TANESCO, Je mnafuta Tariff Zero?

TANESCO, Je mnafuta Tariff Zero?

Achana na hio Bei.. Libya umeme watu walikuwa wanatumia bila kulipa (ingawa walikuwa wanatakiwa kulipa legally lakini haikuwa enforced)..., Na nchi nyingi sana ambazo zina uzalishaji mkubwa wa nishati umeme unakuwa heavily subsidized sababu faida inayopatika indirectly ni maradufu (TANESCO haipo hapo kuhakikisha inakusanya as much money as possible bali kuhakikisha inaprovide affordable electricity kwa kila mwananchi)


Pia tatizo lako unaangalia mambo kwa mafungu na sio kuangalia myororo mzima....

Tanzania nishati ni gharama na nishati ndio inatumika kwenye uzalishaji hivyo nishati kuwa na gharama vitu vyote vinapanda bei (mwananchi analipia maradufu kutokana na uzalishaji usio na ufanisi)

Tanzania ina vyanzo vyote vya kuweza kuzalisha umeme ambavyo havitumiwi to capacity; hence nishati inapotea bure..., nishati hii ikiwa tapped (bwawa tu likimaliziwa to capacity) production itakuwa double..., sasa umeme huu kwanini asitumie mwananchi na pesa yake atumie pengine kuliko pesa yako kutumika kununua dollar ili wewe umletee LPG kutoka nje ya nchi ?
Subiri tufikie huo uwezo wa Libya na hizo nchi tutatumia Bure serikali itagharamia kwa sasa bado
 
Daaah hii inshu imenikumba Sasa itakuaje kama wakitutoa aisee, nilijua ni mistake tu imetokea kumbe kweli aisee ngoja tujipange upya sasa
Hapana inabidi tuwe wakali na sio wewe tu bali kila mtu aweze kulipa kama hio..., sioni kwanini Bwawa linakwisha, tuna gesi asilia, tuna mapaa ya kuzalisha solar n.k., kwanini TANESCO wasitumie hivyo vyanzo na kuhakikisha umeme unakuwa affordable ? Kazi yao sio kutoa GAWIO serikalini bali NISHATI majumbani....
 
Imekuwa ni kawaida kwa wale wateja ambao matumizi yao kwa mwezi ni chini ya 75 units kuwekwa kwenye tariff zero (yaani huyu mtu kwa takribani 9600/= anajipatia units 75); Sasa kuna wadau kama wanne ambao walikuwa kwenye hii Tariff nimesikia wakilalamika ndani ya kama mwezi kwamba wanaondolewa....

Hivyo kabla sijapata taarifa za uhakika siwezi kushutumu kwahio nauliza TANESCO hii ni kweli ?

Na kama ni kweli kwanini mnafanya haya mambo ya ajabu ningewaona wa maana kipindi hiki tunapopigia chapua Nishati safi mgenfanya kila mtu unit ikawa hata chini ya 100/= hapo watu wangepikia majiko ya umeme sababu kwa kufuta hii Tariff nashindwa kuwaelewa mnataka watu waanze kupikia mkaa au kutumia dollar kununua gesi ?

Tafadhali kama ni kweli hizo shutuma please rethink what you are doing....

Kwani haujasikia wanasema wako kwenye maboresho?
Mumewekwa T1.
D1 wamezifuta uchumi mbaya lazima mmyonyoke
 
Wameondoa tayari Tena kimnya kimnya na kipigo juu. Tanesco wamekuwa wezi.
Walipokuwa wanawaambia mtaingiza hizo token kwa mfungu mlifikiri ni maboresho gani?
Hali si nzuri.
 
Subiri tufikie huo uwezo wa Libya na hizo nchi tutatumia Bure serikali itagharamia kwa sasa bado
Moja tuna uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha na vyanzo vya kutosha; pili serikali pesa inatoa wapi kama sio kwa wananchi walewale ? Tatu sasa badala ya kutumia kodi zetu kununua LPG kwanini tusitumie hizo kodi kufanya umeme uwe afrodable watu wapikie ?
 
Hiyo system mkuu ni unaenda wanakuunga au vipi
Kipindi kile ulikuwa unawaambia matumizi yangu ni chini ya 75 units hivyo wanakubadilishia Tariff ila kwa sasa nahisi ni mwendo wa kuwanyofoa wale waliokuwemo unless upo vijijini...
 
Subiri tufikie huo uwezo wa Libya na hizo nchi tutatumia Bure serikali itagharamia kwa sasa bado
Huna hoja kabisa wewe mtu. Nini haja sasa ya kufanya kampeni ya kutumia nishati safi kama hawawezi kupunguza gharama za nishati safi zikawa affodable kwa kila mwananchi? Mwenzako anatoa hoja, wewe umekalia kupinga utadhani hujielewi.

Au unanufaika na uagizwaji wa gesi?
 
Back
Top Bottom