TANESCO board split on MD Rashidi's fate


Mkuu Fundi, umejaribu lakini si kila ng'ombe anaepelekwa mtoni atakunywa maji - huyu bwana angeamua kutumia kiswahili kitupu labda angeweza kueleweka. Hata hivyo mimi nitamsaidia kidogo tu kwa swali lake moja la ukarabati wa nyumba za TANESCO.
Nyumba inayodaiwa alijiuzia kwa sh 80,000,000/- ni hiyo iliyokarabatiwa kwa sh. 650,000,000/- ! Haya madai yalitolewa na Mh. Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), aliyeibua ufisadi mwingine wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwamba wamekarabati nyumba saba zilizokuwa zikikaliwa na wakurugenzi wa shirika hilo kwa sh bilioni 1.4 !
 


I appreciate you opinion and i am grateful to your comment but let us go back to the main issue.

In regards to land valuation, valuers they estimated the value of the land but assets of company are kept by accountants. Going back to the main topic what was the value of the house of Tanesco MD (Idrissa).

Second when you say the cost of repairments mounted to 650 was it a single house, milion of tanesco house, gazillion of tanesco houses or just a figure someone woke up with after having an argument with his wife or her husband!!!!
 
 
Hiyo ya mtaa wa Toure, Oyster Bay ndiyo inayodaiwa amejiuzia au alikuwa mbioni kujiuzia.

Amandla........
 
Angalieni watanzania jamani unaona Mbunge alilipua ufisadi wa nyumba. Mag3 umejaribu kutupa details za ukarabati those are the facts even though sijui source yake but umejitahidi ndugu yangu safi sana utupage na source basi kama alivyofanya Mh Zitto.

Kuhusu ulipuaji wa ufisadi i can understand the role of whistleblowers but i do not buy their story kwasababu wengine huwaga wanatheir secret agenda behind. Atuambie huyo muheshimiwa amepata wapi hizo habari? na katika hiyo tenda ilikuwaje?

Kama ilikuwa ni kweli je serikali imechunguzaje hatua gani zilizochukuliwa na wahusika wamechukuliwa hatua gani??
 
Kiswahili au Kiingereza to me is irrelevant and non-sense lamsingi tujadilini hoja hata maprofessa ulaya huwaga kiiingereza kinawapa shida utamsikia professa anaandika neno kispaniola badala ya kiingereza au anatamka doncument instead of document. Tujadilini contents badala context.

Tuje katika mbunge alisema alitaka kununua nyumba milioni 80 je mmejiuliza mbunge yupo ana vielelezo gani afadhali Dk. Wetu wa chadema jina lishalisahau alipofumua ufisadi wa EPA alikuwa na evidence haya huyo mbunge wetu alikuwa na evidence??? Na kama yes serikali ilichukua hatua gani? isijekuwa ni just a smear campaign ya kumtoa Dr idrissa Tanesco???
 
Not to sound like Jonh Edwards, lakini Tanzania ni nchi mbili kati ya moja.

Wakati wabenz wa Toure Drive wanatumia more than half a mill dollars kukarabati nyumba moja, kuna watu wanasomea chini ya miti, wengine hawana madawati hapa hapa Dar.

I am not even going to get into the nitty gritty but this is simply wrong.

I mean one can argue that Oysterbay this and valuation that and ante it up to milioni 70-80 kwa ukarabati (unapata kibanda kizuri tu katika ukarabati huu)

Lakini milioni 650 jamani? Nyumba yenyewe ile ya pale karibu na kwa balozi wa Finland Toure Drive? ina swimming pool ya maji ya dhahabu au nini? Maana tuambiane ukweli.

Kama nyumba ina thamani ya dola milioni 2-3 hata ukitumia 10% ya value ya nyumba bado unakuja kwenye $ 200, 000 - 300, 000. A far cry from milioni 650.

Milioni 650 tunakarabati nyumba mpya ya Waziri Mkuu Pinda? maana najua Mawaziri wakuu na marais ndio wanakaa kwenye vijiji vyenye nyumba kadhaa ambavyo ukarabati wake unaweza fairly kuingia katika hizo figures.

Milioni 650 hata Northeastern US unanunua nyumba nzuri tu. hii si hela ya kukarabati nyumba moja Dar. hii ni hela ya kujenga nyumba burudani sana, ukizingatia ukarabati haujihusishi na ununuzi wa kiwanja.

Jamani hizi milioni 650 zimeendaje endaje?

Mi nikafikiri milioni 650 ndio mkupuo wa ukarabati wa nyumba zote, pamoja na hizo za Uganda Ave, Guinea Ave etc. tena hizi nyumba za Uganda na Guinea ni simple tu nazijua zote. Nimeingia mpaka ndani Guinea pale next to ofisi ya Msajili wa majumba Oysterbay. Uganda Ave kwa yule mzee wa kiarabu/ mpemba wa Tanesco nyumba ukarabati wa mamilioni yote hayo?

Hiyo milioni 650 ingetosha kufanya ukarabati wa nyumba zote, labda hapo ningesema "this is Oysterbay, wakubwa wana tastes zao, vifaa vya ujenzi na ukarabati vimepanda bei what do you expect" lakini hizi habari za nyumba moja ukarabati milioni 650!

I am very familiar with all these houses, kuanzia alipokuwa anakaa Mzee Mosha pale Toure karibu na nyumbani kwa balozi wa Japan mpaka hii nyumba ya Tanesco iliyo karibu na balozi wa Finland, huku karibu na kwa Nyalali kwa zamani, hakuna nyumba ya ukarabati wa shilingi milioni 650. Mi namjua mzee mmoja private investor yuko Oysterbay, ana nyumba ina kiwanja kikubwa mara nne ya hiki cha nyumba ya Idris, nyumba yake ni kama sawa na hiyo ya Idris, anapiga hesabu ya kuikarabati kwa US $ 70,000!

Kwa maana hiyo hata hizo nyumba za Uganda Ave na Guine Road, ambazo ni ndogo kulinganisha hii ya huyu mzee private investor zingeweza kufanyiwa ukarabati mzuri tu kwa shilingi milioni 40, pengine hata na hela kubaki.

Ni kama vile hawa wazee wamekaa wakaona wanastaafu na Net Group wanakuja kuchukua TANESCO kwa hiyo tuchukue mihela kwa kisingizio cha ukarabati halafu tuone nani atasema.

Hawajui hata "kula na kipofu"!
 

Mdondoaji, haya madai yalitolewa bungeni - je unajua yanayomkuta mbunge ambaye anatoa madai yasiyo na ukweli bungeni ? Sasa kama inatokea kuwa hukubaliani au huamini ni juu yako kukanusha (yaonekana unamtetea Dr. kama vile unajua zaidi !) Sana kwa kuwa wewe ni mdondoaji, nakuomba udondoe utupe yaliyojiri baada ya haya madai kutolewa, TANESCO, Bunge au Serikali zilisemaje na hatua zipi zilichukuliwa. Usiwe mtu wa kupikiwa, kuwekewa mezani na bado ukasubiri kutafuniwa.
 

Hilo ni kweli kaka na ndio tatizo la mashirika yetu ya umma na Tanzania kwa ujumla kila mtu anataka kula hapo hapo matokeo bei za ukarabati zinakuwa highly inflated. Na bosi hawezi kusema no but i do not think that is only in Tanesco mbona BOT twin towers zimegharimu gharama za kutoa majengo kumi ya PPF towers!!!!
 

Mie sie niliyesema Dr Idrissa hafai bali nachotaka mtupe facts za kwanini hafai unapodai jambo mbele za watu usimame na vithibitisho thabiti na sio pumba na allegation zisizokuwa na vithibitisho. Wewe umetupa gharama za ujenzi hujatupa source umezitoa wapi? Pili unadai mbunge alilipuka kuwa Dr Idrissa anataka kujiuzia nyumba bunge likaunda tume je tume imekuja na matokeo gani?

Na Bunge si mahakama mzee pale ni mahali pa kutunga sheria sio kwa pilato ukisema uongo au kuzua unaenda jela. Kuna madudu mangapi yaliyokuwa yamejaa waliyatamka Bungeni. Umesahau lilipoanza dudu la EPA Serikali ilang'aka kwa nguvu zote hamna kitu kama hicho hadi Dk Slaa alipotoa evidence ndio wakaanza uchunguzi je wale waliongaka walichukuliwa hatua gani?


Usitake kujidai umetafuta facts zilizokuwa hazina substance tueleze wazi kwamba Dr Idrissa hafai kwasababu zipi na tupe facts venginevyo nyamaza mzee.
 
Mie Dr Idrissa si jamaa yangu wala ndugu hivyo basi msianze another smear campaign but again narudi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!! Mnaevidence kuwa Idrissa hafai kama hamna tunyamaze kimya tuangalia ishu nyengine na sio Competence ya Idrissa it is out of the question
 

Ka hiyo by saying "but i do not think that is only in Tanesco mbona BOT twin towers zimegharimu gharama za kutoa majengo kumi ya PPF towers!!!" unamaanisha ni sawa tu? TANESCO wasisakamwe kwa sababu BOT nao wamefanya?

Uliona moto tuliowawashia BOT hapa?

Two wrongs do not make a right.
 
Nafikiria kujitoa rasmi katika mjadala maana sijaona hoja ya msingi zaidi ya majungu na allegation zisizokuwa na msingi I rest my case!!!!!

Auf Wiedersehen! na majungu mema hatujengi nchi kwa hali hiyo matokeo yake tunapoteza wataalamu wengi kwa sababu tu hatuishi siasa na majungu. Watalaam Wanakimbilia Botswana, Dubai au Europe wanakoheshimiwa na kuthaminiwa.

Mwacheni mzee wa watu ajipumzikie kwa huyu siko pamoja na nyie labda wengineo but si huyu labda baadae maana huwezi binaadaam ana mapungufu yake lazima nimpe benefit of doubt.
 

Yes Ufisadi wa aina yeyote does not justify but The whole country imeoza kusema la ukweli na si Tanesco peke yake. Lakini kwa kumsakama mzee wa watu si fair ukichukulia ameifanyia nchi hii mengi.

Na hata kama tukiassume jamaa fisadi tumtoe yeye who is going to replace him??? na je will it be to the benefit of the company or benefit of some few individuals. Na je tukiwa tunafanya maamuzi hayo tutafika kweli???
 
he is really one of the best na si dhani katika waliopendekezwa anawezatokea kama yeye' ; for sure hatuwezi kujua uzuri wa kitu mpaka tukiwa hatunacho
 
Mimi siwezi kuongelea utendaji wake and all kwa sana.

Lakini shilingi milioni 650 kukarabati nyumba moja ni scandal.

Kama huyu ndiye best CEO tanzania mimi pia naweza kuwa best CEO.
 

- Mkulu Mag3, heshima yako mkuu, hapo tupo ukurasa mmoja sana maswali simple lakini majibu yake ni mazito sana na the whole debate inatakiwa kuishia hapo hapo, unless kuna majibu ya maswali uliyoweka hapo juu!

- Inatia moyo sana kuona JF bado wapo members kama wewe wanaoweza kuuliza maswali magumu ambayo majibu yake yanalenga masilahi ya taifa.

Respect.


FMEs!
 
Wengine tulisema toka mwanzo kuwa CEO yeyote anayeruhusu matumizi maovu kama hayo kwa ajili ukarabati wa nyumba zake katika mazingira ya umaskini uliojikita katika nchi yetu, hatufai! Kiongozi anyepitisha item kama maua ya plastiki katika nchi kama yetu, hatufai. Bottom line ni kuwa ukarabati huu umefanyika under his watch na ni lazima abebe lawama. Uovu kama huu kufanyika kwengine si excuse. Aondoke tu.

Amandla.........
 
imebidi nikujibu kaka!!

Mambo hayako kama hivyo unavyofikiri hasa kwa nchi kama Tanzania.. Unaweza kuwa hard worker lakini watu wakakuslow down. Unapo zungumzia Tanesco usimuangalie Idris rashid pekee yake. Anaweza kuwa mtendaji mzuri lakini wanaomzunguka wanamlet down. Watanzania wengi baada ya kupata elimu kisha kazi nzuri wanachojali ni familia zao basi na si maendeleo ya nchi. Kama una knowledge na umeme unatajua wazi kuwa Tanzania si nchi ya kuwa na matatizo ya umeme iwapo tu watu watakuwa serious na wanachokifanya. Inabidi mentality ya waswahili ibadilike.. chuki, ubinafsi , uvivu na uzembe ukiondoka nchi itandelea na matatizo kama haya yataondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…