TANESCO board split on MD Rashidi's fate

TANESCO board split on MD Rashidi's fate

Kauli hiyo ya Zitto aliyoitoa kupitia mtandao wa mijadala wa Jamii, imekuja ikiwa ni baada ya gazeti hili kubainisha kuwa jina la Idris limepenyezwa Ikulu ili ateuliwe kuendelea na wadhifa huo, hali ambayo imesababisha mgawanyiko katika Bodi ya Tanesco ambako baadhi ya wajumbe wameukana uamuzi huo kuwa si wao.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye alisema akirejea nchini atachunguza suala hilo kwani inawezekana hata yeye amerukwa kwa kutofahamishwa mchakato huo. Ngeleja kwa sasa yuko na Rais Jakaya Kikwete, nchini Jamaica na baadaye watakwenda visiwani Trinidad na Tobago.

"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya www.jamiiforums.com.

Kwa vile mimi ndiyo niliweka post hii, naomba kuwajulisha kuwa kwenye habari hiyo ya Kulikoni kuna attribution kuwa mjadala huo wa Dk. Rashidi uko kwenye JF. Nadhani pia kwa wanaosoma Kulikoni kila mara wanafahamu kuwa gazeti hilo mara nyingi hawaweki majina ya waandishi wao hadharani
 
sawa.
 
Eti Mwandishi wetu Dar!! Unajificha ficha unaogopa nini kuweka jina lako kama una uhakika na unachoandika?

Duuh taaaabu kweli kweli hapo, waandishi wa habari ni kupenda kutupotezea muda na pesa kununua magazeti na kusoma news zao zisizo na kichwa wala minguu, I think waandishai wa habari nao wapaswa kujua alama za nyakati na kuwa more creative kwa ku deliver news to the community.

Most of the time utakuta magazeti yamejaaaa habari za wanasiasa na siasa zisizo jenga na kudumisha maendeleo ya nchi.

Mwandishi ameishiwa. hana maana.

Jamani lazima tukumbuke Zitto ni mtanzania kama wananchi wengine. na vile vile tunatakiwa tujuwe Zitto hayupo juu ya sheria za nchi. Yeye anao uhuru wa kutoa maazo yake kama mtanzania yoyote ili mradi tu asivunje sheria za nchi.

Kwa hakika hata mimi na kwa ninavyomfahamu Dr Idriss siwezi amini kabisa kama aneeza fanya mabaya dhidi ya Tanesco. Hata vyombo vyenu vya habari vya huko vimesema wazi kuwa Dr anapendwa sana na wafanyakazi wa chini na anachukiwa na mameneja. Sababu kuu ni kuwapunguzia posho zao walizojiwekea na kuwalipa wafanyakazi wa kawaida.

nakuunga mkono Zitto kwa kuona wazi juhudi na kazi zote na maamuzi sahihi ya Dr Idrissa.

Tuache siasa kwenye kitu cha kitaalamu.

Nashangaa mawazo ya Zitto ni kama ya rais vile akisema kitu basi kinakuwa,....this sense of inferiority imetuweka wazi sana watanzania tulivyo. vita ya maneno na mawazo mapya watu waoga hivi ndio maana hata EAC hatutaki!

sad and shame.
 
Kwa vile mimi ndiyo niliweka post hii, naomba kuwajulisha kuwa kwenye habari hiyo ya Kulikoni kuna attribution kuwa mjadala huo wa Dk. Rashidi uko kwenye JF. Nadhani pia kwa wanaosoma Kulikoni kila mara wanafahamu kuwa gazeti hilo mara nyingi hawaweki majina ya waandishi wao hadharani

kwa hiyo huwa wanaandika habari wasizokuwa na uhakika nazo so wanaogopa kukutana face to face na wanaowaandika au inakuwaje?
 
ina maana KULIKONI hawana jina la MWAANDISHI ? wanaogopa nini?

oili inamaaan hawa kulikoni hawawezi kuandika JAMIIFORUMS.COM

its about tgime wan JF mkahit back on these people

Zitto ampigia debe
Dk. Rashidi Tanesco

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya www.jamiiforums.com.

SOURCE: KULIKONI, Novemba 27, 2009

Mkuu GT, wameandika. Naona hukusoma yote na ukaanza kurusha makombora.
 
Mie nadhani njia nzuri ni kujipongeza wanaJF kwa kuwa newsmaker, kwa ujumla tanzania hakuna waandishi wachokonoaji na watafutaji habari wanasubiria JF tunajadili nini na wao wapate njia

Bravo JF
 
Kwani CEO wa TANESCO anachaguliwa kwa kura?? Si walitangaza hiyo nafasi kwa nini wasitumie vigezo kuchagua, hata hivyo mna uhakika kama Dr. Rashid aliomba hiyo nafasi tena?
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto
 
Zito, umeanza lini kua muoga kwenye mambo yanayogusa maslahi ya taifa, katika mchakato wakuutetea ukweli wako mashujaa walio kufa na kutengwa na jamii zao, lakini baadae ukweli ulipodhihiri waliibuka kua mashujaa wakubwa sana, sasa nakutakia kila la heri katika harakati zako.
ila sikubaliani nawe katika hilo la Dr Rashid...huyu ameitumbukiza nnchi kwenye matatizo makubwa, ipo siku tunachapa fimbo hata kaburi lake.
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto
Walishindwa nini kukutafuta wewe binafsi badala ya kudokoa maoni yako hapa?

Lakini sishangai sana, kwani kwenye network zingine watu wamepoteza kazi zao baada ya waajili wao kuona nini wanaandika humo. Hivi karibu katika FB mdada mmoja wa Canada amekatwa mafao yake ya likizo ya ugonjwa baada ya kubandika picha zake zikionesha akiparty kwa vujo.
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto

Ipi tuambie tupime jamani, kwani sisi pia ni binadamu tunaweza ku reason mambo!
Kumbuka kuna siku uliwaambia watu wawe na ngozi ngumu humu ndani ya JF. please nami nakutafadhalisha leo zito hebu kuwa na ngozi ngumu usizire kuandika ukabaki kuwa msomaji ilihali tuna/ninahitaji mchango wako katika ujenzi wa taifa hili CHANGA

We do not see things as they are: we see things as we are
 
Mjadala huu umeonesha huku JF kuna wababaishaji kadhaa na wengi wanaohitaji kupisha mijadala wasioyoijua vyema. Mosi, KULIKONI limeatribute vizuri tu kwani naambiwa hata taaluma ya habari inasema gazeti likinukuu gazeti jingine au chombo kingine cha habari ni vyema likatajwa linalotumika kama chanzo na hii ni kawaida kitaaluma.

Hao jamaa wa KULIKONI ni wapambanaji kama sisi JF (labda leo tujitangaze kuwa si wapambanaji) na mambo mengi waliyoyaibua ndio tumeyajadili sisi hapa na pale nasi tulipoibua jambo nao wamekuwa wakiyasimamia. Hata hili la Rashid walilianza wao na THISDAY ndipo likaja kujadiliwa hapa.

Zitto huna haja ya kutoka JF, ulichangia mjadala kwa kuonekana ukitumia vyeo vyako vyote vya ubunge na kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ndio maana baadhi ya takwimu ulizitoa katika kumtetea Dk Idris zilitokana na hesabu zilizowasilishwa katika Kamati yako.

Hili pia ni fundisho kwako na nakumbuka uliwahi kushauriwa na mwanaJF mmoja kuhusu misimamo unayojiamini kuwa nayo kuwa wakati fulani inahitaji kupitiwa kwa makini.Labda ungekuwa na wataalamu wa mawasiluiano ya umma kwa karibu wangekusaidia nini cha kusema wapi na wakati gani.Lakini ukiacha hilo gazeti msimamo wako wa jana uliwashangaza wanaJF wengi.

Mara kadhaa ulitetea wazi humu kuwa Dk. Idris ni makini na mtawala mweledi, sasa unaogopa vipi kivuli chako jamaa walipoandika ulichokisema hasa kwa kuzingatia ulikotoka na misimamo yako ya nyuma ukiwa mpinga mafisadi, leo mafisadi unawaona most competent?
 
Siasa...........! tungeacha mashirika yakawa na bodi huru na kuziwekea malengo na kuzipima kutokana na malengo mashirika haya yangeenda vizuri sana. Siasa zinaingia sana na huyu Rashidi ni mmoja wa CEOs anayewakatalia wanasiasa waziwazi. Wanamchukia sana. Mfano kawaambia Wizara walipe pango la jengo la TANESCO, wizara eti hawataki..... CCM nao wameng'ang'ania Rest House ya TANESCO dodoma, amewatimua. Wamekasirika. Basi ni matatizo tu..... Sasa kwenye kampeni wanataka waweke CEO goigoi awape pesa maana Rashidi hatakubali na wao wameshazoea.....

Nakubaliana nawe kuhusu tatizo la siasa kuharibu mambo kwani hata wewe hapa naona unapiga siasa zile zile unazozishutumu. Hivi huo uzuri wa Dr. ni upi, kuendelea na mbinu ile ile ya kuongeza mapato ya TANESCO kwa kutubambikiza bili!

Hapana, Zitto nakuona umebadilika, au sikuwa nakuelewa vizuri, Dr Indrisa hajatuonyesha Watanzania uwezo wake kwani hatuoni mabadiliko yoyote pale TANESCO, mabadiliko ya hiyo nishati kwenye jamii.

Madai yanayotolewa kwamba anapendwa na wafanyakazi wa chini inategemea umeongea na nani, aliyenufaika na mfumo wake wa uongozi au aliyeumizwa, kwani wapo wafanyakazi tena hao hao wa chini, hususani mikoani, wanaomuelezea kuwa naye ni mwanasiasa tu, anafuata upepo wake wa kisiasa unavumia wapi.

Kwa ufupi wapo Watanzania wengi tu wenye uwezo wakipewa nafasi na mazingira mazuri, hakuna haja ya kumng'ang'ania aendelee kutupandishia bei ya umeme, tunahitaji mabadiliko kwenye shirika na kwa kuanzia ni hiyo nafasi ya CEO
 
Zito kisha kapoteza mwelekeo siku nyingi ninyi hamjui tu. kisha nunuliwa, hana kauli yake tena. Msimamo wote umeyeyuka.
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto

shujaa hakimbii vita bwana zitto
we endelea na sakata la la uchangiaji na ufafanuzi kama kawaida
 
Zito kisha kapoteza mwelekeo siku nyingi ninyi hamjui tu. kisha nunuliwa, hana kauli yake tena. Msimamo wote umeyeyuka.

kanunuliwa na nani
Rwechu unajua kuna wakati mambo mengine unaweza kujibu na wakati mwingine unaamua usijibu huwa ni msimamo tu
Ukweli na uwazi wake huwa anauongea hapa hapa JF so hilo la kununuliwa mie sina uhakika nalo
 
Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.

Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.

Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.

Zitto

Tumeshindwa kukutumia mh., pia hakuna anayejali unaathirika vipi kisaikolojia kwa haya maneno. Mimi nakubaliana na wewe after all tuna wabunge wengi sana kama 300 hawaonekani humu, tunayekuona tunakupiga mawe humu humu na watu wanalisha watoto wao kwa kuuza magazeti,watu wanasema bila vithibitisho.Hakuna anayejiweka nafsi yako aone unajisikia vipi.Yet tunalilia mabadiliko wakati wapiganaji tunawapiga kabali

Hii dhambi na tabia hii imerudisha nyuma wengi, siasa kwa vijana Tz ni ndoto, watu watabaki kuwa wenyeviti wa kipaimara na harusi za ijumaa na jumamosi kwisha!

Inaboa sana, wazo lako zuri litakusaidia mkuu! tunakujali mkuu!
 
Huyu jamaa kisha poteza mwelekeo, kishakula hela za watu hana tena uhuru wa kusema mambo yake. Misimamo yote kwisha.
 
Back
Top Bottom