TANESCO Kuweka nguzo kwenye Kiwanja cha nyumba imekaaje kisheria?

Nimependa ulivyo mjibu huyu kiongoz naomba niku PM issue yangu na mm nahisi unaweza kunishauri kitu, linaendana kama hili
 
Peleka malalamiko yako kwa Mkurugenzi wa upimaji na Ramani ya ardhi juu ya hilo jambo. Pia lalamiko lako lijikite kwamba wakati wanafanya upimaji hukupewa taarifa/notisi juu ya hilo suala ambalo limepelekea hayo yote kutokea. Laiti ungepata taarifa na ukahudhuria wakati wa upimaji hakika makosa yasingetokea. Hivyo basi, kosa ni la kwao na siyo lako.

Baada ya kupitia malalamiko yako na kujiridhisha kwamba yana mashiko atatoa amri ya kufanya marekebisho kwani anayo mamlaka kisheria ya kutoa amri ya kufanya marekebisho katika masula ya upimaji na ramani ya Ardhi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…