TANESCO mnatulipa lini malipo ya mradi wa 400 KVA Kinyerezi

mountana

Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
40
Reaction score
6
TANESCO Mmekuja mwanzoni mwa mwezi wa sita mkasema mnatulipa wiki ya mwisho wa mwezi wa sita sasa ni tarehe 6 mwezi wa saba hamjatulipa na tumesubiri toka 2016.

Kama hamtulipi tupeni mamlaka ya kuendeleza maeneo yetu tumechoka, wiki ikiisha sasa wengine tutalilipoti kwa Rais Samia.
 
Nyama hatuzifikii toka 2016 ,ardh ni hazina km hawatulipi tuendeleze maeneo yetu sisi

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Ndio mambo ya serikali ya wanyonge hayo, kuna watumishi wamestaafu miaka minne sasa na mafao yao hawajapewa Wala nini full kuzungushwa.

Serikali inapenda kukusanya pesa lkn ikija kwny kulipa pesa hapo ni bure kabisa.
 
Mkuu fanya udadisi vizuri, unaweza kuta baadhi wachache hasa wenye midomo wameshalamba mshiko, jipange vizuri na wenzio muwape deadline kabla ya kulianzisha......haiwezekani TANESCO pesa zote wanazobambika kwa kuwekea wateja bill kubwa kubwa washindwe kuwalipa fidia...
 
Tupo wengi sana km wananchi 180 hakuna aliyelipwa

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
TANESCO Mmekuja mwanzoni mwa mwezi wa sita mkasema mnatulipa wiki ya mwisho wa mwezi wa sita sasa ni tarehe 6 mwezi wa saba hamjatulipa na tumesubiri toka 2016.

Kama hamtulipi tupeni mamlaka ya kuendeleza maeneo yetu tumechoka, wiki ikiisha sasa wengine tutalilipoti kwa Rais Samia.
Tunapenda kukujulisha kuwa unashauriwa kufika ofisini kwa ajili ya hatua zaidi, swala la madai haiwezi kujibiwa mtandaoni kwa kuwa lina masaliha ya watu

Katibu ofisini kwetu
 
Ngoja waje na majibu yao...

Utasikia, taja eneo, sehemu, mahali, muda na siku ya madai yako...
 
Karibu tukuhudumie, ili kuhudumiwa unapaswa kutoa taarifa kamili bila taarifa utahudumiwaje? Tunawasihi wapendwa wateja wetu kutambua umuhimu wa taarifa hata kwa siri
 
Lipeni madai ya watu basi, tatizo ni nini? kama hamna pesa waruhusuni waendeleze maeneo yao badala ya kuendelea kuwatia ufukara.....
 
Back
Top Bottom