TANESCO kuanzisha mkoa maalum kwaajili ya kushughulikia changamoto za umeme katika Reli ya Kisasa (SGR)

TANESCO kuanzisha mkoa maalum kwaajili ya kushughulikia changamoto za umeme katika Reli ya Kisasa (SGR)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema lipo mbioni kuanzisha mkoa maalum wa kiutendaji ili kushughulikia changamoto za umeme katika Reli ya Kisasa (SGR).

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamohanga, amesema hayo leo Machi 26, 2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO).

Kwa mujibu wa Nyamohanga, mpango wa TANESCO ni kuifanya SGR kuwa mkoa maalum wa kiutendaji ili kuhakikisha usambazaji wa umeme unakuwa wa uhakika. Mkoa huo utakuwa na meneja uratibu maalum atakayesimamia mradi huo pamoja na timu maalum ya wataalamu.

Soma Pia: TRC: Treni za SGR zilisimama maeneo matatu tofauti kutokana na hitilafu ya umeme katika Gridi ya Taifa

"Tutakuwa na timu maalum ambayo kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika katika mradi huu," amesema Mhandisi Nyamohanga.

Akizungumzia changamoto za kukatika kwa umeme kwenye SGR, Mhandisi Nyamohanga amesema mradi huo una laini maalum ya umeme, lakini changamoto zilizojitokeza zilihusiana na mfumo mpya uliokuwa ukitumiwa kwa mara ya kwanza.

"Kitu kipya mara nyingi huleta changamoto. Hata hivyo, tunawahakikishia Watanzania kwamba laini hiyo ipo madhubuti na inaendelea kuimarika," amesema.
 
...mada kama hizi ni maji ya shingo kwa chawa na manyumbu ya CHADEMA🤯

Chagua kwa uangalifu na umakini 2025
 
Back
Top Bottom