Jamani, KULIKONI kama yalivyo magazeti mengine hapa Tanzania lina mapungufu yake. Lakini pia lina mema yake. Lazima tuseme ukweli kuwa kwenye hii habari yao wamemnukuu Zitto extensively. Nimehesabu sasa hivi gazeti hilo limetoa zaidi ya paragraph 6 kueleza "hoja" kama sio "Vioja" vilivyojengwa na Zitto kumtetea (kumbeba) Rashidi. Zifuatazo ni direct quotes kutoka kwa Zitto zilizo andikwa na gazeti hilo...
"Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals (mmoja wa viongozi bora zaidi wa mashirika yetu ya Umma)," amesema mbunge huyo machachari kwenye mjadala mkali unaoendelea kuhusu sakata la Rashidi kupitia kwenye tovuti ya
www.jamiiforums.com.
Zitto alipuuza kauli hizo akisema:
"Nimesema hili (la rada) ni suala la mahakamani na tushinikize wanaotajwa wapelekwe mahakamani na mahakama ndio pekee zenye mamlaka ya kusafisha mtu au kuhukumu.
"Sijaona hoja hii (ya rada) imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale Tanesco. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami,
Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.
"Kinachonipa tatizo ni jinsi watu walinvyoline up (jipanga) kuchukua nafasi pale Tanesco ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote,"alisema mbunge huyo na kusisitiza suala hilo bado halijathibitishwa na Mahakama