa kawaida.

nakuunga mkono Zitto kwa kuona wazi juhudi na kazi zote na maamuzi sahihi ya Dr Idrissa.

Tuache siasa kwenye kitu cha kitaalamu.
 
habari zingine huwa hazina kichwa wala miguu ..unaweza kusema ndio wao wakageuza hapana ni vichwa vyao vya habari ambavyo huwa havieleweki
 
Kwanza binafsi ZITO AMEKUA mtata sana kwenye sakata hili lote la umeme Tanzania, kujitokeza kwake hadharani mara kwa mara ni kielelezo cha namna anavyotetea kile anachokiamini ama anachodhani ni sahihi, ama kwa kudanganywa ama kwa utafiti wa kina wa sakata hili lote. yeye amekua akitoa hisia zake bila hofu yoyote....hii ninzuri.

Kuhusu mwandishi anaeficha identity yake kwenye swala ambalo limejadiliwa hadharani humu Jamvini ni upuuzi, ninahisi kua amewadanganya mabosi wake kua amefanya uchunguzi wa sakata hilo kisha akangundua mambo hayo, wakati reality ni kua zito alikua live humu jamvini akijieleza juu ya kwanini anaamini Dr Rashidi ni mtendaji mzuri na sio mtu wa hovyo-hovyo kama watu wengi wanavyodhani.


Mimi naamini Dr Rashid ni kiongozi wa hovyo kabisa, natatizwa hata na elimu yake, ingawa kuna mtu amenithibitishia hapa kua ,ni msomi wa aina yake mwenye kichwa makini na mjuzi aliepevuka katika mambo ya kitaaluma....

Sasa kwa kushindwa kwake inaonekana alikariri darasani ama alifanya kusudi ili apate kamuhogo kake. mambo haya.
 
Wakuu,
Hapa JF sasa panazidi kuonyesha jinsi watu walivyokomaa. Mjadala huu pamoja na ule uliosababisha kuitwa Kubenea juzi juzi kujitetea kuhusu ripoti iliyoandikwa kwenye MwanaHalisi zinatikiwa zitunzwe kwenye safe custody for future reference.

Kwa mtazamo wangu, hapa JF tumegawanyika makundi manne kama ifuatavyo:
1. Wapo ambao wanatafuta ukweli na usahihi wa mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi yetu. Wazalendo wa kweli ambao wanauchungu na nchi yetu.
2. Wapo wanaowakilisha watu, serikali, vyama vya siasa na magazeti haswa ya watu binafsi.
3. Wapo waliopo hapa kwa ajili ya kutangaza na kutetea dini na kabila zao
4. Wapo ambao "they would like to remain neutral" but will not accept been cheated, are educated and would not expect someone to use the forum as a place for fooling others.

Baada ya kusema hayo ninashauri kuwa kwenye kuchangia mambo sensitive kama hili, nawashauri wenye agenda za siri waache kabisa kuchonga vinyago bila mpingo! Nawashauri kwamba pale wanapoona "there exists a conflict of interest they should better allow the constructive debate/s to continue".

Naomba tuliangalie hili kwa makini zaidi!
 
Zitto ampigia debe
Dk. Rashidi Tanesco


*Adai ni mtendaji makini, asiyeyumbishwa na wanasiasa
*Apuuza tuhuma zake za rada, ang'ang'ana tena na Dowans


MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WAKATI kukiwa na hisia ya kuwepo mtandao unaofanya jitihada za kuhakikisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), Dk. Idris Rashidi, anateuliwa tena kushika nafasi hiyo nyeti, Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, ameibuka hadharani kumpigia debe Rashidi katika mazingira yanayoongeza utata kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa mbunge huyo katika siku za karibuni.

Katika hali isiyotarajiwa, Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, amedai kuwa Dk. Rashidi ni mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika ya umma waliopo Tanzania, licha ya tuhuma zinazomwandama na utendaji wake ambao umewakera Watanzania wengi.

Zitto, ambaye alipachikwa jina la "Mr Dowans" na baadhi ya watu mapema mwaka huu baada ya kuchukua mtazamo wa aina yake wa kutetea mpango tata wa Dk. Rashidi wa kutaka kununua mitambo yenye kutu ya Dowans kwa bei kubwa kuliko hata waliyoitumia Richmond kuinunua awali, sasa amejitokeza na kudai kuwa kiongozi huyo ni lulu.

Kauli hiyo ya Zitto aliyoitoa kupitia mtandao wa mijadala wa Jamii, imekuja ikiwa ni baada ya gazeti hili kubainisha kuwa jina la Idris limepenyezwa Ikulu ili ateuliwe kuendelea na wadhifa huo, hali ambayo imesababisha mgawanyiko katika Bodi ya Tanesco ambako baadhi ya wajumbe wameukana uamuzi huo kuwa si wao.

................................................
SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009


ina maana KULIKONI hawana jina la MWAANDISHI ? wanaogopa nini?


oili inamaaan hawa kulikoni hawawezi kuandika JAMIIFORUMS.COM


its about tgime wan JF mkahit back on these people
 
ina maana KULIKONI hawana jina la MWAANDISHI ? wanaogopa nini?


oili inamaaan hawa kulikoni hawawezi kuandika JAMIIFORUMS.COM


its about tgime wan JF mkahit back on these people
wanaogopa visivyoogopesha, wanawadanganya waajili wao kua wanafanya uchunguzi wakina kumbe tunashinda nao humu jamvini
 
Back
Top Bottom