Not surprised,wewe ni delinquent member humuOnve a fool,always a fool.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Not surprised,wewe ni delinquent member humuOnve a fool,always a fool.
Mnaipa tu attention sana lakini kwa nyumba zenyewe ni chache tu hata kuona kwenye hizo picha, huko kilwa mafuriko ya mesomba vijiji lakini kimya sioni taarifa, alafu sijui huko bwawa limesababishaHakuna Mafuriko Makubwa kama Rufiji
Watu 51,000 ndio wameathirikaMnaipa tu attention sana lakini kwa nyumba zenyewe ni chache tu hata kuona kwenye hizo picha, huko kilwa mafuriko ya mesomba vijiji lakini kimya sioni taarifa, alafu sijui huko bwawa limesababisha
Haya mkamsaidie kumjibu mange awaache uchi maana nyote sio wasafi ndio maana mnaogopa sasa nyinyi ni chawa wa vipi muonyesheni mange bwawa, barabara ,hospital na mafuriko yote hayo ni mafanikio ya mama ndani ya miaka mitatu!Mlisema bwawa linachelewa mnataka umeme saizi mnageuka kama Mange 😆😆
Mimi na mambo ya Mange wapi na wapi? Huwa si like Wala ku follow account za kipuuziHaya mkamsaidie kumjibu mange awaache uchi maana nyote sio wasafi ndio maana mnaogopa sasa nyinyi ni chawa wa vipi muonyesheni mange bwawa, barabara ,hospital na mafuriko yote hayo ni mafanikio ya mama ndani ya miaka mitatu!
Alaah huna lolote muoga tu!Mimi na mambo ya Mange wapi na wapi? Huwa si like Wala ku follow account za kipuuzi
Niogope nini sasaAlaah huna lolote muoga tu!
Mwaka 2020 waliathirika wangapi ?, je sasa wangapi wamekosa makazi, alafu nayaongea haya kwasababu nipo nimejionea na siyo nyinyi wa huko kwenye social mediaWatu 51,000 ndio wameathirika
Tuambie wewe walikuwa wangapiMwaka 2020 waliathirika wangapi ?, je sasa wangapi wamekosa makazi, alafu nayaongea haya kwasababu nipo nimejionea na siyo nyinyi wa huko kwenye social media
Katafute ulipo tafutaTuambie wewe walikuwa wangapi
Nimrsikiliza redioni leo, kuwa maji yalikuwa mengi kwenye bwawa,hali iliyohatarisha uhai wa kuta zake, hivyo wakaona njia pekee ni kuyafungulia yatoke nje, hence kilichotokea,walinidanganya sio?Safi sana,kuna watu watasema ni siasa,ika huu ndo ukweli,safi na pongezi kwa mashirika
1. Kwa akili yako elnino hivyo haijawahi kuja Kwa miaka 2023 tangu baada ya Yesu ila Mwaka huu tu?Kwa akili Yako elnino ipo Kila siku?
Huwa siwaamini TANESCO.......kuanzia Richmond,Tegeta escrow ,songas na hili bwawa lao la rufiji...
UFAFANUZI KUHUSU ATHARI ZA MAFURIKO YA KIBITI NA RUFIJI KUHUSISHWA NA UJENZI WA BWAWA LA JULIUS NYERERE (JNHPP)
Alhamisi, 11 Aprili 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu athari za mafuriko yanayoendelea katika maeneo ya Wilaya za Rufiji na Kibiti ambayo yanahusishwa na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).
Tunapenda kuujulisha umma kwamba uwepo wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere umesaidia kwa sehemu kubwa kupunguza athari ya mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla mradi haujajengwa.
Historia ya kitakwimu inaonesha kuwa maeneo ya Rufiji na Kibiti yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kwa miaka mingi ya nyuma kwa kiwango kikubwa kuliko hali ilivyo hivi sasa. Mwezi Mei, 1974 kiwango cha juu cha mafuriko katika mto Rufiji kilifikia mita za ujazo 13,200 kwa sekunde.
Mwaka 1988 kiwango cha mafuriko kilifikia mita za ujazo 8,383.9, mwaka 2016 kiwango cha mafuriko kilifikia mita za ujazo 8,974,7, mwaka 2020 kiwango cha mafuriko kilifikia mita za ujazo 7158.5 na tarehe 15 Februari 2024 kabla ya Bwawa la Julius Nyerere kujaa maji, kiwango cha mafuriko ya maji kilichokuwa kinaingia kwenye Bwawa kilifikia mita za ujazo 8,444 kwa sekunde.
Hata hivyo mafuriko hayo hayakufikia maeneo ya Kibiti na Rufiji kwa sababu Bwawa halikuwa limejaa, kiufupi ni kwamba Bwawa liliendelea kuhimili maji ya mafuriko tokea mwezi Disemba 2022 lilipoanza kujazwa maji mpaka mwishoni mwa mwezi Februari 2024 lilipojaa.
Baada ya Bwawa kujaa, maji ya mafuriko ya Mto Rufiji yaliendelea kupita mtoni kama ilivyo asili yake na hivyo kusababisha mafuriko katika maeneo ya Kibiti na Rufiji jambo ambalo ni la kawaida kwa kila msimu wa mvua kwa mto huu.
Hivyo, kama Mradi wa JNHPP usingejengwa basi maji haya yangefika moja kwa moja kwenye maeneo ya Rufiji na Kibiti na hivyo kusababisha athari kubwa zaidi ya mafuriko na kwa vipindi virefu kuliko tulivyoshuhudia sasa.
Lakini kwa kuwa maji hayo ya mafuriko yalikuwa yakimezwa kwanza na Bwawa la Mradi na kutunzwa kwa muda mrefu, jambo hilo lilisaidia mafuriko kutotokea au kuonekana kwa mapema katika maeneo hayo ya Kibiti na Rufiji.
Ikumbukwe kwamba moja wapo ya sababu ya kuanzishwa Mradi wa Bwawa la kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) katika maeneo ya Rufiji ni kwa sababu ya uwepo wa maji ya mafuriko katika Bonde la Mto Rufiji hali iliyopelekea Serikali kuamua kuyatumia mafuriko hayo ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Kama eneo hilo la Bonde la Mto Rufiji lisingeonekana kuwa na maji mengi ya mafuriko kila mwaka basi hata Serikali isingeamua kuwekeza mradi wa Bwawa katika eneo hilo.
Tunapenda Umma ufahamu kwamba mwaka huu (2024) kumekuwepo na mvua kubwa za El-nino ambazo zimepelekea kuwepo kwa mafuriko makubwa katika maeneo mengi ya nchi yetu ikiwemo maeneo yanayopeleka mtiririko wa maji ya mvua kwenye Bonde la Mto Rufiji.
Hivyo, kiwango kikubwa cha mafuriko katika maeneo hayo ya Kibiti na Rufiji kimesababishwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha.
Sehemu nyingine kumesababishwa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo kutokana na kupanda kwa vina vya bahari, kumekuwepo na upungufu wa spidi ya maji ya mito kuingia baharini hasa wakati maji ya bahari yanapokuwa yamejaa yaani "High Tide".
Hivyo, kwa maelezo yaliyopo kwenye taarifa hii, Shirika la Umeme Tanzania linakanusha taarifa zozote za upotoshaji zinazohusisha Bwawa la Julius Nyerere na mafuriko ya Kibiti na Rufiji na linakemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya Watu wasio na nia njema kubeza juhudi za Serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere.
Shirika linaendelea kuwasihi Wananchi kuwa watulivu na kuendelea kufuatilia taarifa sahihi zinazotolewa na mamlaka husika ili kuendelea kujiweka katika hali ya usalama na kuondoa taharuki isiyo na ulazima.
Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA
TANESCO-MAKAO MAKUU
DODOMA
Mkuu wewe unamlaumu nani katika hili janga, ni serikali ya Samia au marehemu Magufuli?1. Kwa akili yako elnino hivyo haijawahi kuja Kwa miaka 2023 tangu baada ya Yesu ila Mwaka huu tu?
2. Umewahi kuisikia Murphy's law? Au ni kukuruka tu?
3 Hivi mwatuona he nyie? Mwadhani mtaepuka kuwajibijika na janga hili Kwa ujanja ujanja uchwara Kama huu tu; dhidi ya maisha na Mali za watu?
Hivi yale mafuriko ya Arusha nayo yamesababishwa na TANESCO?Haya mkamsaidie kumjibu mange awaache uchi maana nyote sio wasafi ndio maana mnaogopa sasa nyinyi ni chawa wa vipi muonyesheni mange bwawa, barabara ,hospital na mafuriko yote hayo ni mafanikio ya mama ndani ya miaka mitatu!