TANESCO Mbezi Shule tunaomba mtutendee haki wateja wapya

TANESCO Mbezi Shule tunaomba mtutendee haki wateja wapya

Joined
Dec 15, 2020
Posts
1
Reaction score
0
Nianze kwa kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na watumishi wote wa TANESCO nchini kote bila kuwasahau watumishi wanaotuhakikishia huduma hii ya umeme ipo kwa watumiaji muda mwingi KATIKA ENEO la Mbezi na viunga vyake vyote pokeeni pongezi hizi.

Naendelea kutambua na kuheshimu kazi inayofanyika na sio vyema Sana KULETA malalamiko yangu humu Jambo ambalo najua halileti afya kwa taasisi kubwa Kama TANESCO, niwaombe TU wahusika kutuwahishia huduma ya umeme hakuna sababu ya mtu kulipia umeme mwaka huu akawekewa huduma mwaka ujao wa 2021 ukizingatia watanzania tupo na shauku kubwa ya kuendelea kuchangia mapato ya nchi yetu chonde chonde ndugu zetu TANESCO mtusaidie wateja wenu.

Taratibu za kufuata ili kuweza kupatiwa huduma zipo ila majibu ya watoa huduma yamejikita katika utaratibu na ndio MAANA tunaomba.
 
Tanesco muwe na aibu

Mkuranga Kijiji cha magoza.....mnatesa watu kwakweli

Mnaweka nguzo kwa Watu mnaowataka na kuwapenda....wengine hamna time nao....?!


Naombeni sana mulifanyie kazi hili kwa Haraka
Watu wanahitaji huduma
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Jina. Abdallah

Eneo Kitongoji cha Magoza

Wilaya:Mkuranga

Namba ya simu:0685 467 109

Tatizo:Hakuna Umeme baadhi ya maeneo

Toka lini😀unia kuumbwa

Namba ya taarifa:Sijakuelewa

Ahsante sana
 
Jina. Abdallah

Eneo Kitongoji cha Magoza

Wilaya:Mkuranga

Namba ya simu:0685 467 109

Tatizo:Hakuna Umeme baadhi ya maeneo

Toka lini😀unia kuumbwa

Namba ya taarifa:Sijakuelewa

Ahsante sana
Tunashukuru kwa taarifa

Tunaendelea na jitihada za kusogeza hudyma ya umeme maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkuranga
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tunaendelea na jitihada za kusogeza hudyma ya umeme maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkuranga
Tatizo limekuwa sugu Chief
Watu mpaka rushwa ndio wafanye kazi

Au
Atokee mtu mwenye nafasi mbele yenu ndio msikilize kilio chake kwa haraka


Ombi langu
Mnaposambaza Umeme hakikishine huduma inawafikiwa walengwa kwa muda husika

Na si kupitisha nguzo tu kisha mnakimbia miaka

Tunaomba mlifuatilie hili kwa ukaribu
 
Back
Top Bottom