Achana na hio Bei.. Libya umeme watu walikuwa wanatumia bila kulipa (ingawa walikuwa wanatakiwa kulipa legally lakini haikuwa enforced)..., Na nchi nyingi sana ambazo zina uzalishaji mkubwa wa nishati umeme unakuwa heavily subsidized sababu faida inayopatika indirectly ni maradufu (TANESCO haipo hapo kuhakikisha inakusanya as much money as possible bali kuhakikisha inaprovide affordable electricity kwa kila mwananchi)
Pia tatizo lako unaangalia mambo kwa mafungu na sio kuangalia myororo mzima....
Tanzania nishati ni gharama na nishati ndio inatumika kwenye uzalishaji hivyo nishati kuwa na gharama vitu vyote vinapanda bei (mwananchi analipia maradufu kutokana na uzalishaji usio na ufanisi)
Tanzania ina vyanzo vyote vya kuweza kuzalisha umeme ambavyo havitumiwi to capacity; hence nishati inapotea bure..., nishati hii ikiwa tapped (bwawa tu likimaliziwa to capacity) production itakuwa double..., sasa umeme huu kwanini asitumie mwananchi na pesa yake atumie pengine kuliko pesa yako kutumika kununua dollar ili wewe umletee LPG kutoka nje ya nchi ?
Hapana inabidi tuwe wakali na sio wewe tu bali kila mtu aweze kulipa kama hio..., sioni kwanini Bwawa linakwisha, tuna gesi asilia, tuna mapaa ya kuzalisha solar n.k., kwanini TANESCO wasitumie hivyo vyanzo na kuhakikisha umeme unakuwa affordable ? Kazi yao sio kutoa GAWIO serikalini bali NISHATI majumbani....
Imekuwa ni kawaida kwa wale wateja ambao matumizi yao kwa mwezi ni chini ya 75 units kuwekwa kwenye tariff zero (yaani huyu mtu kwa takribani 9600/= anajipatia units 75); Sasa kuna wadau kama wanne ambao walikuwa kwenye hii Tariff nimesikia wakilalamika ndani ya kama mwezi kwamba wanaondolewa....
Hivyo kabla sijapata taarifa za uhakika siwezi kushutumu kwahio nauliza TANESCO hii ni kweli ?
Na kama ni kweli kwanini mnafanya haya mambo ya ajabu ningewaona wa maana kipindi hiki tunapopigia chapua Nishati safi mgenfanya kila mtu unit ikawa hata chini ya 100/= hapo watu wangepikia majiko ya umeme sababu kwa kufuta hii Tariff nashindwa kuwaelewa mnataka watu waanze kupikia mkaa au kutumia dollar kununua gesi ?
Tafadhali kama ni kweli hizo shutuma please rethink what you are doing....
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu. Nishati zilizopo: Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa...
Moja tuna uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha na vyanzo vya kutosha; pili serikali pesa inatoa wapi kama sio kwa wananchi walewale ? Tatu sasa badala ya kutumia kodi zetu kununua LPG kwanini tusitumie hizo kodi kufanya umeme uwe afrodable watu wapikie ?
Kipindi kile ulikuwa unawaambia matumizi yangu ni chini ya 75 units hivyo wanakubadilishia Tariff ila kwa sasa nahisi ni mwendo wa kuwanyofoa wale waliokuwemo unless upo vijijini...
Huna hoja kabisa wewe mtu. Nini haja sasa ya kufanya kampeni ya kutumia nishati safi kama hawawezi kupunguza gharama za nishati safi zikawa affodable kwa kila mwananchi? Mwenzako anatoa hoja, wewe umekalia kupinga utadhani hujielewi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.