JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
Ni mara ya pili sasa nakutana na gari ya Tanesco ikiwa na kile kibandiko cha mduara kama yai mlango wa dereva na ikiwa imebeba ngazi maeneo ya huku ninakojibanza ikiwa na namba ambazo sio "SU" bali zile za kawaida.
Mara ya kwanza mida ya saa mbili usiku niliiona gari moja eneo ambalo kulikuwa na Transfoma. Nilijua wanaweza wakawa wahalifu wa miundombinu nikajipa moyo kwa kuwa jirani pana kijiwe cha bodaboda. Mara ya pili nikakutana na nyingine ubavuni imeandikwa Tanesco Shinyanga mida hiyo hiyo ya usiku.
Je, imekuwaje hii? Shirika limebinafsishwa!? Au lina changamoto za fedha kiasi cha kukodisha magari ya watu/kampuni binafsi?