Tanesco mbona mmezidisha unyonyaji!

Tanesco mbona mmezidisha unyonyaji!

King Kisali

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
1,041
Reaction score
1,349
Hivi hii kampuni kuanza kukata makato ya shilingi 10000 badala ya 1000 ya makato ya kodi ya majengo ina maana gani , maani ni tofauti na agizo la Serikali kuwa kodi ya italipwa majengo kwa makato ya shilingi 1000 kila mwezi kwa miezi kumi, sasa huu utaratibu wa kukata 10000 , na kila mwezi 1000 bila aibu si utapeli huu ?

Na ukinunua umeme chini ya shilingi 10000 haukubali , hivi huu si ni utapeli wa mchana kweupe bila aibu kabisaaa , mafuta juu, tozo za miamala ya simu juu , mafuta ya kula juu kila kitu juu na umeme tena ?
 
Unaionea tu bure tanesco,mulaumu Mwigulu na serikali yake,leo kwa mara ya kwanza nimemkubali mwenyekiti wa SACCOS ya Kaskazini kwenye hotuba yake amesema jambo muhimu sana na somo kwa Mwigulu na January kuhusu tozo na kodi pia kuhusa wanachama wa SACCOS kuwa si lazima wote tufanane au tufuate yale ya SACCOS hata wanaopingana nao waheshimiwe.
 
Kuanzisha uzi na kulialia imekuwa rahisi sana.
 
Makato ni 1000 hata mimi huwa nalipa hivo mjini na kijijini.
Kama unakatwa hivo basi kuna error mahali kwamba nyumba yako inachukuliwa kama jengo la ghorofa kadhaa.
Nafikiri ni busara kwenda ofisini kwao kuliko kulalama nyuma ya keyboard
 
Sio error. Kwa mita mpya unahesabiwa deni tokea mwaka Jana mwezi wa 8. Hivyo mtu akiunganisha umeme Leo anapaswa kulipa miezi 10 iliyopita na ndio inakuja hiyo 10000
Na hata ukija kuunga umeme mwakani, basi jua utakutana na deni la mwaka Jana lililoanza mwezi wa 8
 
Kumbe ni 10000 ya mkupuo mmoja mimi nilijua kila mwezi ndio malipo yake.
Kwa scenario hiyo inawezekana maombi ya kuunga umeme yalipelekwa mwez wa 8 mwaka jana, maana yake nyumba ilikuwepo.
Kama ndivyo ni sahihi maana kodi sio ya ya masuala ya umeme bali ni ya jengo kuwepo
 
Unakatwa deni lote kwa mkupuo mmoja alafu ndio unaanza kukatwa hizo bukubuku
Bado makosa yapo maana hata aliyejenga nyumba mwezi uliopita na mwezi huu akavuta umeme, bado ataapaswa kulipa Kodi ya jengo ya mwaka jana.

Ubaya ni formula iliyowekwa Kama haijafanyia marekebisho basi hata wataojenga 2025 huko watajikuta wanapaswa kulipa Kodi ya tokea 2021.
 
Wana uhakika gani kama jengo lilikuwepo tokea mwezi wa 8?
 
Mkuu soma vizuri, nimesema kama maombi ya kufunga umeme yalifanyika mwezi wa 8 maana yake jengo lilikuwepo huo ni uhakika maana ramani ya wiring iliambatanishwa na surveyor alikuja kuona.
 
Hapo kosa lako ni kuchelewa kujenga, maana yake Kila mtu alitakiwa awe na nyumba mwezi wa 8.
Tunalamba asali.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Unaionea tu bure tanesco,mulaumu Mwigulu na serikali yake,leo kwa mara ya kwanza nimemkubali mwenyekiti wa SACCOS ya Kaskazini kwenye hotuba yake amesema jambo muhimu sana na somo kwa Mwigulu na January kuhusu tozo na kodi pia kuhusa wanachama wa SACCOS kuwa si lazima wote tufanane au tufuate yale ya SACCOS hata wanaopingana nao waheshimiwe.
Hichi wanachokifanya sio haki kabisaaa ,hata kama tuna shida ya kukusanya kodi sio kwa wizi huu ndugu.
 
Makato ni 1000 hata mimi huwa nalipa hivo mjini na kijijini.
Kama unakatwa hivo basi kuna error mahali kwamba nyumba yako inachukuliwa kama jengo la ghorofa kadhaa.
Nafikiri ni busara kwenda ofisini kwao kuliko kulalama nyuma ya keyboard
Hakuna cha errors wala nini inamaana majirani wangu wote wana hiyo errors wote wamekatwa hivyo, maana nimewauliza ,tena mmoja anamita nne kila mpangaji kamuwekea mita yake kote wamekata 10000+1000 =11000 hawana aibu .
 
Mkuu soma vizuri, nimesema kama maombi ya kufunga umeme yalifanyika mwezi wa 8 maana yake jengo lilikuwepo huo ni uhakika maana ramani ya wiring iliambatanishwa na surveyor alikuja kuona.
Sio kweli huu ni wizi ,mimi sikutuma maombi mwezi wa nane , kwahiyo na majirani zangu wote walituma maombi mwezi wa nane.
 
Wana uhakika gani kama jengo lilikuwepo tokea mwezi wa 8?
Mkuu hawa ni matapeli nimeenda kuuliza Tanesco wanasema sio wao nenda TRA nimeenda TRA wanasema andika , nimeandika barua wanasema mpaka makao makuu huku wanaendelea kykata tena kila mwezi .
 
Unaionea tu bure tanesco,mulaumu Mwigulu na serikali yake,leo kwa mara ya kwanza nimemkubali mwenyekiti wa SACCOS ya Kaskazini kwenye hotuba yake amesema jambo muhimu sana na somo kwa Mwigulu na January kuhusu tozo na kodi pia kuhusa wanachama wa SACCOS kuwa si lazima wote tufanane au tufuate yale ya SACCOS hata wanaopingana nao waheshimiwe.
January Makamba mbaya sana , hata aibu hana.
 
Sio kweli huu ni wizi ,mimi sikutuma maombi mwezi wa nane , kwahiyo na majirani zangu wote walituma maombi mwezi wa nane.
Ndio maana nimetumia neno kama, kwasababu hukusema lini ulifanya maombi. Sasa wewe nenda ofisini peleka malalamiko yako, majibu utakayopata ndio yatahitaji mjadala
 
Hakuna cha errors wala nini inamaana majirani wangu wote wana hiyo errors wote wamekatwa hivyo, maana nimewauliza ,tena mmoja anamita nne kila mpangaji kamuwekea mita yake kote wamekata 10000+1000 =11000 hawana aibu .
Huwezi kuichamba serikali mkuu hahaaa eti hawana aibu.
Wewe peleka malalamiko yako upate majibu ya kwanini iko hivo.
Kama wote ni hivyo nafikiri bas kodi hiyo inaanza nyuma kwenye mwaka wa serikali yani mwezi wa 7
Piga vizuri kurudi nyuma utakuta umeanza mwezi wa 7 ndio maana ni 10000 +1000 ya mwez huu kama ulivyoandika
 
Back
Top Bottom