Tanesco mbona mmezidisha unyonyaji!

Tanesco mbona mmezidisha unyonyaji!

Sio error. Kwa mita mpya unahesabiwa deni tokea mwaka Jana mwezi wa 8. Hivyo mtu akiunganisha umeme Leo anapaswa kulipa miezi 10 iliyopita na ndio inakuja hiyo 10000
Na hata ukija kuunga umeme mwakani, basi jua utakutana na deni la mwaka Jana lililoanza mwezi wa 8
Heee! Kazi ipo.

Kwa nini wasiwaanzie mtu anapounganishwa sababu kwa hali hiyo wale wa hali za chini watakaojiunganisha umeme itakuwaje?
 
Mkuu kwa makato hayo wewe humiliki nyumba hiko ni kiwanda.
 
Hivi hii kampuni kuanza kukata makato ya shilingi 10000 badala ya 1000 ya makato ya kodi ya majengo ina maana gani , maani ni tofauti na agizo la Serikali kuwa kodi ya italipwa majengo kwa makato ya shilingi 1000 kila mwezi kwa miezi kumi, sasa huu utaratibu wa kukata 10000 , na kila mwezi 1000 bila aibu si utapeli huu ?

Na ukinunua umeme chini ya shilingi 10000 haukubali , hivi huu si ni utapeli wa mchana kweupe bila aibu kabisaaa , mafuta juu, tozo za miamala ya simu juu , mafuta ya kula juu kila kitu juu na umeme tena ?
Ndugu Mteja

Tunakujulisha kuwa wateja wenye kulipia kodi ya majengo wanakatwa kiasi cha shilingi 1000 kwa nyumba za kawaida au shilingi 5000 kwa nyumba za ghorofa kwa mwezi. Itakumbukwa kuwa makato haya yalianza kutekelezwa kupitia mita za LUKU mwezi wa saba mwaka 2021 ambapo wateja walianza kukatwa mwezi wa nane mwaka 2021 kiasi husika, Aidha kwa wateja ambao hawakuanza kukatwa mapema wamekuwa wakikatwa kiasi halisi ili kutimiza shilingi 12000 (nyumba za kawaida) au 60000 (nyumba za ghorofa) kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mteja mwenye lalamiko au uhitaji wa maelezo ya ziada kuhusu makato haya anashauriwa kuwasiliana na Mamlaka ya Mapato ( TRA) kwa kufika ofisi husika au huduma kwa wateja.
Asante
 
Back
Top Bottom