TANESCO Hamko serious hata kidogo

TANESCO Hamko serious hata kidogo

Kaka naomba nije kufungua kiwanda changu kidogo cha usindikaji hapo kwako, Mimi nitakuwa shahidi wako namba moja tukiwa pale Kisutu.
 
Hahaha atoe location tuje tufungue frame ya kuuza samaki wabichi na majokofu yetu.
Msisahu kunitag na mimi nilinunua AC nikatumia wiki tu nikalitukana matusi yote, ila kama kuna sehemu imepatikana kidgo na mimi nilitumie wapendwa
 
Mimi mita yangu ya Maji imekwama, inatembea polepole sana nimewarumia Mesg hawajanijibu.

Nimeiacha kumbukumbu. NAJIBWEDEA TU.

Nalipa buku kwa mwezi
 
Nimegundua mita yangu haikati umeme hata unit zikiisha, ni mpya kabisa na imefungwa kwenye nguzo yao ya umeme. Wamefunga mita za nyumba kama 4 kwenye nguzo hiyo, kwahiyo tunatumia vile vi remote ku control.

Sasa baada ya kubaini hitalafu hiyo jana nikaenda kwenye ofisi yao kuripoti, mhudumu niliyemkuta akasema inabidi niandike barua ya malalamiko niombe kubadilishiwa mita.

Nikamuuliza kwani taarifa niliyoileta hajaielewa mpaka niandike barua? Nikamuuliza hajui kama namimi na majukumu mengine, akasema huondio utaratibu.

Nikaondoka zangu. Kwakuwa nimeshatoa taarifa na nilifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuandika jina kwenye daftari la wageni kamwe sitarudi.

Mwisho: macho legevu na umbo kisiwe kigezo cha kuajiri.
Kuna siku utalia tu wewe jifanye kiburi. Kwanini usingeenda kwa meneja?
 
Back
Top Bottom