TANESCO kuzima mfumo wa ununuzi LUKU siku nne (Agosti 22 - 25, 2022)

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Dar es Salaam.

Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya LUKU kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Cliff Maregeli amebainisha hayo leo Jumatano Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku. Amesema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU.

Amewataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa LUKU katika kipindi kilichobainishwa.

"Shirika linashauri wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.

"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi," amesema Maregeli.

Kwa upande wake, Msemaji wa TANESCO, Martin Mwambene amesisitiza kwamba faida kubwa ya matengenezo hayo ni kujihami dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye na matengenezo yakawa makubwa zaidi na kusababisha wananchi kukosa umeme.

"Wananchi wazingatie tu kununua umeme wa kutosha ili waepuke usumbufu unaoweza kujitokeza," amesema Mwambene.

Chanzo: Mwananchi
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limewaomba wananchi kununua umeme mapema kwani linatarajia kufanya maboresho ya mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya luku kuanzia Agosti 22 - 25, 2022.

By Peter Elias

Dar es Salaam. Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Cliff Maregeli amebainisha hayo leo Jumatano Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Amesema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku.

Amewataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa Luku katika kipindi kilichobainishwa.

"Shirika linashauri wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.

"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi,"
 
Yaani kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1asubuhi? Nikiwa na maana kuwa nikinunua umeme kwa njia ya LUKU siku ya tarehe 23 saa 5 asubuhi kutakuwa hakuna tatizo lolote? Huduma nitapata kama kawaida? Au ndo huduma hazitapatikana tena muda wowote kwa hizo siku tajwa!

Msaada tafadhari!
 
1660730480127.png

Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Cliff Maregeli amebainisha hayo leo Jumatano Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Amesema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku.

Amewataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa Luku katika kipindi kilichobainishwa.

"Shirika linashauri wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.

"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi," amesema Maregeli.

Kwa upande wake, Msemaji wa Tanesco, Martin Mwambene amesisitiza kwamba faida kubwa ya matengenezo hayo ni kujihami dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye na matengenezo yakawa makubwa zaidi na kusababisha wananchi kukosa umeme.

"Wananchi wazingatie tu kununua umeme wa kutosha ili waepuke usumbufu unaoweza kujitokeza," amesema Mwambene.
 
Yaani kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1asubuhi? Nikiwa na maana kuwa nikinunua umeme kwa njia ya LUKU siku ya tarehe 23 saa 5 asubuhi kutakuwa hakuna tatizo lolote? Huduma nitapata kama kawaida? Au ndo huduma hazitapatikana tena muda wowote kwa hizo siku tajwa!

Msaada tafadhari!
Wewe mtu_mzito nunua umeme mapema acha kuhoji, kiri kupokea taarifa hiyo sio mjadala.
 
wakusanya takwimu za sensa mjipangee, na power bank manake ya ngoswe tumwachie mitomingi

itakuwa vyema zoezi hili la kuzima likaahirishwa hadi weekend ijayo kupisha Sensa (23/08/2022).
 
Dar es Salaam.

Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya LUKU kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.

Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Cliff Maregeli amebainisha hayo leo Jumatano Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku. Amesema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU.

Amewataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa LUKU katika kipindi kilichobainishwa.

"Shirika linashauri wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.

"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi," amesema Maregeli.

Kwa upande wake, Msemaji wa TANESCO, Martin Mwambene amesisitiza kwamba faida kubwa ya matengenezo hayo ni kujihami dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye na matengenezo yakawa makubwa zaidi na kusababisha wananchi kukosa umeme.

"Wananchi wazingatie tu kununua umeme wa kutosha ili waepuke usumbufu unaoweza kujitokeza," amesema Mwambene.

Chanzo: Mwananchi
Kwahiyo ni mida hiyo tu ya saa nne usiku hadi saa koja asubuhi sivyo? Kwamba katika siku hizo ila nje ya masaa hayo huduma itapatikana? Naomba ufafanuzi
 
Back
Top Bottom