TANESCO board split on MD Rashidi's fate


katika financial reporting, hizo zinaitwa "headline figures" na kazi yake ni ku paint picha nzuri
mpaka ma analyst waone full anual report ndio itajulikana ni nini kimefanyika

kama lukule alivyosema hiyo hasara labda ni kutokana na mkataba wa richmond (na yeye ni mmoja wa wafaidika), na kupungua kwa hasara kunatokana na mkataba kusitishwa. kama ni hivyo, basi hiyo siyo kazi yake bali ni wanasiasa

"taifa litaingia gizani kama mitambo isiponunuliwa" kweli the best ceo hana mipango mingine yeyote ya kulinusuru tanesco zaidi ya generator za dowans

je hizo bil 400 kafanyia nini
 
Huna sababu ya kusingizia watu ushallow nenda kwenye hoja straight. Inamaana bei ya umeme imeongezeka kipindi cha Rashid tu? Mbona hatukuona TANESCO inaimarika kipindi cha NET solution au kipindi kingine wakati bei zikipanda?Na hilo ongezeko ukilinganisha na ongezeko la gharama za uendeshaji huoni? Umecheki vizuri aspect za costs na revenue?Au unakimbilia kwenye revenue unasahau expenses nazo huongezeka. Revenue zimeongezeka kutokana na msisitizo wa makusanyo, kuzidi kuwaunganisha watu na kubanya mianya ya upotevu wa pesa. Unaifaham ishu ya kiwanda cha cement, kampuni ya simu na mashirika mengine yaliyokuwa hayalipi ankara zao. Accounting practices kwa Tanzania zimebadilika tokea mwaka 2004 kwahiyo hapo sijaona hoja ya kucritisize performance. Hata zile ambazo on going changes zinakuwa reflected kwene notice za financial statements zinakagulika labda njoo na lingine kwa hapo.
Nadhani unafaham wa accounting km walivyo wengine. Ujanja wa kucapitalised accounting kwa muda wote lazima in the end results zingeonekana. Maana huwezi ukafanya mchezo wa kucapitalise kila mwaka then watu wasikuone. Uje kivingine. Ngoja tukutafutie statements za TANESCo tuargue kwa data.
 

Andrew Chenge alijiuzulu kabla ya kufikishwa mahakani ili kupisha uchunguzi huru ufanyike kwa kosa hili la rada, inakuwa vipi iwe tofauti kwa Rashid?
 

Hasara ya mwaka 2006 haiwezi kuwa inahusiana na mkataba wa Richmond ila inaweza kuwa imeongezeka kutokana na mgawo wa mwaka 2006. Mkataba ulivunjwa mwaka 2007 mwezi Oktoba na hivyo lazima kuangalia hesabu za miaka 2007 na 2007 ili kuweza kujua madhara ya mkataba ule. Mkataba ule umeletaje hasara kwenye shirika? Ninaamini hasara imepungua kutokana na uongozi mpya wa TANESCO kuongeza juhudi za kukusanya madeni na kusafisha vitabu kwa kuondokana na matumizi yasiyofaa na ndio kilichofanyika.

Dr. Rashidi hahusiki na Richmond maana yeye amekuta mkataba tayari umesianiwa na chini ya uongozi wake ndio walivunja mkataba na Dowans baada ya TANESCO kupata ushauri wa kitaalamu kutoka REX attorneys. Kwa hiyo si sahihi kusema Rashidi anahusika na Richmond maana hahusiki kwa njia yeyote ile.

Suala la Dowans limejadiliwa sana na kifupi ni kuwa Rashidi alitaka mitambo ile ili kuongeza uwezo wa TANESCO kuzalisha umeme wake mwenyewe badala ya kununua kutoka kwa wazalishaji kwani hali aliyokuta TANESCO ni ile ambayo nimewahi kuieleza hapa kuwa TANESCO walikuwa wanalipa asilmia 84 ya mapato yao kwa wazalishaji binafsi wa umeme ambao walikuwa wanazalisha asilimia takribani 45 tu ya umeme wote ambao TANESCO walikuwa wanauza kwa wananchi.

mjadala unakuwa mtamu kama tutajikita kwenye facts badala ya maneno ya mtaani na kisha kuyaweka kama facts.

Nimesema kuwa facts mpaka sasa zinaonyesha kuwa amefanya kazi nzuri TANESCO. Sijaona facts zinazoonyesha tofauti. Kama kuna mtu atakaye toa facts hizo za kuonyesha hali ya shirika imekuwa mbaya toka Dr. Rashidi aingine TANESCO nitabadili mawazo. Lakini kwa kufinyangafinyanga maneno hapana.

Tutaweza kuwa fair kwa mtu huyu iwapo tutalitazama shirika kwa miaka 3 ambayo amekuwa pale na kama kuna mafanikio au hapana.

Vitabu vya hesabu za TANESCO vipo wazi
 
Andrew Chenge alijiuzulu kabla ya kufikishwa mahakani ili kupisha uchunguzi huru ufanyike kwa kosa hili la rada, inakuwa vipi iwe tofauti kwa Rashid?

Kaka nimesema pia kuwa tuna viwango tofauti tunavyoweka kwa wanasiasa na watendaji. Nadhani kama kungekuwa na shinikizo kwa Rashidi kama lililokuwepo kwa Chenge angejiuzulu tu.
 
Lukule,

kusema nimekuwa shallow ni kunionea tu. Labda useme ninajengea hoja taarifa ambazo sio sahihi nk. Ripoti za fedha ninazo semea hapa ni ripot zenye nyaraka zote kabisa na zilizochambuliwa na wataalamu. Wakaguzi wa TANESCO ni PwC, ambalo ni shirika lenye heshima kubwa katika kazi ya ukaguzi. Kama wao walikuwa shallow na baadaye CAG naye akawa shallow katika ripoti yake basi nitakubaliana nawe.

Nashauri tujadili kwa hoja sio hisia tu kwa kuwa fulani hampendi mtu fulani.

Nimesema hoja ya Radar na hoja tofauti na sijaona hoja hii imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale TANESCO. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.
 

Gharama zimepungua sana.
Gharama za hovyo hovyo zimeshushwa na zinaendelea kushushwa. Ninadhani nipo priviledged kuwa na taarifa hizo zote. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yanatokana pia na kupunguza gharama. Juhudi za kuongeza mapato zimeongezeka zaidi.

Kumalizika kwa mikataba ya Aggreko na makampuni mengine ya kuzalisha umeme pia kumesaidia. IPTL bado gharama zinalipwa katika escrow account iliyopo Benki Kuu na hivyo bado TANESCO hawajaweza kupunguza gharama hii. Majadiliano na IPTL yakiisha na gharama mpya za capacity charge kuamuliwa, itasaidia zaidi.

Sasa nawe unakosea kuconclude kuwa sijui kama ni gharama au mapato kiasi cha kusema nimekuwa shallow. Jenga hoja yako, sio lazima utumie maneno kama hayo. bring facts na tujadiliane kwa facts kuhusu TANESCO kati ya mwaka 2006 na 2009
 
Kaka nimesema pia kuwa tuna viwango tofauti tunavyoweka kwa wanasiasa na watendaji. Nadhani kama kungekuwa na shinikizo kwa Rashidi kama lililokuwepo kwa Chenge angejiuzulu tu.

mtu unakuwa na scandal huondoki mpaka ushinikizwe.......hizi attitude jamani!!........haya tusubiri hukumu ya mahakama.....possibility ya zile pesa za RADAR kuingizwa kwenye account ya Dr. itakuwa ni kwa ajili ya nini?.......ngoja tusubiri mahakama itatusaidia kutambua hili.......duuhh!!
 

Zitto,
Nakukubali sana pale unapolitetea kwa nguvu zako zote jambo ambalo unaliamini kuwa its right, nakushauri sometimes upime utetezi wako kwa public opinion trend usijefika mahali ukaonekana " An Enemy of The People"

Kwenye hili la Tanesco, mimi binafsi nilikuelewa siku nyingi, haswa kwa kuzingatia wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, tangu lile la mitambo ya Dowans, sasa watu wamefurahi tunameza dozi chungu zaidi ya IPTL, itatuumiza zaidi, lakini imefurahisha watu.

Yes sibishi kuhusu track record yake kwenye utendaji, ila watu bado wanaunganisha na kuchafuka kwa jina lake kwenye hayo mengineyo kiasi kwamba kumtetea nkutaonekana kama kumsafisha.

Ndivyo wanavyoonekana watetezi wa Mkapa ama Lowassa, pamoja na madudu yao, walikuwa na mazuri yao ambayo yanastahili pongezi sio kubezwa, na ukiwapongeza kwa mazuri, unageuka adui, ndiyo hali ya Dr. Rashid hapa.
 

Ni lini watanzania wataamua kuwa objective na kujua kuwa matatizo yetu hayatokani na indivuduals bali mfumo mzima? Hata CEO awe malaika kama mfumo mzima wa uendeshaji shirika kwa kutegemea maamuzi ya wanasiasa hautabadilika hatafika popote. Zitto mwenyewe umesema mapema kuwa mikakati mingi ya Dr Rashid haikuweza kuzaa matunda kwa kuwa mwenye hisa ambaye ni serikali hakutoa funds. Hovyo basi hata kama Tanesco itapata the best CEO around (nami maamini wapo wazuri kuliko Dr Rashid Tanzania sema hawako tayari kufanya kazi ambayo hawatepewa kipimo cha haki) bado kwa mfumo tulio nao tutaendelea kuandika kuhusu matatizo ya Tanesco siku nenda rudi
 
Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.

Mh Zitto, hili unalosema inawezekana ni kweli. Lakini kama tunataka kuangalia performance yake si vema kuangalia vitabu (audited accounts) peke yake. Je Tanesco ilikuwa na objectives gani katika kipindi tunachozungumzia? Were the objectives reasonable? Je wame'achieve' kwa kiasi gani hizo objectives?

Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa kama jana ulitembea km 5 kwa saa na leo ukatembea km 6 kwa saa kwa hakika performance ya leo ni bora kuliko ya jana (as per the audited accounts!). Lakini kama jana uliahidi (targets, objectives) au 'tulitegemea' kuwa leo ungetembea km 20 kwa saa halafu actually ukatembea km 6 kwa saa, then performance yako ni mbovu kabisa!
 


Hoja murua kabisa na nakubaliana na wewe. Tunaanza na hesabu zilizokaguliwa kwanza maana hilo limekuwa tatizo sugu kwa mashirika ya umma Tanzania - mahesabu machafu na hoja za ukaguzi ambazo hazijibiwi kwa miaka mingi.
Halafu tutakuja kwenye je, malengo waliyojiwekea kama shirika miaka 3 iliyopita yamefikiwa kwa kiwango gani? Huu ndio mjadala.
 
Zitto,
Nakukubali sana pale unapolitetea kwa nguvu zako zote jambo ambalo unaliamini kuwa its right, nakushauri sometimes upime utetezi wako kwa public opinion trend usijefika mahali ukaonekana " An Enemy of The People"

Haya kaka, unataka asubuhi niamke niangalie upepo unaelekea wapi ndio na mimi nielekee? Tatizo langu wakati mwingine napenda kuwa devils advocate ili watu wafikiri beyond myths that motivate our orientation in looking into things and make opinion. Najua u devils advocate una nicost haswa. Hata hivyo jamii lazima iwe na watu wanaofikiri tofauti kidogo ili mijadala iwepo. Ikifika siku watu wote tukafikiri sawa itakuwa hatari sana.

Ushauri taken kaka
 
Hapa utaona kupungua kwa Gharama ni kutokana na kuisha kwa Mikataba au kusimamishwa kwa Mikataba mibovu na Sio Efficiency ya CEO.
Angekuwa ni effective sasa hivi tunge isha kuwa na Master Plan ya 5 years, 10 years na 20 years to come.
Kuhusu mwenye hisa kutotoa Fedha za kuwekeza naweza kukubaliana na wewe, lakini yeye akiwa kiongozi wa Shirika hilo akipewa fedha za Kununua Dowans anakubali, badala ya kusema kama ni hizo hela leteni nifanye ninacho ona kina faa, otherwise awaambie kama sivyo siwezi kufanya kazi.
Jingine yeye ni mchumi tena aliye Bobea, sasa mtu unashindwa kuelewa fedha za Mkopo hata kama ni zako, unapowekeza kwenye matumizi ya ukarabati wa nyumba badala ya uzalishaji au vitu vinavyo uhusiana na uzalishaji, kama vipuri, nyaya, nguzo, meter, watu watakuona effectiveness yako ipo chini ya kiwango cha watu wenye busara watakuona unatakiwa kufuata.
 


good points.
kinachonipa tatizo ni jinsi watu walinvyoline up kuchukua nafasi pale TANESCO ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote. Kuna watanzania waturi wasio na mawaa ambao wanweza kufanya kazi nzuri zaidi ya Rashidi. Kwanza Rashidi yupo katika retirement age. Tatizo hao hawapewi nafasi na wanasiasa, narudi na nieleweke, wanasiasa wanataka kujaza sttoges wao katika mashirika.

Angalia Bodi za mashirika zinazoteuliwa miezi hii inayoelekea uchaguzi halafu pima na ujuvi. Wamegoma kata kata kutekeleza hoja ya CAG kuwa wabunge tusiwe kwenye mabodi. Juzi Shamsa kateua kina Ndugai, Seleli katika Bodi ya NGORONGORO. Ndugai ni mhifadhi. Seleli? hata hivyo wote hao kwa kuwa ni wabunge wangepaswa kutokuwa wajumbe. Mbaya zaidi wote Seleli na Ndugai ni wajumbe wa kamati ya Mali Asili ambayo kisera Bodi ya Ngorongoro inawajibika kwayo. Ndugai ndo mwenyekiti. Mzee Misanga yupo bodi ya TPA na wakati huo huo ni mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu.

Jamani - mtanikosa leo siku nzima maana ninasafiri kwenda Trinidad kwenye Commonwealth. So najua kutakuwa na maswali kibao nitajibu nikifika huko.
 

Ni vyote. Angalia hesabu zao.

Master Plan nani kasema hakuna? TANESCO wana masterplan ya mpaka 2037 kuhusu uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Na ni public document wala sio siri.
 
Zitto
Maoni yako mazuri lakini yanafaa darasani na majamvini kama humu tu. Uko kwetu Uswazi hayafai. Dr. Rashidi hawezi kuwa CEO bora unless analinganishwa na ma CEO wachovu. Hakuna nchi yenye ambako ili mtu apawe huduma ya umeme inabidi:-
-Abembeleze power company badala ya kampuni kumbembeleza ili afanye nayo biashara
-Mteja anunue nguzo ya umeme wakati atalipa bill ya umeme
-Mteja atoe rushwa ili apate huduma ya umeme
-Mteja apate hasara ya kuunguziwa vifaa vyake na umeme, akilalamika akatiwe umeme
-CEO atumie milioni 60 kuweka maua na mamazia nyumbani kwake wakati kuna mgawo wa umeme nchi nzima, n.k

Ubora wa CEO huyo uko wapi Zitto? You are not playing devil's advocate, you are blaspheming the public service.
 
Mh Zitto umesema mengi ya msingi sana, cha msingi hapa ni kusema ukweli na kile unachokiamini. hilo tunalikosa kwa viongozi na watendaji wetu ndio maana tunaishia kuamini waandishi na magazeti ambayo nayo siajabu yana upande fulani au yamenunuliwa.

Cha msingi katika mashirika yetu ni kutenganisha siasa na utendaji, hicho ndio cha kwanza kufanyika. mashirika karibu yote hayajui yako wapi, kama alivyosema Zitto kuwa unawweza wauliza NHC thamani ya mali zao hawajui. Kumbe hata haya maubia wanayoingia na wawekezaji kuendeleza prime plot zao wangeweza kujifinance wenyewe na kuwa mmoja ya mashirika makubwa zaidi afrika ya real estate.

Hatuwajibishani ila tunalindana, watendaji hawapimwi kwa walichokifanya ilimradi wanaridhisha wakubwa na wanasiasa. Bila kubadilika tutaishia kulaumiana na kuuza haya machache yaliyobaki. Kumtizamo wangu sioni shirika linalostahili kuyumba kihalali, yote yamemonopoly huduma zake lakini bado yanashindwa!! tujiulize iweje kina Voda, zain etc wawe na nguvu na faida kuliko TTCL!! eti NHC hana hela za kujenga licha ya rent yote na rasilimali zote! POLITICS inauwa; na hata wabunge karibu wote wako kimaslahi binafsi zaaidi
 

Safari njema...

Mie nilitaka kujua huo mkopo wa Bil 400 umetumikaje au ndio wa kununulia Dowans na maua na kutengeneza nyumba ya best CEO
 

Brother kwakuwa ishu hii ipo mahakamani nadhani si vizuri kuichambua zaidi but nadhani kila consultant serikali inatangaza tenda na highest bidder or anayefaa huchaguliwa sasa tutakuja kuta na hapa pana madudu maana siku hizi serikali sio mkandarasi anayefaa anachaguliwa bali ni mkandarasi anayetoa hongo kubwa ndio anayepewa tenda tutakuta hapa pana madudu tusubiri kesi iendelee

Kuhusu Rada nimesema SFO according to their report wamesema Dr Rashid alipokea funds from the company ambayo ilimlipa Chenge pia na yeye ni mdau. Swali lakini laja is it true cause funds zinapotoka katika kampuni kuja katika account yangu zina maelezo ya kutosha kumhakikishia mlipaji ndio maana nikasema tusubiri hatua SFO atakapoitwa mahakamani Dr Rashid ndio ukweli utajulikana venginevyo ni siasa tupu ukweli utajulikana kama inavyodhirihirika ukweli wa Twin Towers kuwa Board ya BOT either ilikuwa haina independence au walikuwa hawajui wanachokifanya.

Mie binafsi sikuiona hio report na ningelifurahi ukituwekea hapa maamuzi yangu huwa yanatoka na kile nachokionahivyo basi kama unayotuwekee tuione.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…