Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Trust me, kiingereza ulichotumia ni kibovu. I am not kidding. Kibovu.
Value ya nyumba haipangwi na accountants. Kuna watu wanaitwa valuers.
Kama ulivyoambiwa, hiyo depreciation uliyotumia ni kubwa mno. Value inajumlusha thamani ya kiwanja kwa hiyo hata hiyo nyumba ikiingua haiwezi kushuka kiasi hicho.
Bei waliojiuzia wafanyakazi wa umma haihusiani na value ya nyumba. Hata wenyewe hawakudai hilo. Ile ilikuwa ni bei waliyopanga bila kujali true value ya nyumba.
Amandla......
Mkuu Fundi, umejaribu lakini si kila ng'ombe anaepelekwa mtoni atakunywa maji - huyu bwana angeamua kutumia kiswahili kitupu labda angeweza kueleweka. Hata hivyo mimi nitamsaidia kidogo tu kwa swali lake moja la ukarabati wa nyumba za TANESCO.
Nyumba inayodaiwa alijiuzia kwa sh 80,000,000/- ni hiyo iliyokarabatiwa kwa sh. 650,000,000/- ! Haya madai yalitolewa na Mh. Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), aliyeibua ufisadi mwingine wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba wamekarabati nyumba saba zilizokuwa zikikaliwa na wakurugenzi wa shirika hilo kwa sh bilioni 1.4 !Kuna ukarabati wa nyumba za TANESCO ulifanyika, nyumba ya kwanza ilikuwa namba 13 iliyopo Mtaa wa Toure- Chaza, Oysterbay ambao ukarabati wake uligharimu zaidi ya sh milioni 600. "Nyingine ni namba 89 ipo Mtaa wa Gine Road ambayo ukarabati wake uligharimu sh 250,463,140, nyingine ni nyumba namba 65, iliyopo Mtaa wa Laibon Road ambayo imegharimu sh 190,407,430 na nyingine ambayo ni namba 459 ipo Mtaa wa Mawenzi Road ambayo imegharimu sh milioni 130.
Nyumba nyingine iliyokarabatiwa ni namba 93 iliyopo Mtaa wa Gine Road ambayo imegharimu sh 88,515,820, nyingine namba 315 iliyopo Mtaa wa Toure Drive ambayo ukarabati wake umegharimu sh milioni 79, huku nyumba namba 98 iliyopo Mtaa wa Uganda Line, ikiwa imekarabatiwa kwa sh 73,600,000.