TANESCO: Dar es Salaam kuanzia leo Februari 23 hakutakuwa na mgawo

TANESCO: Dar es Salaam kuanzia leo Februari 23 hakutakuwa na mgawo

Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema kuwa kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Ijumaa ya Februari 23 hakutakuwa tena na mgao wa umeme. Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha GOOD MORNING kinachorushwa na kituo cha redio cha WASAFI FM asubuhi hii.
Huku Bunju wamechukua muda huu.. saa 3 na dk 48 tarehe 23 Februry 2024
 
Kama huyo msemaji wa TANESCO anadanganya umma wa watanzania basi ikithibitika aondolewe kwenye nafasi hiyo kama yule aliyekuwepo kabla yake. Wa kabla yake na yule wa TPDC waliondolewa na Biteko mwaka jana wakiwa ni waathirika wa mwanzo mwanzo baada ya Biteko kupachikwa u-NWM.
 
Umeme kukatika inaweza kuwa sababu za kawaida tu kwani hata pasipokuwepo na mgao bado umeme hukatika, habari njema ndio hiyo Dsm mgao umeisha atlest feni zituokoe na hili joto.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Watu wanatakiwa wajue hii, sio kila umeme ukikatika ni mgao. Hata wakati wa JPM hakukuwa na mgao ila utakuwa muongo ukisema umeme ulikuwa haukatiki.
 
Lakini kama hiyo haitoshi, kuanzia leo Mkoa wa Dar es Salaam wote utakuwa ukipata nishati ya umeme na hali hiyo tunategemea itaendelea kuwa hiyo siku zinavyozidi kwenda.[emoji848]
Not very sure 100%
 
Sawa na form six wa boarding anapokua likizo na kujiapiza akirudi shuleni hatapiga punyeto Tena.
 
Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema kuwa kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Ijumaa ya Februari 23 hakutakuwa tena na mgao wa umeme.

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha GOOD MORNING kinachorushwa na kituo cha redio cha WASAFI FM asubuhi hii.

===
Tumekuwa tunafanya kazi hii ya kuratibu upatikanaji wa umeme katika maeneo mengi ya nchi yetu bila kutoa upendeleo, lakini kwa kuzingatia kiwango cha umeme ambacho kinazalishwa"

Kuanzia jana usiku (Februari 22, 2024) kuna jitihada kubwa ambazo zinaendelea kufanywa na Serikali pamoja na Shirika kwa ujumla, kuanzia jana usiku maeneo yota ya Kinondoni yamekuwa yanapata nishati ya umeme. Maneno yote ya Temeke yamekuwa yanapata nishati ya umeme, maeneo yote ya Ilala yamekuwa yakipata nishati ya umeme na maeneo yote ya Kigamboni yamekuwa yakipata nishati ya umeme. Maana yangu ni kwamba kuanzia jana usiku, mkoa wa Dar es Salaam wote umekuwa ukipata nishati ya umeme.

Lakini kama hiyo haitoshi, kuanzia leo Mkoa wa Dar es Salaam wote utakuwa ukipata nishati ya umeme na hali hiyo tunategemea itaendelea kuwa hiyo siku zinavyozidi kwenda.

Jitihada kubwa zinaendelea kufanyika kuhakikisha kwamba hali hii inakuwa ya uimarikaji na ya uendelevu kutokuwa na upungufu wa umeme Katika mkoa wa Dar es Salaam lakini pia hali hiyo tutaanza kuiona Siku za hivi karibuni kwenye mikoa mingi, kama siyo yote ya nchi yetu ya Tanzania.
Na ikitokea unakatika, yuko tayari kuachia kiti kwa kutoa ahadi ya uongo?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Na ikitokea unakatika, yuko tayari kuachia kiti kwa kutoa ahadi ya uongo?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Aachie amwachie nani ulishwahi kusikia hio hata siku moja? Ukikatika atakwambia ni matatizo ya kihitirafu za kimiundominu umeme unakosa njia za kuwafikia wananchi Ila umeme uliopo ni mwingi sana mafundi wetu wapo kazini kufanyia marekebisho suala hilo tunatoa pole kwa wateja wetu kwa hali hii iliyotokeza, hutosikia kaachia kiti
 
Hatari

FB_IMG_1708608136838.jpg
 
Back
Top Bottom