TANESCO Kuweka nguzo kwenye Kiwanja cha nyumba imekaaje kisheria?

TANESCO Kuweka nguzo kwenye Kiwanja cha nyumba imekaaje kisheria?

Kimbry donee

Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
16
Reaction score
8
Ndugu zangu nisaidieni TANESCO wameweka nguzo ya umeme tena ni ya TRANSFOMA kwenye katikati ya kiwanja cha nyumba . hivi kuna sheria yeyote itakayonisaidia?

Naombeni msaada jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahyo nieende kwa wakili direct nisianzie local government?
Unaanza taratibu, then unapanda as follows: No, waandikie barua ukipinga kuweka nguzo kwenye kiwanja chako... copy peleka wilayani, mkoani, kanda. Majibu watakayokupa ndiyo yatatoa uelekeo wa wapi uende au ufanye
 
kwenye viwanja vyenu mliacha 1.5 m kwa kila mmiliki au nyote mlijenga kwenye mipaka yenu ? Hili ni tatizo kubwa sana nchini sababu kama hizo meters zipo jaribu kuwaambia / kuwashauri kwanini wasiamishe hizo nguzo zao kwenye hilo eneo
 
Tuliacha kabisa sema wezangu walishajenga mimi ndo nilishakusanya tofali so, jamaa wameanza kuweka transfoma kabisa
 
kwenye viwanja vyenu mliacha 1.5 m kwa kila mmiliki au nyote mlijenga kwenye mipaka yenu ? Hili ni tatizo kubwa sana nchini sababu kama hizo meters zipo jaribu kuwaambia / kuwashauri kwanini wasiamishe hizo nguzo zao kwenye hilo eneo
Tuliacha kabisa sema wezangu walishajenga mimi ndo nilishakusanya tofali so, jamaa wameanza kuweka transfoma kabisa.
 
Tuliacha kabisa sema wezangu walishajenga mimi ndo nilishakusanya tofali so, jamaa wameanza kuweka transfoma kabisa.
wahi kuongea nao kabla hawajafika mbali kwahio wenzako walijenga kwenye mipaka bila kuacha 1.5m ? Sababu hizi meter zina maana sana kama moto ukitokea fire iweze kupita au hizo huduma za kijamii kama hizo nguzo ziweze kuwekwa hapo.

sasa wakijenga katikati ya kiwanja chako wewe utajenga wapi? By the way ramani inasemaje kuhusu barabara inapita wapi na viwanja vinaanzia wapi au master plan haujaiona ?
 
Kimbry the donee, Ndiyo ipo Sheria ya umeme Namba 10 ya mwaka 2008. Hasa kifungu cha 34-36 ikisomwa pamoja na Sheria za Ardhi (4 au 5 zote za mwaka 1999 kutegemea na upo Ardhi ya namna gani), sheria ya utwaaji wa Ardhi sura 118, kanuni za mipango miji za mwaka 2018 (G.N 93/2018) hiyo 1.5 M space na jirani HUWA SIO CONSTANT hubadilika kutokana na ukubwa wa kiwanja, na ibara ya 24 ya Katiba ya JMT 1977.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo ipo Sheria ya umeme Namba 10 ya mwaka 2008. Hasa kifungu cha 34-36 ikisomwa pamoja na Sheria za Ardhi (4 au 5 zote za mwaka 1999 kutegemea na upo Ardhi ya namna gani), sheria ya utwaaji wa Ardhi sura 118, kanuni za mipango miji za mwaka 2018 (G.N 93/2018) hiyo 1.5 M space na jirani HUWA SIO CONSTANT hubadilika kutokana na ukubwa wa kiwanja, na ibara ya 24 ya Katiba ya JMT 1977.

Sent using Jamii Forums mobile app
inavyo hyo vpande vya sheria unitymie. plz lkn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahyo nieende kwa wakili direct nisianzie local government?
Kwa mijibu wa mabadiliko ya sheria ya mwenendo wa madai sura 33 (CAP 33 R.E 2019) kifungu cha 64A imeanzisha kitu kinaitwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi (“Conciliation, negotiation and mediation")

Ndiyo, nenda kwa Wakili 1 kwa 1, wakili ndiyo atawaandikia NOTISI YA KUWATAKA WAZINGATIE HAKI ZAKO (i.e DEMAND NOTICE) ndani ya muda fulan (say 7, 14, 21 days etc). Barua ya wakili wataijibu, ila ya kwako bila wakili utakuwa unaandika wala majibu hupewi ya maandishi (labda ya mdomo ambayo nayo hayaridhishi).

Wakili sio kwamba atakimbiliana mahakamani kama mtu anaharisha kuwahi msalani hapana, Mahakama huwa ni njia ya mwisho baada ya njia za diplomasia kushindikana (Last resort).

A good advocate has a duty to the client, duty to the court, duty to the public and duty to the opponent.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu nisaidieni TANESCO wameweka nguzo ya umeme tena ni ya TRANSFOMA kwenye katikati ya kiwanja cha nyumba . hivi kuna sheria yeyote itakayonisaidia?

naombeni msaada jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunashukuru kwa taarifa

Tunakushauri ufike ofisi ya eneo lako kwa utatuzi wa swala hili kwa kuwa uwekaji wa miundombinu unashirikisha viongozi wa maeneo husika na wakazi pia

TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mijibu wa mabadiliko ya sheria ya mwenendo wa madai sura 33 (CAP 33 R.E 2019) kifungu cha 64A imeanzisha kitu kinaitwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi (“Conciliation, negotiation and mediation")

Ndiyo, nenda kwa Wakili 1 kwa 1, wakili ndiyo atawaandikia NOTISI YA KUWATAKA WAZINGATIE HAKI ZAKO (i.e DEMAND NOTICE) ndani ya muda fulan (say 7, 14, 21 days etc). Barua ya wakili wataijibu, ila ya kwako bila wakili utakuwa unaandika wala majibu hupewi ya maandishi (labda ya mdomo ambayo nayo hayaridhishi).

Wakili sio kwamba atakimbiliana mahakamani kama mtu anaharisha kuwahi msalani hapana, Mahakama huwa ni njia ya mwisho baada ya njia za diplomasia kushindikana (Last resort).

A good advocate has a duty to the client, duty to the court, duty to the public and duty to the opponent.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunakushauri kabla ya kwenda mbali sana fika ofisi zetu kwani wewe ni mteja wetu na TANESCO ni mali yako hivyo hakuja kinachoshindakana wala hakuna haja ya case wakati haujatoa lalamiko rasmi

Mfumo upo hivi

Toa lalamiko TANESCO maaumizi yatatolewa kama haukiridhika nenda EWURA, tambua maamuzi ya EWURA ni sawa na maamuzi ya Mahakama kuu, Hivyo badala ya kuingia gharama za wanasheria fata taratibu hizi bura kabisa

HUDUMA KWA WATEJA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tunakushauri ufike ofisi ya eneo lako kwa utatuzi wa swala hili kwa kuwa uwekaji wa miundombinu unashirikisha viongozi wa maeneo husika na wakazi pia

TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongereni #TANESCO kwa kujitahidi kuwa karibu na mitandao ya kijamii. Natumaini huyu ndugu atafuata maelekezo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom