TANESCO, huku kukata ovyo umeme kutaisha lini?

TANESCO, huku kukata ovyo umeme kutaisha lini?

Ubungo sahivi washakata sijui nalalaje
Usilale na swali moja kichwani mwako, jikung'ute maswali kibao ya msingi, mbona yapo tu mengi?

Utachajije na kuchatije na simu yako hiyo?

Asubuhi hilo birika ama keetel utaiwasha na nini?

Vibaka utawaonaje na kuwadhibiti bila ya taa za security?

Jipige maswali ya kutosha mkuu halafu uje na jibu asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekuaje haya mambo enzi za jiwe hayakuwepo. Mama asiwachekee wahusika awawajibishe tu.
 
Imekuaje haya mambo enzi za jiwe hayakuwepo. Mama asiwachekee wahusika awawajibishe tu.
Mama anamuona Mbowe tu, kama ndio anayemvunjia heshima, haya mengine sijui kwa nini hayaoni kama ni utovu wa heshima kwake na kutokuwajibika na wahusika wanapaswa kachukuliwa hatua, sio kwa kubambikiwa kesi sizizo na ushahidi, la hasha, ushahidi uko wazi!
 
Kwani mkilala mnafunga macho au Yanakua wazi huku mkikoloma na kuota ndoto Pevu?
 
Ondoa matumaini maana hata zile siku 2 za ahadi ya BALD-HEAD ndio zimeshakatika.
 
Kama wananchi wote wamekuwa ma-popomaa wanaona ni halali yao kukatiwa umeme na maji unafikiria serikali au viongozi wataacha starehe zao kushughulikia mambo ya ''kijinga'' kama haya? Kila siku mimi huwa nasema: mbwa tabia yake ni jinsi umleavyo. Na viongozi ni hivyo hivyo. Wananchi wasipokuwa wakali na wenyewe wanastarehe. Hebusiku moja wananchi watoke kwa umoja wao wakiwashe nchi isitawalike hata kwa masaa machache halafu uone kama kutatokea tena ujinga kama huu.
Serikali ya CCM ina monopoly ya kila kitu nchini. Na propaganda kuu inayoendelea ni kuwa wazalendo; kuipenda nchi na viongozi wake; kuiamini na kuiunga mkono serikali. Kuachana na “pinga pinga” hasa CHADEMA.

Certainly, serikali haina haja wala sababu ya kusumbuka na wapiga kelele tupu wanaoishia kuabudu viongozi.
 
Back
Top Bottom