Dr Rashid ninayemfahamu
Kwa bahati nzuri nimeshiriki katika kazi maalum ya pale TANESCO wakati wa kipindi cha NET Group na baada kuingia kwa Dr Rashid pia. Watanzania tuache uchafuzi wa CVs za watu pasipo kuwa na uhakika. Kuna mabadiliko makubwa sana ambayo Rashid ameyafanya ndani ya TANESCO, ambayo ni mazuri na makubwa. Rashid alikabidhiwa mkoba wa lile shirika ukiwa na pumzi inayokaribia kufa. Jambo la kwanza la kuangalia, tazama hati za ukaguzi wa mahesabu za sasa zinazofanywa na kampuni moja ya kimataifa, (Audited financial statements) ambayo imekuwa ikikagua kampuni hiyo tangu wakati wa NETI Group. Utaona kuna mabadiliko makubwa sana. Kutoka Adverse opinions/Disclaimer opinions hadi sasa utaona atleast Qualified opinions. Ukweli ni kwamba Dr Rashid ni kati ya ma CEO makini na wazuri katika nchi hii. Ndiyo, upende usipende, pamoja na kelele nyingi na mapungufu yanayoweza kujitokeza, bado Dr Rashid ni CEO makini. Kwa wanao ongea kwa kutazama maandishi ya kwenye magazeti tu, hawawezi kuelewa!.
Siasa zinapokuwa zimeingia katika professionalism ndipo tunaona kupakwa kwa kinyesi kwa Dr Rashid. Tatizo letu wa TZ mambo ambayo yanahitaji wataalamu tunayawekea kimbelembele cha siasa, hata pasipohitajika!. Tangu tuhuma za Rashid zianze siyo leo, lakini kila siku ni tuhuma tuhuma tuhuma tu!. Hata wasiokuwa na data, ni tuhuma tu.
Jambo la pili, tazama hata maendeleo ya baadhi ya makampuni ambayo Dr Rashid anayasimamia kama Mwenyekiti wa Bodi, kwa mfano benki ya Akiba, tazama miaka miwili ambayo huyu mzee wetu Rashid ameingia kwenye board na kupewa uenyekeiti wa bodi, amefanya mabadiliko makubwa na tunaona benki hii ni kati ya benki ambazo zinakua na kufanya mabadiliko makubwa katika technolojia na utendaji pia, hapa nchini.
Tatizo letu wa TZ tunachonga sana hata pasipokuwa na data za kutosha kuendeleza mchongo!! Utakuta mwandishi wa habari au M- TZ mwenzangu, yeye pekee ni prosecutor, yeye huyo ni Forensic expert, yeye ni Auditor, yeye ni Engineer, yeye Mhasibu nk, huu ni mtazamo hasi. Lazima tufike mahali tuwe tunachonga kwa data, pale panapohitajika, si kuchonga tu!. Tunawasaidia wafanyabiashara kuuza magazeti bure!!. hali wengine wakisubiri pesa za wananchi zitumike kuwanyamazisha kuendeleza uandishi wa habari usiokuwa na tija na uliojaa udaku udaku tu!. Magazeti mengi yanajifanya yanaandika habari za uchunguzi, lakini ukisoma utaona ni UDAKU TU!. Soma hata habari hii ya Thisday, hapo juu; kwa umakini, utaona hakuna investigative journalism inayoonekana katika makala hiyo, zaidi ya kujaa udaku udaku tu!; See this "According to these sources, the TANESCO board of directors chaired by Peter Ngumbulu has already formally recommended the re-appointment of Rashidi - but under controversial circumstances............Ngumbulu was yesterday not available for comment on the implication of a split amongst TANESCO board members (directors) over the Rashidi issue, while acting board chairman Adolar Mapunda flatly declined to comment". Sasa kama hawa Thisday walikuwa wamemkosa Ngumbulu, walikuwa na haraka gani ya kuileta hii habari gazetini, kabla ya kupata uhakika wa taarifa hizi. Hata habari yenyewe haielezi, what are the contravential circumncistances.... Huu ni ubabaishaji katika uandishi wa habari. Hebu angalia, Sources za habari hawajatueleza, hata hizo contravential circumncistances hawajaeleza. Maana yake ni kwamba, sources na taarifa zenyewe wanazotaka kutuhabarisha hawazijui. Isipokuwa wanataka kuuza gazeti tu!
Ninachokiona na ambacho waandishi wengi wa habari wanakosa, ni "Report Writing Skills". Pia ninadhani, wahariri wengi, hawana uwezo mzuri wa kukaachini na kuhariri habari vyema. Pia waandishi wa habari waelewe kwamba kuwa mwandishi mzuri wa habari kunahitaji kuwa na skills zaidi ya taaluma ya uandishi wa habari. Wajitahidi waongeze taaluma, mbalimbali ambazo zitawafanya wawe wanaelewa namna shughuli zinavyofanywa katika makampuni na mashirika. Si ajabu kumkuta mwandishi wa habari aliye andika habari hii katika Thisday, hajui hata Corporate Governance, hajui hata namna masuala mbalimbali yanavyosimamiwa na kutekelezwa katika mashirika na makampuni. Yeye alivyoambiwa Ngumbulu hayupo, basi, akaona ndiyo mwisho wa fikira! Akakimbia kwenda kwenye mtambo kupeleka habari eti Habari hizi nilizoziandika ngumbulu hakupatikana kuthibitisha!!. Hata asijue kwamba suala kama hili ni sensitive, linalohitaji umakini katika kulitolea taarifa kwa maslahi ya taifa. Tatizo wanatoa taarifa kama WANAVYOPEANA TAARIFA ZA MISIBA!!.
Nadhani Thisday nao wamepoteza mwelekeo!! They are more of Majungu, kuliko investigative journalism wanayoiimba kila kukicha!
"For actions speaks louder than words, let us embrace actions more than words!!!!!"