TANESCO inarudi mikononi mwa mafisadi?

Hiyo combination iliyopo sasa ni hatari Sana. huwezi amini zitto ndio wanamtumia kusema
 
Ufisadi haujawai kuisha TANESCO hata awamu ya mwendazake ulikuwepo tena wa kutisha...kila awamu inakuja na MAFISADI wake ila kinachofanyika ni kuwabrain wash WADANGANYIKA kwamba tulikuwa tunaibiwa sana.
Mkuu pamoja na ubaya wote wa mwendazake,Ila kwa Tanesco tutakuwa tunamuonea. Hakukua na kampuni ilifyofilisi Tanesco Kama kipindi Cha Dowans, Richmond, iptl, symbion n.k
Fikiria tu kipindi hicho symbion aliingia mkataba na Tanesco ili kuwauzia umeme milele.
Wanasheria wa Tanesco wanaishauri Tanesco ivunje mkataba na Dowans, alafu haohao wanaenda mahakamani tena kuiwakilisha Dowans.
 
Wewe ndiyo ulikuwa kinara wa kumtukana Magufuli , acha laana iwatafune mtanyooka tu na bado.
 
Ufisadi haujawai kuisha TANESCO hata awamu ya mwendazake ulikuwepo tena wa kutisha...kila awamu inakuja na MAFISADI wake ila kinachofanyika ni kuwabrain wash WADANGANYIKA kwamba tulikuwa tunaibiwa sana.
Ufisadi wote tunaujua toka mkapa Hadi Kikwete haya tuambie wa Magufili.
 
Ufisadi wote tunaujua toka mkapa Hadi Kikwete haya tuambie wa Magufili.
Kuna watu ni wagonjwa wa chuki za kupitiliza kwa JPM. Hata Lissu aliyepigwa risasi yapo mengi ameanza kujua uhalisia wa mambo hasa picha halisi za wanasiasa wengi. Tatizo kubwa la Lissu kwa JPM na alilojitahidi kumrekebisha (ingawa hakuwa na approach rafiki) ni ubabe ambao wakati mwingine unakosa maarifa ya msingi. Ziko vita unaweza kushinda bila kuingia vitani.

Ila ukimpa Lissu nchi leo tofauti yake na JPM ni atatumia sheria halali kunyoosha watu ila Lissu ni aggressive kama JPM! Akiwa Rais hata Chadema wenyewe watachukia kama ilivyotokea kwa CCM dhidi ya JPM.
 
Lisu ni bingwa wa kujipendekeza kama Zito tu wala hawana uaggressive wowote.
 
Ndo hvyo ndugu technically, hata tukisema Hadi tulie, wenye mpini wanafanya yao cc tunaleta jukwaan..two different dimensions..na hakuna wa kuwazuia, unaweza kukuta wanasoma post wanacheka tu
Wewe ni mmoja wao nn Mkuu???
 


That is the fact. Nashangaa mgao umerudi kwa kasi. Tuone aibu kuendelea kuizika Tanesco. Chande Maharage ana kazi kubwa sana ndugu yangu yule. Kivule tutarudi salama kweli? Watanzania wakituchukia ni tatizo
 
Nasema hivi,kwa uelewa wangu hii nchi kuna genge kubwa na la hatari Sana lenye nguvu kubwa kuliko Serikali tunayoijua.Ndilo linaloyumbisha na kufukarisha nchi.Ni mfano wa MAFIA au YAKUZA.Kiongozi pekee aliyethubutu kulishughulikia genge hili na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ni Hayati JPM.Sasa hayupo tena mwenye jeuri hiyo.Wameshika hatamu kwa kasi ya tsunami.Tutarajie maumivu maradufu huko tuendako maana genge hili limepenya kila mahali.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Hao mafisadi wafe tu, kama Mwenye Enzi Mungu anavyo taka maana kachoka na mafisadi uchwara walahi
 
Private sector ilifeli kwenye ATCL Ikafeli kwenye TRC,lakini wacha tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…